Asilimia 90 ya Watanzani Wamejikuta tu.........

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393
Jambo moja ambalo wengi hamlijui ni kwamba, takriban asilimia tisini ya Watanzania wamejikuta tu wakiwa ni wafuasi wa dini hizi za mapokeo yaani Uislamu au Ukristo sio kwa utashi wao, bali kwa utashi wa wazazi, au walezi wao, yaani kwa kuwa wazazi au walezi ni wafuasi wa dini fulani, watoto hawawezi kwenda kinyume na imani za wazazi au walezi wao. Asilimia kumi waliobaki wapo kwenye dini hizo kwa kimaslahi zaidi, kama sio kwa sababu za kielimu basi yaweza kuwa kwa ajili ya mke, mume au hata ajira……………..

Kama mnavyofahamu, kuna baadhi ya watu walijikuta wakibadili dini ili kuweza kupata elimu kutokana na mfumo wa kielimu uliokuwepo kipindi cha ukoloni. Na pia wapo waliobadili dini sio kwa sababu ya utashi wao, bali ni kwa sababu ya kupata ridhaa ya kuoa au kuolewa. Na wapo waliolazimika kubadili dini ili kupata ajira mahali fulani kulingana na sera za taaisisi husika. Na ndio maana nikasema ni kwa sababu za kimaslahi zaidi…………………………..

Nimewaza tu kwa sauti……………………
 
Nadhani Watz tunatakiwa kuwaza kuhusu dini kwa kupitia angle hii.

Nadhani huu utakuw ani mwanzo mzuri wa kuanza kujidadavua na hizi dini za mapokeo..................... Ahsante mtoa mada kwa kuligusia hili........
 
Nadhani Watz tunatakiwa kuwaza kuhusu dini kwa kupitia angle hii.

Nimekuwa nikisoma mada nyingi zinazohusu dini na nimekuwa nikiona watu wakitaka kutoana ngeu humu............... kwa kuwa tumefundishwa kuwa DINI ni kitu ambacho hakitakiwi kuhojiwa, wengi tumejikuta tukihemkwa pale ambapo dini ambazo tumekuwa tukiziamini zikiguswa kwa namna yoyote.............. Huu ni ujinga tu.......!
 
jambo moja ambalo wengi hamlijui ni kwamba, takriban asilimia tisini ya watanzania wamejikuta tu wakiwa ni wafuasi wa dini hizi za mapokeo yaani uislamu au ukristo sio kwa utashi wao, bali kwa utashi wa wazazi, au walezi wao, yaani kwa kuwa wazazi au walezi ni wafuasi wa dini fulani, watoto hawawezi kwenda kinyume na imani za wazazi au walezi wao. Asilimia kumi waliobaki wapo kwenye dini hizo kwa kimaslahi zaidi, kama sio kwa sababu za kielimu basi yaweza kuwa kwa ajili ya mke, mume au hata ajira……………..

kama mnavyofahamu, kuna baadhi ya watu walijikuta wakibadili dini ili kuweza kupata elimu kutokana na mfumo wa kielimu uliokuwepo kipindi cha ukoloni. Na pia wapo waliobadili dini sio kwa sababu ya utashi wao, bali ni kwa sababu ya kupata ridhaa ya kuoa au kuolewa. Na wapo waliolazimika kubadili dini ili kupata ajira mahali fulani kulingana na sera za taaisisi husika. Na ndio maana nikasema ni kwa sababu za kimaslahi zaidi…………………………..

nimewaza tu kwa sauti……………………
nina wasi wasi na uelewa wako wa hesabu................unasema asilimia tisini walifuata mkumbo na asilimia kumi wako kimasilahi zaidi,jumla ni asilimia mia.mimi siko kwenye makundi hayo mawili uliyoyataja,wala haukunifikiria kwenye asilimia zako au kwa sababu mie ni negligible?
 
Ndio maana nikasema nimewaza tu kwa sauti............. samahani kwa kukusahau..................LOL
 
kwa mara ya kwanza katika jamvi ili nimemuona mtu aliye HURU! Hongera sana katika kujitambua wewe ni nani, mimi pia niliamua kuwa huru kitambo tu baada ya kujiuliza kuhusu mimi na dini kipi muhimu, naomba wale ambao ufahamu wao umevuka mipaka ya dini tuwasiliane.
 
Naomba tuungane katika kuondoa hili ombwe la DINI ambalo linaleta kisirani katika jamii.................. Inawezekana vipi watu wakose subira katika kujadili jambo ambalo hata wao wapo humo pasipo utashi wao...........................
 
Hii ni mara yangu ya pili kusoma makara yako nimefurahi sana kuona kuna wataalaamu humu kwenye jamvi safi sana.
 
