Asiyoyajua Yericko Nyerere katika utafiti wa historia ya Mapinduzi ya Zanzibar

Nshinda,
Yericko ndiyo kaanza sasa kuandika tuna wajibu wa kumtia moyo.
Hii ndio busara na hekima ambayo mzee wangu ulipaswa uanze nayo tangu kule mwanzo, hakika tusinge puuzana kiasi kile...

Nakushukuru sana kwa kurejea mezani pa uungwana, hekima na busara...
 
Yericko,
Mimi siku zote nasahihisha unayokosea katika maandishi yako lakini inakuwia tabu kukubali kuwa umekosea.

Nakupa mfano mmoja tu.

Umekazania kuwa AA iliasisiwa 1927 nimekusahihisha kukuambia kuwa mswada wa Kleist Sykes "Kleist Sykes The Townsman," ambao uko katika kitabu Modern Tanzanians (1973) kilichohaririwa na John Iliffe, Kleist ameandika kuwa AA iliasisiwa 1929.

Hujakubali ukweli huu.
Wewe ushanitukana.

Mimi sijathubutu kufanya hivyo si kwako wala kwa yeyote awaye yule.

"Hili zee."
Lugha yako hiyo ukidhani nitaumia.

Kwangu mimi kuitwa mzee hainisumbui hakika miaka imekwenda February 25 nitakuwa 66 In Shaa Allah.
 
Hii ndio busara na hekima ambayo mzee wangu ulipaswa uanze nayo tangu kule mwanzo, hakika tusinge puuzana kiasi kile...

Nakushukuru sana kwa kurejea mezani pa uungwana, hekima na busara...
Yericko jifunze heshima kwa wazee wetu nina imani mama yetu ajakulea kwenye malezi hayo.
6d7bb98f40aa0adc1cacec8d91772395.jpg
 
Yericko jifunze heshima kwa wazee wetu nina imani mama yetu ajakulea kwenye malezi hayo.
6d7bb98f40aa0adc1cacec8d91772395.jpg
Mama yangu umemleta hapa anahusika na nini katika mjadala huu? Nakuheshimu sana mzee, tujadili mimi na wewe sio kuhusisha mama yangu... Adabu ni jambo zuri
 
Mama yangu umemleta hapa anahusika na nini katika mjadala huu? Nakuheshimu sana mzee, tujadili mimi na wewe sio kuhusisha mama yangu... Adabu ni jambo zuri
Hahaha wewe unapowaita wazee wa wenzio wajinga ulikua unafkiria nini, Mama yetu imewekwa tuu picha yake povu linakutoka lakini unapowatukana wazee wa wenzio unaona raha sana!

Ndio ujue sasa hata hao unao watusi ni wazee wa wenzio,
 
Hahaha wewe unapowaita wazee wa wenzio wajinga ulikua unafkiria nini, Mama yetu imewekwa tuu picha yake povu linakutoka lakini unapowatukana wazee wa wenzio unaona raha sana!

Ndio ujue sasa hata hao unao watusi ni wazee wa wenzio,
Sina haja ya kujibu tna swali lake nafikiri umenisaidia vzuri sna kiongozi maana umemjibu km nilivyokuwa nataka sikuwa na nia ya kumtusi mama yetu nia yngu ilikuwa kumkumbusha tu kuwa awe makini na kauli zake kwa wazee wetu maana ana mzazi pia...
 
Sina haja ya kujibu tna swali lake nafikiri umenisaidia vzuri sna kiongozi maana umemjibu km nilivyokuwa nataka sikuwa na nia ya kumtusi mama yetu nia yngu ilikuwa kumkumbusha tu kuwa awe makini na kauli zake kwa wazee wetu maana ana mzazi pia...

