Askari huyu wa JWTZ akamatwe na kushtakiwa kwa kosa la ujangili

Nakumbuka mwaka 2020 aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla alimtuhumu aliyekuwa Meya wa Iringa kuwa ametenda kosa la ujangili baada ya kupakia picha kwenye mtandao wa Twitter akiwa amemuua nyoka aina ya chatu. Zaidi soma Dtk. Kigwangalla amtuhumu Alex Kimbe kwa ujangili baada ya kuua chatu

Leo nimekutana na video ikimuonesha Askari wa JWTZ akiwa anajinadi kwa kumuua nyoka mkubwa aina ya chatu. Ukimsikiliza vizuri utagundua kwamba nyoka huyo hakuwa katika mazingira ya kuleta madhara yoyote kwa binadamu, ni kwamba alikuwa katika mazingira yake ya maisha ya kila siku. Kitendo cha Askari huyo kumuua bila sababu za msingi si kitu cha kufumbia macho.

Nyoka mkubwa kama yule anachukua muda mrefu kufikia ukubwa ule, na pia anapitia katika mazingira hatari tokea kuanguliwa ikiwa pamoja na kuwindwa na wanyama wengine hatari. Anapoweza kukabiliana na hatari zote mpaka kufikia ukubwa ule ni suala la kushukuru.

Huyu Askari angetumia busara hata kuwaita maafisa wanyama pori waje kumchukua, mnyama kama huyu ni kivutio kikubwa sana cha utalii, anaweza akaleta mapato makubwa sana akiwekwa kwa snake park

BINAFSI CLIP HII YA ASKARI WA JWTZ ILINISIKITISHA SANA, anaona sifa kumwua chatu na wengine wakamwita jasiri hawakujiuliza taifa limepoteza nini kwa sifa za mjeda huyu asiyejitambua
 
Ni hadi ameze mtoto ndipo mseme angemuua. Kumbuka huyo sio kiumbe rafiki hata kidogo na alipokuwepo kuna naingiliano ya karibu na watu. Wewe ni kati ya Ndezi wanaokosoa kila jambo
upo sahihi, lakini angetakiwa awasiliane na askari wa maliasili wangekuja kumchukua na kumhifadhi au kumrudisha katika pori ambalo angekuwa salama
 
upo sahihi, lakini angetakiwa awasiliane na askari wa maliasili wangekuja kumchukua na kumhifadhi au kumrudisha katika pori ambalo angekuwa salama
Halafu "guard" ya usiku ungeenda wewe mkuu? Mtu umeona hatr halafu akaite maliasili?kuna mdau hapo ameeleza kabisa uhatari wa chatu na namna anavyoweza kudhuru halafu mnasema akaite maliasili. Hizi theory za darasani ziacheni wakuu.

Mnaongea tu sababu mnaishi mijini, hivi ingekuwa huyo private ameuliwa na huyo chatu mngesema kitu gani zaidi ya R.I.P?
 
  • Thanks
Reactions: HLM
upo sahihi, lakini angetakiwa awasiliane na askari wa maliasili wangekuja kumchukua na kumhifadhi au kumrudisha katika pori ambalo angekuwa salama
wakati huo anapiga simu na kuchati nao hadi maliasili waanze kuandaa mafuta ya gari huyo nyoka unafikiri angetulia tu kuwasubiri maliasili waje?unafikiri ni kuku yule eeh?umetoa comment ya kitoto kabisa

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
BINAFSI CLIP HII YA ASKARI WA JWTZ ILINISIKITISHA SANA, anaona sifa kumwua chatu na wengine wakamwita jasiri hawakujiuliza taifa limepoteza nini kwa sifa za mjeda huyu asiyejitambua

Taifa halijapoteza chochote.

Huyo chatu angeleta madhara tu kwa watu!
 
Mtoa mada
IMG-20210708-WA0013.jpg
 
Back
Top Bottom