Waafrika hasa hao ( Wamarekani Weusi ) hawajaanza Kuuwawa ( Kuuliwa ) Kinyama na Wazungu ( Wamarekani ) Leo na Sisi huku tukifurahia hii Hukumu ni Kazi bure na wataendelea tu Kuwauwa...
Lakini kwa history ya USA, hii ni hatua kubwa sana kuwahi kutokea, ni mwanzo mzuri!!kwani kila mzungu atakaye fanya hivyo ajue kuwa haki itatendeka , tofauti na zamani hakuna hatua kali inayochukuliwa dhidi yake.lazima achezee si chini ya miaka 40 jela.
 
Waafrika hasa hao ( Wamarekani Weusi ) hawajaanza Kuuwawa ( Kuuliwa ) Kinyama na Wazungu ( Wamarekani ) Leo na Sisi huku tukifurahia hii Hukumu ni Kazi bure na wataendelea tu Kuwauwa....
toa wazo ....tunatokaje hapa tulipo........comment yako imejaa ushupavu bro....na ina afya....
 
Kwenye Kesi Ya G. Floyd My Lord Cahil nasema kwamba Chauvin acted with intent to kill Floyd because he pressed his knee into the man’s neck for several minutes while ignoring repeated cries that he could not breathe, as the widely seen video shows.... Kwenye trial Judgment ya My Lord Peter Cahil J. Anasema Chavin u point a gun and pull the trigger; the law presumes u mean to kill..... u hold ur knee on a man’s neck for this long–the law presumes u mean to suffocate him.
 
Kulikua hakuna umuhimu wa kutumia nguvu katika kumtia nguvuni, nilifuatilia court session hivi uliona chauvin lile goti lake alivyomkandamiza hayati George, goti lilikua limeegemea shingo kwa nguvu kiatu chake kilionekana kilionekana kutogusa eneo la chini, usiwe shabiki bali fuatilia namna hukumu ilitolewa, nimekushangaa kuona unasema hukumu imetoka kuwafurahisha watu weusi, je wewe ulikua eneo la tukio, umesikia utetezi wa mashahidi waliokua eneo la tukio?wewe ni muongo

mkuu msamehe tu bure kuna watu wamejaliwa maneno tu
Ushahidi kesi na hadi hukumu zilikuwa live , CNN, kwa mtu aliyefauatilia ile court session hawezi kuja na arguments shallow kama hii kuwa ati weusi wamependelewa .
 
Kupendeleana kwa watumishi wa vyombo vya dola au vinavyohusika na usimamizi wa sheria ni jambo la kawaida sana duniani. Ndio maana hata wamarekani wamefurahi askari Derek Chauvini kutiwa hatiani

Ila hapa Tanzania it is too much, maana kama haki ingekuwa inatendeka ni viongozi wengi sana wa vyombo vya dola ambao wangekuwa hatiani. Labda kwa kuwafichia makosa watumishi wao au wao kuhusika.

Sasa kama Taifa ambalo linanza kukomaa lazima tuzingatie misingi ya sheria. Kama askari au mtumishi wa vyombo vya dola akiua kwa kuchukua sheria mkononi nae ashitakiwe. Sio kupindisha sheria huku raia wao kila siku wanakamatwa na kusota magerezani
 
Waafrika hasa hao ( Wamarekani Weusi ) hawajaanza Kuuwawa ( Kuuliwa ) Kinyama na Wazungu ( Wamarekani ) Leo na Sisi huku tukifurahia hii Hukumu ni Kazi bure na wataendelea tu Kuwauwa.

Na kinachonishangaza zaidi ni kwamba Sisi Waafrika huku Kwetu 'tumeshupalia' hili 'Sakata' na kuona kuwa ni baya wakati huku huku Kwetu Afrika Waafrika tunauana 'Kinyama' tena 24/7 huku Viongozi ( Marais ) nao 'Wakiua' sana Watu ( hasa Watesi wao ) lakini 'hatushupai' hivi na tunanyama na kuona ni sawa tu

Tatizo Kubwa la Sisi Waafrika ni Unafiki.
Utajisikiaje au utaongea nini siku wamarekani weusi na raia wengine wa ulaya na marekani wakianza kukemea kwa nguvu sana maovu ya afrika kama ugaidi wa boko haram, serikali za kitapeli na Ulafi wa madaraka wa viongozi wa afrika pamoja na kutetea maslahi ya waafrika waishio mazingira magumu barani afrika.