WanaMajlis,
Tusameheane katika hayo yenye kuudhi na kwa kuwa tumewagusa
mama zetu nakuwekeeni hapo chini historia ya Mwami Theresa Ntare
mama yake rafiki yangu Costa Shinganya:

Mchango wa Baadhi ya Machifu Wazalendo katika Harakati za
Kudai Uhuru wa Tanganyika



Mwami Theresa Ntare

(1922 - 1999)

''Chachu,

Hii makala sikuandika mimi mwandishi hataki jina lake litokee lakini siku hiyo ya mazungumzo tulikuwa pamoja ilikuwa November 1992.''
(Kutoka JamiiForums)

Tuliyohadithiwa na Wazee wetu Paramount Chief Dantes Ngua na Mkewe Mwami, Theresa Ntare

Ilikuwa mnamo mwezi wa Novemba 1992, mida ya adhuhuri katika mizuguko ya kuwatembelea wakogwe walioshiriki katika harakati za ukombozi wa Tanganyika kutoka ukoloni wa Waingerza.

Safari yetu ilitufikisha nyumbani kwa Alhajj Chief Abdallah Saidi Fundikira eneo la Magomeni Mikumi, Dar es salaam. Tulipata bahati kubwa kwakuwa tulimkuta Chief Fundikira akiwa na rafiki zake Chief Dantes Ngua na Mhe. Joseph Kasella Bantu pamoja na watu wengine wawili, wakiwa katika mazungumzo ya kawaida. Baada ya kuwasalimia, tulikaribishwa tukaketi.

Mohamed Said hakupoteza muda. Aliwachokoza na maswali yahusuyo mambo muhimu wanayoyakumbuka sana katika enzi za harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika. Wote walitabasamu huku kila mmoja wao akimuangalia Chief Fundikira kana kwamba wakitaka Mzee Fundikira aanze yeye. Mzee Fundikira akasema kuwa yapo mengi ya kuzungumzwa ila muda ule haukuwa wa kutosha kwa sababu alikuwa ameshauriwa asikae muda mwingi pasipo kupumzika. Masharti hayo alipewa na daktari baada ya kutoka katika mtikisiko wa homa. Na hapo tukatambua kuwa wale wazee walienda kumjulia hali baada ya kupata taarifa ya kuumwa kwake.

Hata hivyo, Mzee Fundikira akanyanyuka huku akisema; “Mohammed, ngoja nikuletee zawadi…” Alipanda ghorofani na kurudi na kitabu kidogo cha kurasa 55 kiitwacho, Ukombozi wa Tanganyika kilichoandikwa na Simon Ngh’waya; na kuchapwa na Chief Printer, CCM Printing Press, Dodoma, 1991. Mzee Fundikira akasema, “huyu mwandishi aliniletea mimi hiki kitabu. Nimekipitia na ninaona kitakufaa.” Mzee akaongeza kusema, “Ni vyema watu waandike watakavyoweza kuandika juu ya yale yaliyotokea wakati wa enzi za kudai uhuru.”







Sahhihi ya Chief Abdallah Said Fundikira na ya Mwandishi Simon Ngh'waya


Mwandishi

Baada ya hapo yakafuatia mazungumzo machache tena, ya kuagana tu. Mzee Dantes Ngua akatuambia, “karibuni nyumbani, siyo mbali ni hapo jirani huku akituelekeza na kumalizia njooni, mtanikuta.” Mzee Kasella Bantu yeye alituaga akisema yeye atakuwa tayari kwa mazungumzo siku yoyote tutakayopanga na kwamba tukipita kwa Mzee Fundikira itakuwa rahisi kujua alipo na namna ya kuwasiliana nae.

Hivyo wazee wale walipoondoka nasi hatukuwa na haja ya kumchosha Mzee Fundikira ingawa hakuonyesha dalili ya kutaka tuondoke kwa haraka. Tukamuaga na kuelekea kwa Chief Dantes Ngua.

Wakati tukiwa kwa Chief Fundikira, Mohamed Said alimfahamisha Mzee Ngua kwamba alikuwa akiwafahamu baadhi ya vijana wake ambao baadhi yao wakati ule wakiongoza kampuni ya kuingiza magari kupitia Bandari ya Dar es Salaam. Hiyo ilituongezea ukaribu kwa Mzee Ngua.

