Asilimia kubwa ya askari si wapenzi wa CCM

KAUMZA

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
699
237
Inawezekana usiamini, lakini huu ndo ukweli. Askari wengi wa vyeo vya chini na vya kati wa majeshi yote(JWTZ,POLICE NA MAGEREZA) hawana kabisa imani na CCM. Unaweza ukaniuliza utafiti huo nimeufanya lini na wapi na kwa sample ipi!

Kifupi ni kwamba, mzee wangu mimi ni afisa mstaafu wa jeshi. Nina ndugu zangu wengi sana wapo ktk majeshi. Kila jion tumekuwa tukienda ktk bwalo kubadilishana mawazo. Mara nyingi mada za siasa huibuka na hapo ndo utagundua wengi wameichoka CCM. Wapo wanaosema walikuwa na imani na Jk(si CCM) kwa kuwa alikuwa askari labda angewaboreshea maslaha yao, ila amewaangusha.

KAMA HUAMINI, JARIBU KUFANYA UTAFITI JAPO MDOGO KWA SAMPO YOYOTE UNAYOITAKA, JIBU UTAPATA.
 
Sina ubishi.Ni kweli.Nadhani sisi watu wengi tunadhani polisi na ccm kwa kuwa wanaisaidia ccm kama mahita vs cuf<ngangari vs ngunguri) na visu vya cuf,that was/is on cause of business.

But when it comes to an individual, askari wetu ni ngome imara ya upinzani kama ilivyo vyuo vikuu.bahati mbaya hawapati nafasi ya kupiga kura. Kipindi cha uchaguzi wanasambazwa na hvyo kukosa fursa.
 
Very True! But let's not worry because the day will come when they'll be redeemed and that day is very near.
 
Ni kweli askari wengi hawapendi ccm na kama mdau alivosema hawapigi kura sababu ya kusambazwa sehemu mbalimbali tofauti na walizojiandikishia. Inashangaza hata JK jana ktk hotuba yake kasisitiza sana "haki ya msingi" ya kupiga kura kwa wana Igunga illhali haki hiyo chaguzi zote haiangaliwi kwa askari kuwawezesha kuifurahia.

Big up askari wote wapenda mabadiliko.
 
Nilikutana na mama mmoja ambaye ni askari magereza hapa Ruanda mbeya. Anatoa maneno makali kiasi ambacho hata mimi japokuwa ni mpinzani siwezi. Amemchoka jk na ccm, hafurahishwi kabisa na wizi wa raslimali za taifa na ufisadi.

Nikaenda BOT hapa nako nilipokewa na askari police. Nilijitambulisha kuwa mwanafunzi wa chuo, nikapokewa na neno la ajabu, 'vijana ninyi ndio wa kuleta mabadiliko'.

Du! Jaman kweli majeshi yetu yanaichukia serikali ya ccm.
 
Kwa uelewa wangu vyombo vyote vya ulinzi na usalama havitakiwi kuwa wanachama wa chama chochote cha siasa. Hii ilifanywa hivi mara tu tulipoanza mfumo wa vyama vingi hapa nchini.

Pamoja na hilo laini watumishi katika vyombo hivyo vya ulinzi na usalama wanaruhusiwa kupiga kura chama chochote wakipendacho. Hivyo kura wanaruhusiwa lakini uanachama hapana.

Kutokana na hilo, ni kama askari wamebanwa kuonyesha mapenzi yao katika medani ya siasa hivyo kupractice indirect. Uchunguzi usio na mawaa imebainisha askari wengi uchaguzi uliopita waliipigia upinzani kura zao. Sababu zipo nyingi, moja maslahi duni kwa mujibu wa madai yao, mbili kutolipwa madai ya yao ikiwemo likizo na night allowance kipindi wanapohama toka sehemu moja kwenda nyingine n.k

Kutokana na hilo, askari wengi wa ngazi za chini hawakipendi chama tawala wakiamini huyo ndiyo mchawi wao. Viongozi wengi hawashabikii hili kwa kuwa wao wana marupurupu mengi na uoga wa kupoteza madaraka endapo itajulikana wana support upinzani. Huo ni kwa kadri ya uelewa wangu.
 
Nilikutana na mama mmoja ambaye ni askari magereza hapa Ruanda mbeya. Anatoa maneno makali kiasi ambacho hata mimi japokuwa ni mpinzani siwezi. Amemchoka jk na ccm, hafurahishwi kabisa na wizi wa raslimali za taifa na ufisadi.
Nikaenda BOT hapa nako nilipokewa na askari police. Nilijitambulisha kuwa mwanafunzi wa chuo, nikapokewa na neno la ajabu, 'vijana ninyi ndio wa kuleta mabadiliko'.