Unahusi utachukizwa na bidii zao kukemea hilo au?!
 
mkuu msamehe tu bure kuna watu wamejaliwa maneno tu
Ushahidi kesi na hadi hukumu zilikuwa live , CNN, kwa mtu aliyefauatilia ile court session hawezi kuja na arguments shallow kama hii kuwa ati weusi wamependelewa .

Nimemshangaa sana
 
Sema nini chief, angekua trump hii kesi ingepindishwa huo ndiyo ukweli, maana trump tangu awali alionyesha dalili za kuwa na upande,
Hakuwa na upande alikuwa anawaambia ukweli mweupe,kwamba issue ya Floyd kuuawa ni kosa na pia kuchoma miji kwa kisingizio cha kudai haki pia ni kosa.Plain and simple bila unafiki..Sasa leo kuna mnafiki liberal pale WH watu wanaona ni mpenda haki sana,yule yupo kwenye system ile ile ya kibaguzi na wala hatachukua hatua yeyote..
 
Wazee wa baraza katika kesi ya mauaji ya mwafrika mmarekani George Floyd wanatarajiwa kurejea mchana huu na majibu ya hatia kwa mashtaka yote matatu.

Derek Chauvin ambae alikuwa askari polisi alimwekea goti shingoni George Floyd kwa dakika tisa na sekunde 29 alipokuwa akimkamata na kusababisha ukosefu wa hewa kwake hali ilompelekea kufariki.

Matarajio ya hukumu ya kukutwa na hatia kwa Wazee hao kunatokana na kutochukua muda mrefu wa kutafakari kila kosa kati ya matatu yanomkabili Derek Chauvin.

Kesi hiyo ya mauaji inafanyikia katika jiji la Minneapolis katika jimbo la Minnesota.

Chauvin anakabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni mauaji ya bila kukusudia katika daraja la pili kosa linalobeba miaka 40 ya kifungo. Kosa la pili ni mauaji kwa kudharau taratibu na kanuni za kazi miaka 25 na kosa la tatu ni linabeba miaka 10 ambalo ni kusababisha kifo kwa kuweka goti kwenye shingo ya George Floyd bila kuzingatia hali ya muathirika.

Chanzo:

Vyanzo mbalimbali vya habari.

Update:

View attachment 1758869
Derek Chauvin akielekezwa kwenda nje ya mahakama akiwa amefungwa pingu mara baada ya kusomewa uamuzi wa kukutwa na hatia ya mauaji ya George Floyd: Picha na Reuters

Derek Chauvin amekutwa na hatia ya mashtaka yote matatu na hukumu itatolewa baada ya wiki nane.

Wazee wa baraza walikaa karibu masaa kumi na nusu kufikiri na kupima uzito wa mashtaka yalowasilishwa na upande wa mashtaka kwenye mahakama na hakimu mkazi ya Hennepin jijini Minneapolis katika kesi hiyo ilochukua wiki tatu.

Chauvin alikuwa akikabiliwa na mashtaka matatu ta kumuua George Floys baada ya kumwekea goti katika shingo yake tarehe 25 mwezi March mwaka 2020, tukio lilozua maandamano nchini Marekani na kuungwa mkono duniani kote.

Chauvin mwenye umri wa miaka 45, anatazama miaka 75 jela ikiwa atatumikia miaka yote iliomo kwenye kila shtaka kwa pamoja.

Ikiwa kila shtaka litatumikiwa kivyake , Chauvin atatumikia kifungo cha miaka 25 jela kwa kila shtaka.
Hili li njagu boya kweli ngoja likanyee debe
 
Back
Top Bottom