Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,271
Narudia tena mzee Mohamed acha unafiki, ukiwa mzee unafiki ni uchawi.....Gu Dume,
Mimi sina tatizo na kitabu cha Yericko.
Nimemjibu Yericko baada ya kunitaja katika historia ya uhuru wa Tanganyika na Mapinduzi ya Zanzibar na nimeeleza yale ninayoyajua na nyote mmeona.
Watakaokihukumu kitabu chake ni wasomaji.
Kama kuna watu wataamini kuwa Dar es Salaam alikuwapo Sheikh Issa Amiri mimi ninasema kuwa hajapatakuwapo sheikh mwenye jina hilo si Dar es Salaam wala katika historia ya AA na TANU.
Kama Yericko atasema kuwa Kanisa liliunda TANU mimi sina ugomvi na hilo kwani historia ya TANU ilipatapo kuandikwa na Chuo Cha Kivukoni 1981 na hao wenye TANU yao akina Tatu bint Mzee, Sheikh Suleiman Takadir, Idd Faiz Mafungo, Sharifa bint Mzee, Halima Selengia, Idd Tosiri hata makachero wa Special Branch akina Ali Mwinyi Tambwe hawakuwemo kwenye kitabu chao.
Hakuna la ajabu ikiwa itakuja historia ya TANU ya Kanisa iliyoandikwa na Yericko Nyerere.
Wasomaji gani waliokufuata wewe wakakulalamikia juu ya kitabu changu?
Narudia tena, Mohamed hujakisoma kitabu changu, ili uweze kujadili jambo lilolote toka kitabuni ni vema ukakisoma na kuacha chuki za kipuuzi zisizo na maana....