Jambo moja ambalo wengi hamlijui ni kwamba, takriban asilimia tisini ya Watanzania wamejikuta tu wakiwa ni wafuasi wa dini hizi za mapokeo yaani Uislamu au Ukristo sio kwa utashi wao, bali kwa utashi wa wazazi, au walezi wao, yaani kwa kuwa wazazi au walezi ni wafuasi wa dini fulani, watoto hawawezi kwenda kinyume na imani za wazazi au walezi wao. Asilimia kumi waliobaki wapo kwenye dini hizo kwa kimaslahi zaidi, kama sio kwa sababu za kielimu basi yaweza kuwa kwa ajili ya mke, mume au hata ajira……………..

Kama mnavyofahamu, kuna baadhi ya watu walijikuta wakibadili dini ili kuweza kupata elimu kutokana na mfumo wa kielimu uliokuwepo kipindi cha ukoloni. Na pia wapo waliobadili dini sio kwa sababu ya utashi wao, bali ni kwa sababu ya kupata ridhaa ya kuoa au kuolewa. Na wapo waliolazimika kubadili dini ili kupata ajira mahali fulani kulingana na sera za taaisisi husika. Na ndio maana nikasema ni kwa sababu za kimaslahi zaidi…………………………..

Nimewaza tu kwa sauti……………………

Binafsi nimezaliwa katika familia ya kiislam,nimekuwa Mwislam mzuri kwa miaka 23. Niliamua kuondoka na Dini yangu Islam ambayo nimekuzwa kwayo si kwa Maslahi wala mkumbo,sana sana kwangu Dini ni maandalizi ya maisha baada ya haya ninayoishi na si kwa maisha haya hadi kifo. Kwa hiyo nimeshindwa kujipambanua kati ya hayo makundi yako,naomba msaada wako mkuu nijijue nipo kundi gani kati ya hayo makundi yako.
 
nina wasi wasi na uelewa wako wa hesabu................unasema asilimia tisini walifuata mkumbo na asilimia kumi wako kimasilahi zaidi,jumla ni asilimia mia.mimi siko kwenye makundi hayo mawili uliyoyataja,wala haukunifikiria kwenye asilimia zako au kwa sababu mie ni negligible?

Mm nilifikiri ni asilimia 90 ya walio kwenye hizo dini, meaning we the atheists have been excluded. Japo census iliyopita iliyoonyesha wapagani Tanzania ni zaidi ya asilimia 10 na less than 20%.
 
Kinachonikera mm ni msimamo ktk IMANI kati yetu wengi. Uwe na hizi dini za kimapokeo (Ukristo, Uislam, Uhindu etc) au uwe unaamini ktk mizimu, u-mpagan (atheist) km mm n.k. amini na shikilia hapo hapo. Naamini kwamba na niliwahi andika humu JF, kwamba hata uwe maskini vp, IMANI ndio ngao pekee inayokuokoa. Unapobadili u r nothing..... unakua huna chochote tena........ Shikilia hapo ulipo, usiwe mnazi na kujidai flexible kwa kubadilidha imani kama nguo......
 
Naomba nitofautiane na wewe.......... kwa hiyo wale waliokufa kabla ya ujio wa hizi dini za Mapokeo wako upande gani? Mimi sishikilii kitu ambacho nimechaguliwa kuwa humo na sio kwa utashi wangu, nimeamua kuzisoma falsafa za hizo zinazoitwa dini za Mungu na siku sio nyingi nitauweka ukweli wote hapa................ kwa nini nimeshindwa kufuata mkumbo huo..................
 
Binafsi nimezaliwa katika familia ya kiislam,nimekuwa Mwislam mzuri kwa miaka 23. Niliamua kuondoka na Dini yangu Islam ambayo nimekuzwa kwayo si kwa Maslahi wala mkumbo,sana sana kwangu Dini ni maandalizi ya maisha baada ya haya ninayoishi na si kwa maisha haya hadi kifo. Kwa hiyo nimeshindwa kujipambanua kati ya hayo makundi yako,naomba msaada wako mkuu nijijue nipo kundi gani kati ya hayo makundi yako.

Fanya utafiti ndugu yangu, na pale utakapouona ukweli basi jiunge nao............ Mimi siwezi kukuchagulia imani, kwani imani ni ya mtu binafsi na sio jambo la kuchaguliwa na mtu yeyote............. kama hicho kinachitwa MOTO wa milele kipo, basi kila mtu ataenda mwenyewe....... kama wale wanaosema kila mtu ataubeba msalaba wake mwenyewe.................
 
Back
Top Bottom