Askari huyu wa Usalama Barabarani anayeongoza magari kwa mbwembwe anafurahisha wengi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,905
2,000
Kuna huyu trafiki anaeongoza magari kwa mbwembwe(huku anachezacheza) anaonekana kuvutia na kufurahisha watu wengi.

Sijui ndio kuipenda kazi yake au laa, ila anachofanya ni kuwafanya watu wengine wanaomuona kupenda kazi zao hata kama wanazifanya katika mazingira magumu kwani anaonesha kuipenda kazi yake.

Ni askari kijana ambaye leo asubuhi yuko Njia Panda ya Kawe akiongoza magari na kufurahisha watumiaji wa barabara lakini pia akitoa hamasa kwa watu kupenda kazi zao ukizingatia mida hii watu ndio wanaenda makazini.

Binafsi nampongeza kwa ubunifu huu unaojenga ari kwa watu wengine kuzipenda kazi zao.

Anafurahisha.

======

Afande Ashraf.jpg
 

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
10,046
2,000
Anaitwa Ashrafu. Dogo anaipenda kazi yake na dancing inamsaidia asichoke

Akikupiga bao wakati mwingine anataka kupiga story tu. Kama ukiwa hata na buku ukimpa anashukuru. Kama huna fresh tu anakuacha uende kiroho safi.

Sometimes wana huwa wanamtip ya ku brash viatu bila issue yoyote
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
57,096
2,000
Kuna wakati alikuwa anakaa njia panda coca mpk daraja la mlalakuwa,alinipiga bao chini nlikuwa na chupa ya mzinga wa nyagi kitu sealed...ni mtu wa kuchekacheka
Aliniambia naona unakwenda kumshusha mikono huyo nkamjibu humo humo

Ova
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom