Mtata Mbosa
Member
- Jun 28, 2011
- 14
- 0
Wana jf wenzangu, sijui tunaelekea wapi na katika karne gani? ukiachilia mbali swala la wanafunzi wengi kutopata mkopo, uongozi wa chuo kikuu cha Dodoma ilitoa tangazo kwenye website yao www.udom.ac.tz kuwa mwisho wa kulipa gharama za accomodation pamoja na ada ni tarehe 30/09/2011, wameongeza kuwa yeyote atakaye kaid agizo hizo hata pewa nafasi ya masomo mwaka 2011/2012. cha kushangaza zaid ni kwamba usajilli utaanza tar 15/10 kwa mwaka wa kwanza na kufuatiwa na wanafunzi wa mwaka wa 2 na 3, ni jambo la kusikitisha kwani asilimia kubwa yanawafunzi inaonyesha kutolipa, hii yote ni kwasababu ya hali duni za familia zao na kwamba wengi wao hutegemea pesa ya kujikimu kutoka bodi ndo iwasaidie kulipa gharama za accomodation na sehemu ya ada ambayo wanatakiwa kulipa wao. ndg zangu watanzania wenye mapenzi mema na nchi yetu hili si jambo la kulifumbia macho kwani wanafunzi wamekuwa akionewa na kuwafanya kutokuwa na sauti kuhofia kufukuzwa.