Asiye na dhambi awe wa kwanza kumrushia jiwe Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Asiye na dhambi awe wa kwanza kumrushia jiwe Lowassa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mazoko, Jun 15, 2011.

 1. Mazoko

  Mazoko JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2011
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 676
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ASIYE NADHAMBI AWE WAKWANZA KUMRUSHIA JIWE LOWASSA

  Imenichukua mda kupata tafsili ya neno " kujivua gamba" kwa viongozi wetu wa CCM nimelikosa.Nimsemo unaotumika sasa na viongozi wa CCM baada ya kutoka kwenye kikao cha kukosoana baada yakugundua kuwa walikuwa hawawatendei haki watanzania kwakufuja mali za watanzania.

  Leo hii imekuja sera yakuwatoa kafara watu walioitwa "hawakubariki "kwenye chama mmoja ya watu hao ni Ndugu Edward Lowassa .Kama inavyofahamika kuwa huyu alibeba zigo zima la RICHMOND mitambo ya kuzalisha umeme.Hii ilitokana kuwa yeye alikuwa mtendaji mkubwa serikalini (waziri mkuu wa Tanzania).

  Sina hakika kama kuna gazeti lilishawahi kumwandika kwa mazuri zaidi yakusema kuwa ndiye chanzo kikuu cha kuingiza Taifa kwenye mgogoro wa umeme na kampuni hiyo.Lakini kwaupande wangu nasema mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

  Katika viongozi waliopo katika chama cha mapinduzi (CCM) nadhani hawazidi watano au sita ambao wanaweza kusema wao wako safi na hawajaifikisha Tanzania hapa tulipo.

  Leo hii viongozi wa CCM wanaitana kuambizana achia madaraka kweli!!?? Bila hata aibu? Nikipi hasa cha kuwafukuza wengine na wengine wakabaki kama siunafiki na umbea kuchongeana mbele ya wananchi wengine waonekana hawafai wengine niwazuri.Hii nijambo la ajabu sana hata magazeti kila siku kuandika ubaya wa mtu mmoja wengine hawaguswi kama nichuki binasfi kati yenu na Lowasa nibora kusema.


  Imenilazimu kuandika hivi kama mtanzani mwanachama wa CCM nisiyependa unafiki.Najuwa watasema kuna njia yakuwasilisha malalamiko na si kwanjia hii ya magazeti.Mimi nasema njia hiyo niyaviongozi na sisi wa hali yachini haituhusu maana kama ingekuwa inatuhusu maamuzi mengi yangeletwa kwetu na sisi tutoe maoni yetu. Kwa kuwa kusema ukweli daima ni moja ya imani za chama chetu

  Najaribu kuweka wazi kuwa simfahamu Mheshimiwa Lowasa kwa undani kwa maana kuwa sijawahi kufanyanaye kazi au kukutana naye kwa njia yoyote ile zadi yakukutana naye kwenye utendaji wake wakazi kama Waziri mkuu na mimi kama raia.

  Kinachonisikitisha zaidi nikusoma katika vyombo vya habari kuwa kunasiku aliitwa na viongozi wakuu wa CCM nakumwomba ajivue gamba kwakuwa watu wanamsema vibaya kwa kweli kwa hili walimkosea na wanatakiwa kumwomba samahani kwa kumweka kwenye kundi hili sikwamba hastahiri kuwa huko ila kwa mambo aliyoyafanya kama kiongozi wa kitaifa nimakubwa zaidi ya anayoshutumiwa.

  Wapo wanaostahili kuwajibika kwa kuwa wamelitumbukiza taifa hapa lilipo kwa mfano walioleta hoja ya mrahaba kwenye migodi leo tunakula makapi ya zahabu zahabu yote wanabeba wanapeleka kwao viongozi wanapasenti zao,kuuzwa nyumba za serikali,kulipana posho zisizo stahili,posho za wabunge ambazo niubinafsi,magari yakifahari matumizi makubwa ya serikali,waliouwa viwanda,vyama vya ushirika leo viko taabani na watuhumiwa wapo wanakula raha nchi hii na vitu vingi vinavyo waumiza watanzania .