Mazungumzo yetu kwa Mzee Ngua hayakuchukuwa muda kuanza. Mzee alianza kwa kutufahamisha kuwa yeye kimila ni Paramount Chief wa Ufipa ambako makabila ya Wafipa wakati huo yalienea kutoka maeneo ya Rukwa hadi kaskazini mwa Zambia ambako wakijulikana pia kama Wawemba. Hivyo yeye alikuwa ni Chief Mkuu (Paramount Chief) wa machifu wadogo, wajumbe na wazee wa koo mbalimbali, wakiongoza katika maenneo yao. Alitujulisha pia kuwa na Mkewe Bibi Theresa Ntare alikuwa Mwami, yaani Chief Mkuu wa kabila la Waha wote waliokuwepo maeneo ya Kigoma hadi katika maeneo ya Burundi. Makao yake makuu kiutawala yalikua Kasulu.

Jinsi Dantes Ngua na Julius Nyerere Walivyokutana kwa Mara ya Kwanza

Chief Dantes Ngua alituhadithia jinsi walivyokutana na Mwlalimu Julius Nyerere kwa mara ya kwanza.
Chief Dantes alisema:

''Wakati huo nilikuwa Mwanafunzi Tabora School mwaka wa pili. Ilikuwa kipindi cha kupokea wanafunzi wapya. Wakati huo pale palikuwa na utaratibu wa kuwathamini watoto wa machifu. Waliorodheshwa na kupewa Head Prefect kiranja wao. Pale shuleni pia wanafunzi walikuwa wakipewa vyakula vya kurutubisha afya; karanga na maziwa. Watoto wa Machfu pia walikuwa wakipata ration (mgao) huo; ila kwao ulikuwa mkubwa kiasi. Hivyo mimi nilikuwa Head Prefect wa wanafunzi ambao ni watoto wa Machifu.

Siku moja wakati wanafunzi wapya wakipokewa pale shule, niliitwa ofisi ya Head Master. Nilipofika nikawakuta wanafunzi wapya wawili. Head Master akaniambia, ‘Hawa ni wanafunzi. Ni watoto wa Machifu.’ Kisha akanitajia majina yao. Mmoja alikuwa ni Julius Nyerere na mwengine Wilbert Chagula.''

Chief Dantes alituambia kuwa yapo matukio mengine muhimu ya kipindi cha mapambano ya kudai uhuru na katika muelekeo wa kupatikana uhuru. Matukio yaliyojaa visa vya wakoloni na vituko vya Nyerere. Mama Theresa alikuwepo pale sebuleni katika yale mazungumzu, bahati mbaya hakuwa akijisikia vizuri. Lakini alikuwa na shauku ya kuzungumza mengi kuhusu jinsi alivyoshiriki mapambano yale ya kudai uhuru wa Tanganyika.

Aliyotuhadithia Mwami Theresa Ntare Jinsi Alivyoipa Nguvu TANU Buha

Mzee Dantes alitushauri tumsikilize Mama Theresa kisha tumpe nafasi akapumzike. “Mama yenu msimuone hivyo, ana mengi sana,” alisema Chief Ngua, na kuongeza, “Tena yeye uhuru ulipopatikana alipewa uwaziri.” Kwa maneno hayo ya sentensi ya mwisho ya Mzee Dantes Ngua, Mwami Theresa akaitikia; “Ah, nikikumbuka yale niliyokumbana nayo katika mapambano ya kudai uhuru wetu na kitendo nilichofanyiwa na kuondolewa uwaziri, ah, basi tu.”

Mwami Theresa hakutaka kuzungumzia kilichomtoa katika uwaziri. Aliamua kutuhadithia kisa cha mpambano wake na maafisa Wazungu wa serikali ya kikoloni kwa ajili ya kuipanguvu TANU ili nchi hii iwe huru:

''Serikali ya kikoloni haikutaka sisi machifu tuwe katika siasa hasa kuisaidia TANU. Hata hivyo tukiwa wananchi na viongozi wa wanchi wanaotaabika chini ya utawala wa kikoloni, tuliiamua kushiriki siasa kwa siri na kuipa nguvu Tanu ili tujitawale. Kuna wakati taarifa zilinifikia kwamba ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulikuwa unakuja kusikiliza maoni ya kudai uhuru. Utaratibu wa kikoloni ni kuwa chama japo ni cha kitaifa, kilitakiwa kipate pia usajili katika kila jimbo. Hivyo TANU ikidai kuwa inawakilisha wananchi wote, watawala wa mikoa walikuwa wajiandaa kukisuta kuwa si kweli na kuonesha sehemu ambako hakikuwa na wanachama. Moja ya sehemu hizo wakoloni waligundua ni katika himaya ya utawala wangu wa Buha. Waligundua TANU haipo kwa Waha. Taarifa za siri zikanifika kwa wakoloni wataiambia tume hiyo ya UNO juu ya hilo. Nikaamua kuchukua hatua kwa siri na kwa haraka.