Du! Jaman kweli majeshi yetu yanaichukia serikali ya ccm.
Akipata upenyo huyo anaweza kujitoa mhanga kwa chuki aliyonayo!
 
Hii ni siri iliyobayana, angalia mfano mdogo tu majimbo mawili ya Kawe na Ubungo amabako kuna concentration kubwa ya wanajeshi, wabunge wake ni Chadema.
 
Kata ya longuo jimbo la moshi mjini diwani wao ni Chadema,longuo wakazi wake asilimia 90 ni askari maana ipo ndani ya chuo cha polisi ccp
 
Nakumbuka mwaka 1995 askari polisi wengi wa pemba waliamishiwa Bara baada ya kuonyesha mapenzi ya wazi kwa CUF akiwemo askari aliyekamatwa anachora ramani ya kituo kuwapelekea CUF,Baada ya hapo waliamishwa askari vijana toka bara wakapelekwa Pemba bila hata malipo matokeo yake nao wakageuka wapinzani wa serikari ,kwa ujumla hata baadhi ya maofisa hawaridhishwi na serikari ya CCM
 
Inawezekana usiamini, lakini huu ndo ukweli. Askari wengi wa vyeo vya chini na vya kati wa majeshi yote(JWTZ,POLICE NA MAGEREZA) hawana kabisa imani na CCM. Unaweza ukaniuliza utafiti huo nimeufanya lini na wapi na kwa sample ipi! Kifupi ni kwamba, mzee wangu mimi ni afisa mstaafu wa jeshi. Nina ndugu zangu wengi sana wapo ktk majeshi. Kila jion tumekuwa tukienda ktk bwalo kubadilishana mawazo. Mara nyingi mada za siasa huibuka na hapo ndo utagundua wengi wameichoka CCM. Wapo wanaosema walikuwa na imani na Jk(si CCM) kwa kuwa alikuwa askari labda angewaboreshea maslaha yao, ila amewaangusha. KAMA HUAMINI, JARIBU KUFANYA UTAFITI JAPO MDOGO KWA SAMPO YOYOTE UNAYOITAKA, JIBU UTAPATA.

Pia hawana imani na Chadema!
 
Sidhani!! Bado kuna mambumbu wengi tu huko jeshi la wananchi na majeshi mengine ambao kwa kuwa kwao jeshini wanajiona kama wapo juu ya kila kitu.

Nina jamaa zangu kama watatu hivi ambao waliingia jeshi la wananchi mara tu baada ya kumaliza chuo, nataka kukwambia hawa wehu hawataki kabisa kusikia mtu anamlaumu au kumbeza JK. Wanasema waliapa kwa upanga kumlinda, kwa hiyo hawapo tayari kusikia anadhalilishwa kwa namna yoyote ile. Mwingine akafikia hata kunitishia eti niachane na siasa, nifanye kazi zangu.

Mmoja ambaye ni jirani yangu na anakaribia kustaafu hivi sasa, katika mazungumzo ya kawaida tu alinichimba mkwara eti alikuwa ananiheshimu lakini anashangaa nashabikia chama cha vurugu yaani chadema.

Kwa utafiti wangu, wanajeshi wengi ni mambumbu tu, wanaridhika sana na vile vibanda vya bati toka chini hadi juu na bia za ruzuku wanazokunywa makambini. Msije mkajifariji ndugu zangu, tusitegemee utetezi kutoka kwa jeshi letu kama ilivyokuwa huko Tunisia na Misiri.

Ikitokea tukaamua kuandamana, tutaishia kuuana kama Libya tu, maana majeshi yetu yatachukua silaha kupambana na sisi. Hakuna tumaini lolote kutoka kwa jeshi letu ndugu zangu.
 
Police kama hayo yote yamewakumba wakati ni sasa kukata kutumika kuwaibia ccm kura ili washinde yafaa tuwe wamoja ktk kulikomboa taifa letu
 
Nilikutana na mama mmoja ambaye ni askari magereza hapa Ruanda mbeya. Anatoa maneno makali kiasi ambacho hata mimi japokuwa ni mpinzani siwezi. Amemchoka jk na ccm, hafurahishwi kabisa na wizi wa raslimali za taifa na ufisadi.

Nikaenda BOT hapa nako nilipokewa na askari police. Nilijitambulisha kuwa mwanafunzi wa chuo, nikapokewa na neno la ajabu, 'vijana ninyi ndio wa kuleta mabadiliko'.

