Askari 13 wafukuzwa kazi kwa kuwaingiza gerezani wanawake wacheza utupu kuwaburudisha wafungwa

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
pic+jela.jpg


Sun City. Askari 13 wa Gereza la Sun City nchini Afrika Kusini wamesimamishwa kazi na watachukuliwa hatua zaidi za kinidhamu kwa kosa la kuwaingiza wanawake wacheza utupu gerezani kuwaburudisha wafungwa.

Akina dada hao walikodiwa kwa kazi hiyo maalumu katika hafla rasmi iliyoandaliwa na idara ya huduma ya kurekebisha tabia nchini humo.

Mahabusi walionekana wakiwa wamekumbatiana na akina dada hao na baadhi ya picha kwenye mitandao zikiwaonyesha wanawake hao wakiwapapasa wafungwa sehemu mbalimbali mwilini.

Hata hivyo, Ofisa wa Idara ya Magereza, James Samllberger amesema uchunguzi unafanywa kuhusu tukio hilo.

"Hatuwezi kuvumilia yale ambayo tumeyaona katika mitandao ya kijamii tangu Jumamosi," amesema Smalberger, ambaye ni Kaimu Kamishna wa Idara ya Taifa ya Magereza.

Hafla hiyo iliyoandaliwa 21 Juni ilikuwa sehemu ya maadhimisho ya Mwezi wa Vijana, ambayo ni sehemu ya mpango unaokusudiwa kuwarekebisha tabia wafungwa.

Msemaji wa Idara ya Magereza ya Gauteng, Ofentse Morwane aliliambia gazeti la TimesLive: "Wanenguaji viuno walifika, tuliona walikuwa wanavalia nguo za ndani. Waliandaa igizo kama la kuvua nguo hivi na wahalifu hao."

Picha za wanawake hao wakiwaburudisha wafungwa zilianza kusambaa mitandao ya kijamii wikendi na kusababisha uvumi kwamba huenda labda maisha ni mazuri gerezani kuliko nje ya jela.


Chanzo: Mwananchi
 
Lete habari za ndani na wahusika wa kibiti vingine mpelekee shigongo ndo mdaku
 
Back
Top Bottom