Nilitoa pesa zangu binafsi na kuagiza haraka kadi za TANU elfu tatu. Zikaletwa kwenye vikapu. Nikaweka mkakati wa siri na watu wangu jinsi ya kuzigawa kadi hizo kwa haraka kwa wananchi wa maeneo ya Buha. Majira ya saa tatu za usiku lilipigwa baragumu la wito wa dharura watu waje kwa Mwami. Wito ulifikishwa kwa haraka kila eneo. Wananchi wakamiminika. Eneo la makazi yangu lilikuwa na uwanja mkubwa sana. Niliwapanga watu wangu katika lango la kuingilia wakiwa na vikapo vilivyokuwa na kadi za TANU na karatasi zake za risiti.

Kila mtu alipoingia alipewa kadi na risiti isiyoandikwa. Kisha akaambiwa aifikiche kadi na hiyo risiti pasipo kuichana. Na asiongee chochote hadi afike lango la nyuma ambalo ni la kutokea. Hapo palikuwepo watu wamejipanga katika meza. Walipofika hapo walimpa huyo aliyekuwepo katika meza hiyo kadi na risiti kisha kumtajia majina yake, anakoishi nk.

Yule karani aliiiandika ile kadi na risiti kwa tarehe za miezi ya nyuma, meza nyingine ilipiga muhuri. Mwisho mwenye kadi aliambiwa kuwamba ameisha kuwa mwanachama wa TANU wa muda mrefu. Akiulizwa atoe kadi na aitetee TANU pasipo kumtaja Mwami wala kilichotokea usiku ule; kwake hicho ni kiapo cha utiifu kwa Mwami. Aliruhusiwa na kusisitizwa kuitunza hiyo kadi na risiti yake.

Mwami Theresa alitufahamisha kuwa zoezi lile lilikamilika mnamo saa tisa za usiku. Meza zikaondolewa na wafanyakazi wakatawanyika na kwenda kulala. Mzee Ngua akasema, “Sisi machifu tulikuwa na utiifu mkubwa toka kwa wananchi. Hata hili tatizo la Ukimwi, kama ingelikuwa enzi zile, tungetoa tamko la muongozo wa kuacha zinaa, Ukimwi ungeishatokomezwa.”

Mwami akaendelea kutuhadithia:

''Ilipofika alfajiri karibu ya saa kumi na mbili za asubuhi, nikaambiwa kuna msafara wa magari ya polisi unaelekea kwenye makazi yangu. Niliyategemea hayo, maana vibaraka wapelelezi walikuwepo enzi hizo. Hata hivyo, kwa tukio lile walikuwa wameshachelewa. Mimi siku ile sikuwa nimelala wala kupata usingizi. Nilikuwa katika nguo zangu za kawaida. Nilipoletewa taarifa ile, nikaingia chumbani na kuwaambia walinzi wangu kuwa wakifika, kwanza kuweni imara kuhusu siri ya kilichotokea usiku.

Pili waambieni kuwa Mwami hajamka. Ngoja tukamwamshe. Kisha mje kunigongea. Na kwamba nitakapotoka na kufokeana nao, nyiye onesheni utiifu kwangu na kuwakasirikia wao; wala msioneshe kuwahofu. Mkakati huo ukaeleweka.''

Mwami Theresa akatueleza kuwa wakaingia maofisa wa polisi akiwemo mmoja Mzungu na DC (District Commissioner) Mzungu pia. Wakauliza kama Mwami yupo. Wakaambiwa amelala, na kwamba wanaenda kumuamsha. Walinzi wa Mwami wakaenda kungonga mlango wake. Baada ya muda akaitikia na kuuliza kwa sauti ya juu, “kunanini mnanigongea usiku huu?” wakamjibu, “kuna Bwana DC na mkubwa wa polisi.” Mwami akajibu kwa sauti kali, “wanataka nini wakati hakujakucha ngoja nije.”

