Asiwadanganye mtu, CHADEMA ilionekana tishio sana na mambo inayokabili ni mkakati uliopangwa - hata NCCR Mageuzi wakipanda watakabili hayo hayo!

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Watu wengi wasichoelewa ni kwamba vurugu na mkanganyiko inaoukabili Chadema kwa sasa ilikuwa ni programu maalum iliyopangwa ili kuimaliza Chadema baada ya kuona nguvu za Chadema na kukubalika kwake kwa wananchi kulizidi kuongezeka. Mkakati uliopangwa ilikuwa kutumia kila mbinu ili ikiwezekana kuiondoa kabisa Cahdema katika wigo wa siasa nchini.

Mkakati huu pia ulihusu propaganda dhidi yao, kutia ndani kununua viongozi ambao walitakiwa kuihujumu Chadema wakiwa ndani ya Chadema, mashitaka na kufungwa kwa viongozi, kunyamazishwa Bungeni kwa kila namna, kuzuiwa kufanya mikutano ili wasiongeze ushawishi kwa wananchi, kununuliwa kwa viongozi wake nk. Kuna kila dalili kwamba mbinu mojawapo ilihusu hata kuuwawa kwa viongozi wake!

Katika suala la propaganda, timu za watu ziliandaliwa ili kukosoa na kukashifu kila walichofanya, kutia ndani katika vyombo vya habari na hata mitandao ya jamii. Kuna watu walilipwa kwa kufanya hili. Mkakati ulihusu pia viongozi wa ngazi za wilaya na mkoa kuhusishwa katika kampeni hii. Vyombo vya dola vilitumiwa na watauele wa juu waliambiwa hili wazi.

Kwa mkakati uliopangwa kuimaliza Chadema haingekuwa rahisi kwa chama chochote kupona. Na hili lilifanya iwe rahisi kutokana na udhaifuwa mbalimbali wa kiuongozi ndani ya Chadema. Ksingizio kimojawapo kilichotumiwa ni kwamba Chadema wakichukua nchi wataiuza kwa wageni au kusababisha vurugu nchini kwa kulipiza visasi kwa viongozi waliopita hata maraisi, hivyo lazima wapigwe vita kwa kila namna! Na ilisemwa pia watavunja muungano. Na pia watu waliaminishwa kwamba ni chama cha kijimbo, kitu ambacho toka zamani hata Nyerere alijaribu ku-supress ujimbo huo.

Mbinu nyingine iliyopangwa ilikuwa kuwafanya waonekane hawafai ukilinganishwa na vyama vingine vya siasa, na hususa chama kidogo kilichoonekana hakina nguvu, NCCR, kilitumiwa kufanikisha hili. Na ndio maana nasema wazi kwamba urafiki wa NCCR kwa CCM ni wa kimkakati sana dhidi ya Chadema, na utakuwapo ili mradi NCCR haifikii kuwa tishio kwa chama tawala. NCCR wasidhani kwamba wakianza kuwa na nguvu kama Chadema watabaki kuonwa rafiki wa CCM. James Mbatia anatumiwa bila kujitambua - kama hajatambua hilo.

Nimeamua kuyasema haya kwa kuwa binafsi nachukizwa na mbinu hizi chafu katika siasa za Tanzania. Kama Mtanzania, sina tatizo kuona CCM au Chadema au NCCR nk wakiwa chama tawala, lakini ningependa kuwepo chama cha upinzani nchini chenye kutoa changamoto kwa chama tawala kwa ajili ya kuchochea maendeleo nchini. Kupanga mkakati wa kukimaliza chama kikubwa cha upinzani ni uroho wa madaraka, umasikini mkubwa wa uwezo wa kufikiri, na ukosefu wa uzalendo wa kiwango cha juu kabisa.

