Asiyejua Historia ni mtumwa!

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
127
Asiyejua historia ni mtumwa! Robert Nest Marley au maarufu kama Bob Marley anasema "if you don't know your history and you will kwow where you came from" Historia ya nchi yetu imepotoshwa sana imetiwa chumvi nyingi sana.

Si zanzibar pekee Historia inapotoshwa hata bara. Mafano kwa makusudi watu wanasema bila ya nyerere Tanzania isingepata uhuru wanaojua historia watakuambieni nyerere alifanya kuingia kwenye chama na kuwakuta kina Abdulwahid Sykes,Shekh Takadir na wengineo yeye hakuwa mwasisi wa harakati. Lakini Historia haisemi hivyo! hazungumzi jinsi Mwalimu alivyowageuka wale aliowakuta! hazungumzii kuhusu Kambona! Nyerere alikuwa anakitu kama uchu wa madaraka!

Kuna watu wanasema Nyerere alimuua Kambona, Nyerere huyo huyo alimuua Edward Moringe Sokoine, Kuna mzee mmoja aliniambia ukikutana na Prof Shaba ukimuuliza kuhusu Sokoine akaweweseka! yeye ndie aliufanyia mwili wake uchunguzi anajua nini kilimkuta Sokoine. Je Wanaoandika Historia wanaandika kwa manufaa ya nani? hivi kweli hakuna wanyekuijua historia wakaiandika? Hakuna wanaujua harakati za kudai uhuru wa Tanganyika wakaandika bila ya upendeleo wa upande wa Mwalimu?Sipingi juhudi za Mwalimu kwenye kuusaka uhuru wa Tanzania ila napinga na historia inaposema bila ya Mwalimu uhuru tusingeupata wakati tunaambiwa Mwalimu alikaribishwa kwenye Chama cha TAA na hao waasisi wa TAA hawatajwi kabisa! Tunaomba wanaJF wenye uweledi wa haya mambo tupe ili nasie tujue tulikotoka tuondokane na utumwa.

Naomba kuwasilisha hoja
 
Haya ni makosa ambayo yako kila nchi na kila eneo la maisha, watu wanalekebisha na kuandika historia kulingana na matakwa yao ya wakati huo kila nchi ina makosa ya aina hii, kila dini ina makosa ya aina hii, ndio maana inabidi kuwatafuta wazee wanaofahamu vizuri historia kabla hawajafa ili watusaidie kuiandika upya.
 
ni kweli kabisa kauli yako kusema jamaa alikuwa na uchu wa madaraka...
na uchu huu kawarithisha mpaka viongiozi hawa wa sasa.
 
Back
Top Bottom