Akatuambia kuwa alijiandaa kwa kuvaa “night dress” akatimua nywele zake kisha akajiviringisha shuka na blanketi akatoka akiwa ameshikilia na alipofika sebuleni na kuwaona hakuwa salimia wala kusubiri salam zao. Alianza kwa kuwafokea kwa lugha ya Kiingereza:

“How dare you wake me up at this time of the hour? Can you do this to the Queen of the UK? Don’t you know I am the the Queen of Buha? Is it because I’m an African that’s why you are doing this to me? I will file my complaints and report you to the Governor for this.”

Mwami akatuhadithia kuwa wale maofisa wa kikoloni walichanganyikiwa na kuanza kujitetea kuwa walipata taarifa kwamba alikuwa akigawa kadi za TANU usiku. Akawajibu, “Je, mmkuja na ‘’search warrant?” Kisha akaongeza kwa kuwaambia, “Nyiye askari wanaume watupu pamoja na DC mmekuja kunipekua mimi mwanamke? Nitamlalamikia Gavana.

Hawakuwa na ‘’search warrant.’’ Mwami akawageukia walinzi wake na kuwataka wawaambie wale DC na mapolisi wake watoke mara moja au wapige baragumu kuashiria Mwami amevamiwa ili waje wamhami. Yule DC na watu wake waliomba radhi haraka na kuondoka.''

Baada ya kutuhadithia kisa hicho Mwami Theresa Ntare alituambia bora turudi pale siku ya Jumamosi iliyofuata kwa mazungumzo na mahojiano zaidi. “Jumamosi mtapata mengi. Maana kuna waandishi Wamarekani watakuja kunihoji kuhusu harakati za wanawake kuhusu kupigania uhuru wa Tanganyika.”

Bahati mbaya hatukuweza kupata fursa ya kwenda siku hiyo. Mwami akasafiri. Na hatukuonana nae tena.
 
Nawatakia kumbukumbu njema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyovikomboa visiwa hivi.
P
Leo tarehe 12 January ni Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, nachukua nafasi hii kuwatakia nyote heri na fanaka za Mapinduzi na kukutakieni maadhimisho mema ya sherehe ya kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa watakao shereheka kwa wale wenye kumbukumbu njema, na kwa vile Mapinduzi Matukufu yale pia yaliandamana na umwagaji damu, natoa pole kwa wenye kumbukumbu chungu.
P
 
Hicho anachoita kitabu wala hakina publisher wala mswada haukusomwa na mhariri yeyote aijuae historia ya mapinduzi ni sawa na mtu aliyejifungia chumbani kwake anaandika katika mtandao wa kijamii.

Yericko hana moja alijualo katika historia ya mapinduzi. Ili kitabu kiwe ni kitabu kinatakiwa kiwe na habari mpya zisizo fahamika.

Huwezi kuungaunga habari walizoandika waandishi wengie ukasema umeandika kitabu.

Anachofanya Yericko ni kunakili yaliyoandikwa na wengine na kisha akayaleta kama fikra zake.

Hicho kichwa chake cha habari kwa haya aliyoandika ameyanakili kutoka kwangu kayabadilisha kidogo tu.

Mwenye maneno hayo ambayo mimi ndipo nilipoyachukua ni Prof. Mohamed Bakari nimemsikia akiyasema kwenye kongamano Kampala mwaka wa 2003 akisema, ‘’Ikiwa sisi hatutoandika historia yetu watakuja watu kutuandikia na huenda tusipendezewe na hayo waliyoandika.’’

Mimi ninapofanya rejea ya maneno hayo humtaja Prof. Mohamed Bakari.


Prof. Mohamed Bakari ofisini kwake Fatih University Istanbul 2015

Yericko angekuwa mjuzi kweli wa historia ya mapinduzi angemtaja kwanza Ali Mwinyi Tambwe aliyetumikia ''Intelligence.'' toka ukoloni hadi uhuru unapatikana 1961 tena akisafiri kueneza TANU na Nyerere bila ya Baba wa Taifa kujua kuwa taarifa zake zote zinafika kwa Gavana.