Inasikitisha sana kuona kwamba uchanga wa upeo wa kuelewa mambo wa Watanzania wengi unafanya wasione mchezo mchafu unaofanyika dhidi ya Chadema. Huu mkakati mchafu haukuwa dhidi ya Chadema tu, ulikuwa dhidi ya Watanzania wote. Matumaini yangu ni kwamba kuna siku Watanzania wataamka na kuelewa jinsi gani katika nchi yetu kuna watu wanacheza siasa chafu sana kwa faida yao binafsi na si kwa maslahi ya Tanzania
 
Ndio ilionekana tishio kwa usalama wa nchi kama kikundi cha Kigaidi hivi ndio maana inapotezwa kimyakimya isilete mambo ya muslimbrothrhood hapa
 
Siasa ni kuaminika kwa uhalali na ubora wako. Je, walipomkumbatia Lowasa over Wilbroad Slaa aliyekiinua chama walitegemea nini? That was suicidal! CHADEMA inaumizwa na unafiki, ukabila, wizi na IQ mbovu ya viongozi. Wao waliona kura zinakuja na ruzuku itaongezeka na mapato yao yatakuwa makubwa. Wako wapi sasa?

Maprofesa wa kuaminika waliingia wakiamini watatoa uelekeo mzuri wa chama ili kukipa nguvu, wote waliondoka bila kueleza sababu. Sasa leo hii Mbowe awe na maono kuliko hata hao ambao hakuwa hata na sifa za kuwa mwanafunzi wao?

Suala lisiwe kuungwa mkono, iwe ni nani anakuunga mkono? Ukiungwa mkono na wahuni wenzako, kabila lako, unategemea umshawishi nani hadi zitoshe kuchukuwa nchi?
 
Yote hayo ni kudhihirisha kuwa mfumo wa vyama vingi haukutakiwa tangu pale ulipoanzishwa. Wafanye tu turudi kwenye mfumo wa chama kimoja, tuache kuishi uongo.
Hapana Mkuu. Mfumo wa vyama vingi ni jambo zuri sana kwa nchi yetu. Na ukikomaa na kutumika vizuri unakuwa kichocheo kizuri sana kwa maendeleo. Tatizo letu ni kwamba tuliuanzisha bila kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi na wapiga kura. Na pia bado watu wanaojiita viongozi wapo pale kwa faida zao binafsi na sio maendeleo ya nchi.

Ndio maana hawatakubali kukosolewa hata kama wakijua wazi kwamba wanachokosolewa ni kweli kina maslahi kwa taifa, Hawajali kwamba wanavuruga nchi ili mradi tu wanabakia madarakani, na hivyo watafanya lolote kuendelea kuwa madarakani.
 
CHADEMA inaumizwa na ukabila na IQ mbovu ya viongozi.
Chadema ina udhaifu katika uongozi, lakini sidhani kama ukabila ni tatizo lao kubwa. Hayo ni maneno ya propaganda ambayo wengi wameyaamini. Ukiwalaumu Chadema kwa ukabila, basi ni wazi Raisi Magufuli anapaswa pia kulaumiwa kwa kufanya teuzi nyingi kikabila au kikanda, na hata kindugu. Lakini mie nadhani la msingi ni kwamba wanateuliwa watu wenye uwezo, na hilo ndilo jambo linalotakiwa.

Wakati wa enzi za Nyerere, mkurugenzi wa NIC Gibson Mwabulambo, aliwahi kuambiwa kwamba aliajiri watu wengi pale NIC kikabila.- Wanyakyusa. Aliuliza watu wamwonyshe mtu aliyeajiriwa bila kuwa na sifa zilizostahili katika nafasi aliyopewa, na hilo lingethibitisha kama anaajiri kikabila au kwa kuangalia sifa za muajiriwa!
 
CHADEMA inaumizwa na ukabila na IQ mbovu ya viongozi.
Soma hapo juu Mkuu, nimejibu comment kama hii. Nguvu za nje (externa factors) zinazoiangamiza Chadema ni kubwa mara milioni kuliko udhaifu wa ndani, hata kama ingekuwa kweli wana tatizo la ukabila.

