Askari alewa na kuanza kutishia wapita njia na silaha Arusha

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,619
4,292
Leo asubuhi nimeona kituko cha ajabu sana kuhusiana na askari mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi akiwa lindoni kwenye duka la kubadilishia fedha Snow Crest mtaaa India street akiwa amesimama mlangoni akiwa ameshika bunduki huku amelewa chakari huku anaikok bunduki yake na kuwatishia watu waliokua wanapita, mtaa mzima watu akawa amechanganyikiwa wasijue la kufanya, lakini muda si mrefu wahusika wa pale dukani wakapiga simu kwenye kampuni iliyo muajiri pamoja na polisi wakafika hapo na kumyang'anya ile silaha nakuondoka naye. Pamoja na kunyang'anya silaha hiyo ilikua ni mbinde mpaka jamaa alipozidiwa nguvu. Hayo ndio mambo mseto asubuhi hii jijini Arusha.
 
namsikitikia
mipombe ikiisha akilini
atajikuta lupango na ajira
ndo kwishnehiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
ahaa kumbee nashkuru kwa kunifahamisha
makofia pombe ni noumer asa angemlipua mtu sijui
ingekuwaje?inabidi waajiri waangalie
akili za watu kabla ya kuwapa kazi
za kushika silaha za moto bana
tena huyo atakuwa kala msuba na gongo
bila kuisahau banana wine
 
Huyo askari anawakilisha kile kinachotokea nchini... mambo ndivyo yalivyo

..kwani anatofauti gana na hawa wagawa umeme wa taifa???
 
Du haya mambo yakuchezea maisha ya watu haya,hizo pombe alijua ni maji anakunywa au?na anategemea apeleke mtoto shule kama kdogo anachopata ni pombe 2.
 
Back
Top Bottom