  Kuna mwasisi waujamaa ambaye kwa uongozi wake enzi za baba wa taifa alitakiwa leo hii awemshauri wa viongozi lakini yeye ndiye wakwanza kulitafuna taifa kupitia familia yake kwenye ukusanyaji ushuru ubungo.Kuna aliyekuwa Rais wa nchi hii tuhuma rukuki amemwagiwa kati ya hizo asilimia sabini sizakweli lakini zilizobaki nizakweli je niatuagani watu hawa wamechukuliwa hatua?Je nawao wanatakiwa kujivua gamba ?

  Hata kashfa ya mkataba wa kuzalisha umeme ya Richmond ambayo inaelekea kuweka msumari wa mwisho katika maisha ya kisiasa ya Lowassa ndani ya CCM, inaelezeka kwamba, nchi ilikuwa inaingia gizani kama ambavyo imekuwa gizani hata baada ya kashfa hiyo. Lowassa kwa nafasi na kawaida yake ya kulazimisha mambo kwa manufaa ya taifa, akafanya maamuzi yanayomgharimu mpaka leo.

  Kisiasa anaweza kujitetea kuwa alikuwa anafanya hivyo ili serikali ya rafiki yake isiaibike mbele ya wapiga kura. Tamko la namna hiyo ni tusi kwa mkuu wa nchi na ndiyo maana zigo hili linamwelemea Lowassa mpaka leo. Anabeba gharama ya kutenda vema kwa njia mbaya. Na huo ndiyo ubaya wa Lowassa kwa mtu mwenye mtizamo endelevu anaweza kumwelewa.

  Tujiulize kama si unafiki nini leo mitambo imewaka Rais wetu yuko mstari wa mbele kuwapokea kwa jina la Symbion hakuna gazeti linalopiga kelele wala wabunge wetu wote wako kimya ,Hata hao viongozi wa CCM hakuna anayehoji kama uhalali wa mitambo hiyo kuuzwa wakati kisheria tulitakiwa kuwanyanganya kutokana na utapeli walioufanya RICHMOND huku kesi iko mahakamani.Inatia aibu kuwa tunaviongozi makini .

  Tufike sehemu viongozi wetu waache unafiki hii yote ni unafiki kama kweli wanataka kujivua gamba waanze na aliyekuwa spika wajamuhuri ya muungano Samweli sitta na mwenzake Spika msaidizi Anna Makinda, Waziri mkuu wa sasa Mizengo Pinda hawa ndiyo wanajuwa ukweli wa RICHMOND na kukatisha mjadala bungeni huku wakiweka chama mbele Taifa nyuma leo ndiyo wanaona uchungu kuwa watanzania hawatendewi haki !? ndiyo wanajivua gamba niunafiki mkubwa huu.

  Hakuna hata kiongozi mmoja leo hii wa CCM ambaye anaweza kusimama na kusema yuko kwa ajili ya watanzania.Haiitaji kwenda chuo wala kumaliza elimu ya msingi ili utambue kuwa maisha nimagu kwa watanzania ambao wanakila kitu,Mito,Maji ,Madini,Aridhi na vitu vingi sana ambavyo leo hii tungekuwa na unafuu wa maisha ila tatizo kubwa niuongozi au mfumo mbovu uliopo.Sasa hawa viongozi watajitoa vipi kwamba wao sigamba na wenzao nimagamba?

  Waache kuzurula na kuhubiri kwa watanzania hasa wa vijijini wasichoweza kukitekeleza kwa kuwa wao pia ni gamba gumu.Ningumu kuelewa viongozi wa CCM wanapata wapi ujasili wakuwavua magamba wengine wakati nchi iko taabani na wao ndiyo wanoongoza dola!!?Turudi nyuma tumwogope mungu tuwatendee haki watanzania tuache unafiki.