Na kama ingekuwa ni ukabila wasingepanda chati hata kidogo. Kwani ukabila wa Chadema, kama kweli upo, umeanza wakati tu Magufuli alipochukua madaraka?
 
Ndio ilionekana tishio kwa usalama wa nchi kama kikundi cha Kigaidi hivi ndio maana inapotezwa kimyakimya isilete mambo ya muslimbrothrhood hapa
Ahaaa, unaona basi? Kwa hiyo ni kweli inapotezwa (japo si kimya kimya) na ni kweli inasemwa inatishia usalama wa nchi? Propaganda mbaya kuliko hata za Hitler.
 
Hapana Mkuu. Mfumo wa vyama vingi ni jambo zuri sana kwa nchi yetu. Na ukikomaa na kutumika vizuri unakuwa kichocheo kizuri sana kwa maendeleo...
Ni kweli huo mfumo ni jambo zuri, tatizo linakuja kwenye ukweli kuwa kila kitu kinachokuwepo kina "conditions" zake. Kwa habari hii conditions ni mbili: 1) utashi na 2) uwezo wa wananchi kuupigania mfumo.

Ndiyo tunarudi kwenye point zako kuwa walioko kwenye mamlaka wanatumia utashi wao kuhakikisha mfumo hauleti faida inayotarajiwa, na wananchi bado hawajafikia level ya kuweza kupigania mfumo usimame.

Matokeo yake wananchi wanabaki kama victims of the circumstances ambapo misigano inayotokea inabaki kuwa ni hasara kwao, huku kwa muda mwingi nchi ikiacha kushughulika na mambo ya maana ya kuipeleka mbele.

Nakubali kuwa kwenye single party system hakuna faida zaidi itakayokuwepo lakini wananchi watakapoamka mambo yatabadilika "genuinely".
 
Ni kweli huo mfumo ni jambo zuri, tatizo linakuja kwenye ukweli kuwa kila kitu kinachokuwepo kina "conditions" zake. Kwa habari hii conditions ni mbili: 1) utashi na 2) uwezo wa wananchi kuupigania mfumo. Ndiyo tunarudi kwenye point zako kuwa walioko kwenye mamlaka wanatumia utashi wao kuhakikisha mfumo hauleti faida inayotarajiwa, na wananchi bado hawajafikia level ya kuweza kupigania mfumo usimame. Matokeo yake wananchi wanabaki kama victims of the circumstances ambapo misigano inayotokea inabaki kuwa ni hasara kwao, huku kwa muda mwingi nchi ikiacha kushughulika na mambo ya maana ya kuipeleka mbele.
Mkuu umegusa jambo linalonisikitisha sana. Natamani kulila Tanzania Tanzania nchi yangu ninapoambiwa maneno kama uliyosema
 
Lipi wamewahifanya wakafaulu bado Wana mawazo ya ukale kuamini akili za watu zimefungwa kwenye box Kama zama za Nyerere,wanaotawaliwa Wana upevu zaidi kuliko watawala
 
Ndio Mkuu kuwaruhusu Chadema kuendelea kuwepo ni kuhatarisha amani ya Nchi
Ndio ilionekana tishio kwa usalama wa nchi kama kikundi cha Kigaidi hivi ndio maana inapotezwa kimyakimya isilete mambo ya muslimbrothrhood hapa
 
Mkuu umegusa jambo linalonisikitisha sana. Natamani kulila Tanzania Tanzania nchi yangu ninapoambiwa maneno kama uliyosema
Mimi nimekuwa nikiililia nchi hii mpaka nikakubali kuwa kwa kizazi chetu (na huenda kijacho) kuyaona mabadiliko yatarajiwayo itakuwa ngumu. Tatizo kubwa la watu wetu wana-promote sana 'destructive mindset" (na inashangiliwa) badala ya constructive mindset. Yaani tunapenda sana egosystem badala ya ecosystem.
 