Du! Jaman kweli majeshi yetu yanaichukia serikali ya ccm.
Hakuna lolote hujakutana nao kwenye maeneo yao. Nilipokuwa UDSM nilikutana na mikasa ya migomo karibu kila mwaka kwa muda wa miaka minne, na kila mgomo ulipotokea nilikuwa mmoja wa waliokuwa wanakamatwa na kupelekwa polisi.

Nataka kuwaambia tu kwamba experience yangu na hii mijamaa ni kwamba majority ni mambumbu tu. Huko police daima nimekuwa nikikutana na askari wakorofi kupita kawaida, na wengi wao ni wale wa kutafuta sifa.

Hakuna hata mmoja anayefikiria kwamba vijana wa chuo wanaweza kuwa chachu ya mabadiliko, mitizamo ya wengi ni kwamba vijana wa chuo ni watu wa vurugu. Kusema ukweli nawachukia sana hawa watu, si JWTZ si polisi si nani. Na si nawachukia kama binadamu bali umbumbu wao katika utendaji wa kazi zao.

Hamjiulizi polisi wanaopenda upinzani kuwapiga risasi wapinzani wenzao? Nawahakikishieni, huko jeshini wala si mahali pa kuweka tumaini. Kuna wapenda sifa ile mbaya.
 
Kata ya Mbalizi road.Mbeya mjini,nusu ya wakazi wake ni wajeda,(polisi&magereza)inashikiriwa na Chadema.
 
hii habari ni kweli.na anaye pinga akapimwe akili.nakumbuka uchaguzi uloisha kituo mojawapo pale kwa wanajeshi rugalo jimbo la kawe kikwete alipata kura nne.yaani alifunikwa na slaa.mwisho wa siku halima mdee akakinukisha jimbo zima likaenda chadema.mia
 
Ni ukweli asilimia 100 Tazameni vituo vyote vya jeshini CCM walipata kura chahe sana za Urais. Mfano Lugalo alipata kura 4, Huko Arusha Tanganyika Packers jeshini kura 17 kati ya 178, kwingine tatuteni wanajf.

Niliwapa lifti wanajeshi wanne wakitokea Mbweni kama wiki 3 hivi nyuma to ubungo barabara nzima wanalia na CCM. fIKA MWENGE WAKAONA MAMA MMOJA KAVAA KIJANI WE sikuamini matusi yao. M ture. Viongozi wa top wapo CCM kimagumashi ila majority neva kabisa.
 
Unachokiongea ni kweli kabisa mkuu, ila tatizo ni kuwa hawa ndugu zetu bado ni mawazo mgando kwa sababu bado wanaamini kuwa bila ccm wao hawana kazi eti kwa kuwa wanapewa vitisho na wakuu zao wa kazi
 
Sidhani!! Bado kuna mambumbu wengi tu huko jeshi la wananchi na majeshi mengine ambao kwa kuwa kwao jeshini wanajiona kama wapo juu ya kila kitu. Nina jamaa zangu kama watatu hivi ambao waliingia jeshi la wananchi mara tu baada ya kumaliza chuo, nataka kukwambia hawa wehu hawataki kabisa kusikia mtu anamlaumu au kumbeza JK. Wanasema waliapa kwa upanga kumlinda, kwa hiyo hawapo tayari kusikia anadhalilishwa kwa namna yoyote ile. Mwingine akafikia hata kunitishia eti niachane na siasa, nifanye kazi zangu. Mmoja ambaye ni jirani yangu na anakaribia kustaafu hivi sasa, katika mazungumzo ya kawaida tu alinichimba mkwara eti alikuwa ananiheshimu lakini anashangaa nashabikia chama cha vurugu yaani chadema.

Kwa utafiti wangu, wanajeshi wengi ni mambumbu tu, wanaridhika sana na vile vibanda vya bati toka chini hadi juu na bia za ruzuku wanazokunywa makambini. Msije mkajifariji ndugu zangu, tusitegemee utetezi kutoka kwa jeshi letu kama ilivyokuwa huko Tunisia na Misiri. Ikitokea tukaamua kuandamana, tutaishia kuuana kama Libya tu, maana majeshi yetu yatachukua silaha kupambana na sisi. Hakuna tumaini lolote kutoka kwa jeshi letu ndugu zangu.

Mpe pombe masikini asahau shida zake, ina maana wameridhika na yale mabanda ya kuku?
 
Back
Top Bottom