  Mwisho kama mhesimiwa Edward Lowassa unasoma makala hii basi nakushauri ugombee urais wapo wananchi tunaotambua uongozi wako na nchi hii inakuitaji.Usijali magazeti yanaandika nini watu wanasema nini kama kweli dhamira yako kweli ilikuwa nikuiondoa Tanzania kwenye giza ila kunawatu waliotumia mwanya huo kukuingiza mtegoni ambao serikali iliyopo imeshindwa kuwachukulia hatua endelea kufanya mikakati yakuingia ikulu.
   
 2. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mh, umetumwa?
   
 3. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Nimesoma lakini sijakuelewa vyema, una maana kuwa wizi ni Ruksa hapa kwetu Tanzania kwa hiyo Lowasa hasilaumiwe au una maana gani?
   
 4. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu when it comes to UFISADI, na kufuja pesa za Jamii hakuna cha mwenye dhambi au asiye na dhambi, ukishikwa lazima uwajibike...
   
 5. S

  Salimia JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Umerukwa na akili wewe!
   
 6. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  hivi ameshatua tok nigeria kwa tb.joshwa?.....
   
 7. N

  Nanu JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tangu Lowassa kujiuzulu, bado nchi iko kwenye mgao?
  Kwanza wakati anajiuzulu mabwawa yalikuwa yamejaa na hivyo wananchi na waheshimiwa wabunge hawakumbuki tena kuwa ni wakati gani hatua hizo zilichukuliwa na taifa lilikuwa linapitia wakati mgumu hasa wa mgao mkali uliokuwa unatishia nchi nzima kuwa giza na wala siyo mgao tena. Lakini kwa sababu zama hizo zilipita na watu hawakumbuki tena, ilikuwa rahisi kuwatoa waliokuwa wanajaribu kuiokoa nchi isiwe gizani kwa sababu tu imeonekana kuwa Waziri Mkuu wakati huo alikuwa anasukuma hilo jambo liende haraka naye alikuwa akisukumwa na rais wake.
  Ni kwa mantiki hiyo Msabaha akasema kama hakutakuwa na sheria ya kushughulikia "emergencies" basi wengi watajiuzulu. Ni kwa mantiki hii hii juzi Januari alimwandikia Ngeleja kuwa anataka kuona 260MW au barua ya kujiuzulu kwa Ngeleja as if yeye ndiye aliyemteua. Ni wabunge hawa hawa ambao muswada wa kushughulikia maswala ya dharura wanapiga dana dana na muswada wenyewe bado haujapitishwa.
  Tutegemee kuwa shutumu viongozi wetu kwa hili lakini bila kuweka nyenzo (sheria) ya kushughulikia dharura tutapiga kelele sana na kila atakayekuwa pale ataogopa kuchukua leading role kwa kuogopa kuwa kama akina Msabaha na Lowassa. Ni ukweli usiopingika kuwa Lowassa hakutajwa kuchukua hata senti moja kwa mkataba wa Richmond na hata Sitta and Slaa kwa nyakati tofauti wamelisema hili.
  Sasa wizi wa Lowassa uko wapi? Kujiuzulu kwake ametimiza demokrasia ya collective responsibility kuwa kwa kuinusuru nchi ili bidi afuatilie hili swala kwa ukaribu zaidi na pia kwa kutimiza matakwa ya bossi wake aliyemwambia sitaki nchi iingie gizani.
  Lakini hili limegeuzwa kuwa siasa za chuki baadaye hasa baada ya REDET kutoa Ripoti kuwa Lowassa ni maarufu kuliko Kikwete na Regina ni maarufu kuliko Salma. Hapa ndipo kiini cha matatizo imeanzia. Kwa Lowassa anabahati hata kuishi mpaka leo maana tunakumbuka yaliyomkuta Ouko wakati wa Moi.
  Tuache kuchafua watu kwa minajili ya kisiasa, penye ukweli tuseme ukweli. Kama Lowassa ni mwizi itakuwa ni kwingine na siyo kwa swala la Richmond. Kama kweli ni mwizi na kuna ushahidi kwanini asikamatwe na kushtakiwa. Lowassa hana kinga ya kushtakiwa kama ana criminal offence!
  Ndiyo maana nasema ukiwa mzuri katika kundi la wabaya utakuwa mbaya wewe. Ukiwa na bidii katika kundi la wavivu utakuwa mbaya na watafanya juu chini utoke waendeleze uvivu na uzembe wao.
  Kinachomgarimu Lowassa ni umaarufu na misimamo yake isiyoyumba hasa pale anapojua anasimamia ukweli!!!!!
  I STILL BELIEVE LOWASSA CAN TAKE THIS COUNTRY TO ANOTHER LEVEL IF HE IS GIVEN THE OPPORTUNITY TO LEAD. Tumeona elimu kwa muda kidogo aliyokaa alivyoongeza literacy ratio mpaka Tanzania tukarudi kwenye nafasu yetu ya juu kama wakati wa mwalimu.
   