Ni kweli huo mfumo ni jambo zuri, tatizo linakuja kwenye ukweli kuwa kila kitu kinachokuwepo kina "conditions" zake. Kwa habari hii conditions ni mbili: 1) utashi na 2) uwezo wa wananchi kuupigania mfumo. Ndiyo tunarudi kwenye point zako kuwa walioko kwenye mamlaka wanatumia utashi wao kuhakikisha mfumo hauleti faida inayotarajiwa, na wananchi bado hawajafikia level ya kuweza kupigania mfumo usimame...
True mfano tu for 5 yrs wamekuwa bize kupambana na watu badala ya kupambana na umasikini,hizo nguvu zilizotumika kupambana na upinzani vipi Kama zingewekezwa kutatua tatizo la ajira kwa vijana tungekuwa wapi.

Eti Leo mtu anawaza kuanzisha chama pinzani ili kipingane na upinzani badala ya kuwaza afanye nn ili angalau watu wale Milo mitatu.
 
Chadema ina udhaifu katika uongozi, lakini sidhani kama ukabila ni tatizo lao kubwa. Hayo ni maneno ya propaganda ambayo wengi wameyaamini. Ukiwalaumu Chadema kwa ukabila, basi ni wazi Raisi Magufuli anapaswa pia kulaumiwa kwa kufanya teuzi nyingi kikabila au kikanda, na hata kindugu. Lakini mie nadhani la msingi ni kwamba wanateuliwa watu wenye uwezo, na hilo ndilo jambo linalotakiwa...
Nimewahi kusema hapa JF kwamba Mbowe kama kiongozi wa CHADEMA anaweza kuwa hana hisia za ukabila, lakini kuna Misimamo ya wazi ya watu wanaoifuata CHADEMA kwa sababu ya raha kwamba kiongozi wake ni kabila lao. Hiyo ipo na inajionesha. Yeye mwenyewe Mbowe kama hayuko hivyo alistahili akwepe support za aina hiyo.

Ilifikia hatua hata mbunge wa CHADEMA Mwanza anatafutwa mchaga! Bahati mbaya naye anaonesha hayo hayo! Angalia wanaomzunguka. Baada ya kukosana kwao ndo tunajua kuna mashemeji, wadogo zake wanaopewa tenda za kufanya kazi za chama.

Mfano wako wa NIC ya Mwaikambo (siyo Mwabulambo kama ulivyoandika) hiyo ni kweli hata NBC ya Nsekela ilkuwa hivyo. Matawi yote ya NBC kasoro mawili ya DAR, mabosi walikuwa Wanyakyusa: Siyo suala la sifa, tatizo ni pale unapotafuta wenye sifa toka kabila moja. Mbona sasa hatuwaoni NIC na NBC?

Walipoondoka maboss wa kabila lao nao wakapoteza sifa? Unapounda serikali huwezi kusema kikubwa ni uwezo, NO! Uwezo lazima utafutwe makabila yote, mikoa yote! Kama Unaliona kwa rais Magufuli, wote tuseme ni vibaya na isiwe sababu ya CHADEMA kuendeleza hayo.
 
Nimewahi kusema hapa JF kwamba Mbowe kama kiongozi wa CHADEMA anaweza kuwa hana hisia za ukabila, lakini kuna Misimamo ya wazi ya watu wanaoifuata CHADEMA kwa sababu ya raha kwamba kiongozi wake ni kabila lao. Hiyo ipo na inajionesha. Yeye mwenyewe Mbowe kama hayuko hivyo alistahili akwepe support za aina hiyo...
Thus haifai makabila makubwa kupewa uongozi watajipendelea wao kwa wao ,lipo hata ccm ilo check teuzi ni za maagizo
 
Back
Top Bottom