Asipewe Uenyekiti: Atashindwa hata kufikia robo ya mafanikio ya Kikwete

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Nashauri CCM wasimpe uenyekiti JPM kwa kuwa watakuwa wanamuongezea kazi ambazo nahisi itakuwa ngumu kuzimudu!
Raisi anapenda kufanya kila kitu mwenyewe, so akiwa na kofia mbili kwanza italeta confusions na pili itazorotesha maendeleo ya nchi!
Naona pamoja na uzalendo aliyokuwa nao, pamoja na dhamira njema aliyonayo, JPM atashindwa kufikia hata robo ya mafanikio aliyofikia Kikwete sehemu kubwa itakayomuangusha ikiwa ni kushindwa kutengeneza team itakayomsadia kufanya kazi! Tazama mafanikio ya Kikwete sehemu kubwa ametenda Magufuli, Sita, Lowasa, wapinzani kina Slaa, Mbowe etc! Lkn mwisho wa siku credit itarudi tu kwa raisi wa awamu husika!
Kaka yetu sasa ameingia na mguu wa kushoto! Alianza kazi mwenyewe akidai anabana matumizi, sasa ametengeneza Baraza, bado yeye ndiye anayekamata sukari, ndiye waziri wa mambo ya nje, ndiye waziri wa elimu, ulinzi, fedha etc! Hata kama ana mapenzi ya aina gani, hata akiwa na dhamira njema vipi, kuwa na team ya utendaji ndiko kutampa JPM uwezo wa kufanikiwa ktk utendaji!
Hebu tazama uwezo wa kuunda team ulivyosaidia miaka 10 ya kikwete imekuwa na manufaa makubwa sana!
  1. Ujenzi wa chuo kikuu kikubwa zaidi Africa ya mashariki (UDOM)
  2. Ujenzi wa hospitali 2 kubwa zaidi ukanda wa Africa Mashariki na miongoni mwa hospitali kubwa kusini mwa jangwa la Sahara! (Mh2 mpya na hospitali ya UDOM)
  3. Ujenzi wa barabara uliounganisha karibu kila mkoa nchini
  4. Ujenzi wa madaraja makubwa zaidi ya moja likiwemo daraja la kigamboni
  5. Upanuzi wa airport ya Dar es Salaam
  6. Upanuzi wa barabara ya Moro kuruhusu mabasi ya haraka ktk jiji la Dar
  7. Kuboresha huduma za afya ktk tiba za HIV, huduma za Mama na mtoto, utafiti nk
  8. Kuongeza idadi ya wanafunzi wanaokwenda sekondari kwa kuanzishia shule za kata zinazoruhusu wanafunzi wengi zaidi kusoma hadi sekondari
  9. Mishahara ya watumishi kupanda kwa zaidi ya asilimia 500 (500%) toka alipochukua usukani toka kwa mkapa
  10. Taasisi nyingi za umma kuwa na uwezo mzuri zaidi ktk kujiendeleza na kuwa na utegemezi mdogo kwa serikali! Mashirika mengine mpaka kuwa na uwezo wa kuisaidia serikali kwa kuikopesha eg PPF,NSSF, na PSPF!
  11. Kupanuka kwa Uhuru wa habari, uwezo wa kuichallenge serikali na upinzani kuwa na nguvu zaidi bila ya kuwa na maafa zaidi kwa jamii!
Unless Mkuu anawaamini wenzake na wanafanya kazi kwa kushirikiana na kutegemeana, hatutoweza kufikia hata lengo moja tulilojiwekea! Sasa tunakaribia kufikia mwaka mmoja wa kazi za awamu ya 5, dalili za mafanikio hamna kabisa, kuna confusion kubwa kuliko hope! Watu wako puzzled, nchi inakuwa doomed na visa na visasi vya kisiasa! Watumishi wameparalyse, wanasiasa wanajifungia ndani, bunge limekuwa la chama kimoja na spika wake!
Jamani kumbukeni huu mwaka mzima alikuwa anaongoza serikali tu, sasa wakimpa na chama itakuwa shida, either chama kishike hatamu na tuue vyama vingine au tudorore kiuchumi! Mimi naipenda Tanzania na nina shauri CCM muipende nchi yenu, chagueni mwenyekiti mwingine! Nadhani hata raisi mwenyewe anaomba kikombe hiki kimuepuke Ila kama kimeandikwa basi neno litimie!
Hebu na tumuombee raisi wetu akose uenyekiti wa chama kwa awamu hii, lkn pia aweze kuona umuhimu wa kuajiri (kuteua) watu ambao watafanya kazi kumsaidia na sio just kutimiza jukumu la uteuzi!
 
Back
Top Bottom