Yericko anamwaga majina ya kina Mzena ambao wakijulikana sana si mara moja katajwa katika mikasa ya akina Hashil Seif na John Okello.

Ali Mwinyi ndiye kiongozi wa Kambi ya Kipumbwi na ndiye aliyemtia Mohamed

Omari Mkwawa
katika njama ya mapinduzi na kumpa kazi ya kuvusha askari mamluki akifanyakazi chini ya Victor Mkello.


Victor Mkello akiwa nyumbani kwake Nguvumali, Tanga

Vitabu vyote vya historia ya mapinduzi hakuna mwandishi aliyelijua hili.

Yeye Yericko kazi ni yake kukopi tu.

Ghassany
kazungumza na Victor Mkello si mara moja au mbili ilikuwa kazi ya kwenda Tanga na kurudi Muscat, Mkello hakufungua kinywa chake hadi nadhani alipohisi hana siku nyingi za kuishi na hapo alikuwa tayari mguu mmoja ushakatwa.

Mimi nilikuwapo kwenye vikao vyote isipokuwa cha mwisho Mkello alipoamua kueleza ukweli mbele ya mkewe kikao hiki mimi nilitoka nje kuwapa faragha na kumtoa Mkello wasiwasi kwa kuwa Dr. Ghassany yeye mgeni mimi naishi na yeye mji mmoja.

Yericko hana moja alijualo.


Na Dr. Ghassany nyumbani kwake Muscat 1999 alipomfahamisha Mwandishi mradi wa kutafiti historia ya mapinduzi ya Zanzibar ya 1964


Dr. Ghassany na Mzee Mkwawa, Tanga 2003
Mohamed said...bila kujali umri wa yeyote humu mnaita JAMVINI...usikate tamaa kwa wakosoaji wako..andika..andika tu maana jamii forums followers wanajua kazi yako ni..NZURI vumilia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona umeonyesha ulivyofanya kazi ktk ushauribwangu wa pili ilioutumia kama hitimisho langu..
Lkn nimepitia moja baada ya nyingine nimeona bado hujajitendea haki ww mwenyewe na sisi wasomaji.
Ulichofanya ni kidogo kuliko uwezo wako..
Kubwa ulilofanya ni hili la kumshambulia Yericko na kitabu chake kwa kumwita majina yote.

Ushauri na maneno mengine niliyoyaeleza hapo tafadhali yafanyie kazi.
Tuone Tamthilia ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa filam au kwa Audio au kitabu au kwa mashairi n.k

Aufwidersehen!
Wewe unashindwa nini kufanya mawazo yako?

Ulivyoandika umenikumbusha kijana mwanamme handsome, hajaoa, anamuona binti mzuri mwenye sifa zote azipendazo halafu anawafata vijana wenzake wa kiume anawaambia "muoeni huyu binti, Ma shaa Allah" anammwagia sifa zote njema. Kijana mmoja anamuuliza, kwanini usimuoe wewe? Anashindwa kujibu kwa haraka, hakulitegemea swali lile, anapeleka uso kutazama chini, anawaza ajibu nini...

Umeelewa maana yake?

Kwa maandiko yako huna tofauti na huyo kijana, pole sana.

Talk is cheap.
 
Hicho anachoita kitabu wala hakina publisher wala mswada haukusomwa na mhariri yeyote aijuae historia ya mapinduzi ni sawa na mtu aliyejifungia chumbani kwake anaandika katika mtandao wa kijamii.

Yericko hana moja alijualo katika historia ya mapinduzi. Ili kitabu kiwe ni kitabu kinatakiwa kiwe na habari mpya zisizo fahamika.

Huwezi kuungaunga habari walizoandika waandishi wengie ukasema umeandika kitabu.

Anachofanya Yericko ni kunakili yaliyoandikwa na wengine na kisha akayaleta kama fikra zake.

Hicho kichwa chake cha habari kwa haya aliyoandika ameyanakili kutoka kwangu kayabadilisha kidogo tu.