 8. CPU

  CPU JF Gold Member

  #8
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hii barua ungeenda kuwasomea chama tawala ambao kwao ndio HAKUNA WA KURUSHIA JIWE Lowassa. Huku kwenye public kuna mawe mengi sana ya kurushiwa, atakufa siku si zake.
   
 9. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Hivi ile mvua ya thailand iliishia wapi?
  Naona agombee labada ile mvua ikitunyeshea tuta pata akili.
   
 10. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,134
  Likes Received: 7,383
  Trophy Points: 280
  Ndo maana yake,jioni anakwenda kudaka kwa EL
   
 11. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,015
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Lazima utakuwa umetumwa wewe.
   
 12. ngamiamzee

  ngamiamzee JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 246
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa ukweli unawekwa wazi hakuna daraja lisillona mwisho sasa watanzania tumeanza kujua ukweli wote tumetumika sana kwa miaka mitano kwa faida ya watu majungu na futina zenu ,udini , kurushana issue ya rechmond walirushana mgawo
   
 13. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  ndo ujue nchi hii mataahila wengi sana! Eeti mvua ya kujaza mabwawa duuu!
   
 14. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #14
  Jun 15, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Dhambi ninazo na jiwe nitarusha
   
 15. youngsharo

  youngsharo JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2015
  Joined: Jan 8, 2015
  Messages: 2,483
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Wanajukwaa,
  Ivi Tanzania si ina maliasi za kutosha? Madini hatuna? Mbuga za wanyama hatuna?

  Hivi Bandari zetu tunafaidika na nini?

  Je ni Lowassa Ndo kachukua hela zote izo?
  Je ni Lowassa ndo kamaliza wanyama wetu?

  so kama kuna mtu ambaye sio fisadi Ccm na awe wa kwanza kumtuhumu Lowassa.
   
 16. Malinyingi

  Malinyingi JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2015
  Joined: Jun 5, 2013
  Messages: 855
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ni Fisadi tu
   
 17. youngsharo

  youngsharo JF-Expert Member

  #17
  Sep 7, 2015
  Joined: Jan 8, 2015
  Messages: 2,483
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  hahahaa na kwenu je?
   
 18. JAMII-ASM

  JAMII-ASM JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2015
  Joined: Jul 30, 2015
  Messages: 1,299
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  usihalalishe dhambi kwa dhambi.
   
 19. hekimatele

  hekimatele JF-Expert Member

  #19
  Sep 7, 2015
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 9,489
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Ha ha ha ha ha ha
  Between the two devils you choose the lesser, so they say.
  I quote
   
 20. JAMII-ASM

  JAMII-ASM JF-Expert Member

  #20
  Sep 7, 2015
  Joined: Jul 30, 2015
  Messages: 1,299
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Better the devil you know...Zimwi likujualo.
   
Loading...