Asilimia 90 ya vijana wamefunga ndoa na watu ambao hawakuwa ni ndoto zao?

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Kuna utafiti nimeufanya kupitia kwa marafiki zangu wa karibu ambao wako katika ndoa wengi wananielezaa ya kwamba.

Watu ambao wamefunga nao ndoa ni wale watu ambao hawakuwa ndoto zao katika maisha.

Watu ambao waliwapenda na walitamani waje kufunga nao ndoa mwisho wa siku waliwaacha kwenye mataa na kuoa au kuolewa na watu wengine.

Leo hii kijana wa kiume ambae hajaoa ukimuuliza ni mwanamke wa ndoto yake ni wa aina gani atakwambia mimi nataka watoto wazuri wenye ngozi laini weupe wamesoma kidogo n.k.

Kijana wa kike ukimuuliza mwanaume wa ndoto yake atakwambia ni yule mwenye mali magari, fedha za kutosha na anajiweza kiuchumi.

lakini wachunguzi wa mambo na tabia nakadhalika asilimia kubwa ya vijana waliongia katika aina hii ya mahusiano huishiwa kutendwa na kuachwa kwenye mataa.

Wachunguzi wa maswala ya mahusiano wanakwambia kama upo serious unatafuta mke au mume wa ndoa basi mtafute mtu ambae ni hadhi yako bila kuangalia uzuri wala kipato chake huyo ndio mke au mume mwema.

Ndo maana wengi wameowa na kuolewa na watu ambao sio ndoto zao lakini wana hadhi sawa.
 
Panya hata anywe maji mengi kiasi gani, atakunywa tu mengi ya kutosha kujaza tumbo lake dogo....Tembo anatembea na tembo, akitembea na Kobe ataishia kumkanyaga
 
Shake your bambaa kwenda sukuma
Shake your bambaa eeeeeh , ndio ndoa nyingi znafungwa kwa style hiyo.
 
True na sio wanaowapenda,wanaweza kuwa wamevutwa na tamaa ya ngono,Mali nk
 
Miye naona wana wake ndiyo wahanga maana wao Hawa na uwezo wa kuchagua
 
Back
Top Bottom