Mwenye maneno hayo ambayo mimi ndipo nilipoyachukua ni Prof. Mohamed Bakari nimemsikia akiyasema kwenye kongamano Kampala mwaka wa 2003 akisema, ‘’Ikiwa sisi hatutoandika historia yetu watakuja watu kutuandikia na huenda tusipendezewe na hayo waliyoandika.’’

Mimi ninapofanya rejea ya maneno hayo humtaja Prof. Mohamed Bakari.


Prof. Mohamed Bakari ofisini kwake Fatih University Istanbul 2015

Yericko angekuwa mjuzi kweli wa historia ya mapinduzi angemtaja kwanza Ali Mwinyi Tambwe aliyetumikia ''Intelligence.'' toka ukoloni hadi uhuru unapatikana 1961 tena akisafiri kueneza TANU na Nyerere bila ya Baba wa Taifa kujua kuwa taarifa zake zote zinafika kwa Gavana.

Yericko anamwaga majina ya kina Mzena ambao wakijulikana sana si mara moja katajwa katika mikasa ya akina Hashil Seif na John Okello.

Ali Mwinyi ndiye kiongozi wa Kambi ya Kipumbwi na ndiye aliyemtia Mohamed

Omari Mkwawa
katika njama ya mapinduzi na kumpa kazi ya kuvusha askari mamluki akifanyakazi chini ya Victor Mkello.


Victor Mkello akiwa nyumbani kwake Nguvumali, Tanga

Vitabu vyote vya historia ya mapinduzi hakuna mwandishi aliyelijua hili.

Yeye Yericko kazi ni yake kukopi tu.

Ghassany
kazungumza na Victor Mkello si mara moja au mbili ilikuwa kazi ya kwenda Tanga na kurudi Muscat, Mkello hakufungua kinywa chake hadi nadhani alipohisi hana siku nyingi za kuishi na hapo alikuwa tayari mguu mmoja ushakatwa.

Mimi nilikuwapo kwenye vikao vyote isipokuwa cha mwisho Mkello alipoamua kueleza ukweli mbele ya mkewe kikao hiki mimi nilitoka nje kuwapa faragha na kumtoa Mkello wasiwasi kwa kuwa Dr. Ghassany yeye mgeni mimi naishi na yeye mji mmoja.

Yericko hana moja alijualo.


Na Dr. Ghassany nyumbani kwake Muscat 1999 alipomfahamisha Mwandishi mradi wa kutafiti historia ya mapinduzi ya Zanzibar ya 1964


Dr. Ghassany na Mzee Mkwawa, Tanga 2003
Bandiko limejaa wivu, Andika na ww
 
Bandiko limejaa wivu, Andika na ww
Anthony,
Nimeandika unaweza ukaangalia hapo chini:

1. PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES
2. The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.
3. The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006
4. Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.
5. Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.
6. Uamuzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.
7. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam.
8. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No.2, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam
9. Dar es Salaam na Wazalendo Wake Mashujaa Katika Kupigani Uhuru wa Tanganyika Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaaam
10. Watu Mashuhuri Katika Kuulingania Uislam Tanzania, Sheikh Ilunga, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam
11. Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam
12. The School Trip to Zanzibar, Africa Proper Education Network 2020, Dar es Salaam
13. In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).
14. Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).
15. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
16. The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).
17. Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).
18. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
19. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
20. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).
21. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).
22. Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).
23. Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.
24. 14. Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.
25. Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.
26. Awards: Several Awards
27. Visiting Scholar: (2011)
28. University of Iowa, Iowa City, USA
29. Northwestern University, Chicago, Illinois, USA
30. Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.
31. OTHER COUNTRIES VISITED
32. Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.
 
Leo tarehe 12 January ni Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, nachukua nafasi hii kuwatakia nyote heri na fanaka za Mapinduzi na kukutakieni maadhimisho mema ya sherehe ya kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa watakao shereheka kwa wale wenye kumbukumbu njema, na kwa vile Mapinduzi Matukufu yale pia yaliandamana na umwagaji damu, natoa pole kwa wenye kumbukumbu chungu.
P
Mzee ms anawatetea waarabu haelewi kabisa mabaya waliyoyafanya hizbu wanashida sana
 
Back
Top Bottom