Askari aliyeua Iringa hana kosa: Kamuhanda

Mkulima wa Kuku

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
1,270
533
Akihojiwa na Radio One kwa nini asijiuzulu kamanda wa polisi Iringa Kamuhanda alijibu kwa kujiamini kuwa hawezi kujiuzulu kwani alikuwa akitekeleza sheria inayotaka CDM watii sheria bila shuruti. Hii inaweza kuwa na maana kadhaa:
1. Askari aliyeshitakiwa anaonewa kwani alitekeleeza sheria
2. Mwangosi alikuwa akivunja sheria wakati anafanya aliyokuwa akifanya
3. Tume ya Nchimbi ni kiini macho hakuna chochote kitakachofanyika
4. Kufungua matawi ya vyama vya siasa ni kosa kwa mujibu wa sheria anayozungumzia Kamuhanda na atakayefanya hivyo anastahili adhabu ya kifo
5. Sheria za nchi zinaruhusu mauaji ya watu wanaovunja sheria za mikusanyiko kinyume na sheria
6. CHADEMA ijiandae kwa mauaji zaidi na waandishi wajiandae kwa kuuliwa zaidi na jeshi la polisi kwani hawavunji sheria yoyote
7. :.:.........
 
Hii Tanzania bana kwani nani alitegemea haya yasingetokea?
 
Hata mtu ambaye hajasikia hiyo interview anajua moja kwa moja kuwa umeweka chumvi na tafsiri zako ili kupush agenda unayoijua wewe mwenyewe!!!
 
Hata mtu ambaye hajasikia hiyo interview anajua moja kwa moja kuwa umeweka chumvi na tafsiri zako ili kupush agenda unayoijua wewe mwenyewe!!!

Aise kumbe bado upo, umepotea humu kama mwaka hivi ila naona mawazo yako bado ni yale yale.
 
Kuna wakati huwa nashawishika kuamini kuwa huyu mtu alipewa maelekezo maalumu na ndio maana hana hata aibu.iko siku akisikia CHADEMA imeshika dola mtu wa kwanza kula mvua awe huyu afande mla watu.
 
Kuna wakati huwa nashawishika kuamini kuwa huyu mtu alipewa maelekezo maalumu na ndio maana hana hata aibu.iko siku akisikia CHADEMA imeshika dola mtu wa kwanza kula mvua awe huyu afande mla watu.

Wamekulana wenyewe kwa wenyewe...tunasema mbwa kala mbwa! Miaka minne mahabusu,plus miaka 15 aliyohukumiwa,plus unyanyapaa gerezani,plus unynyapaa akirudi mtaani kama atakuwa hai bado, plus hukumu ya mwisho ahera basi nahisi sasa hivi anajuta kwanini alizaliwa!
 
Back
Top Bottom