Asilimia 85% ya watanzania hawaitaki serikali ya jk kama uchaguzi ungefanyika leo

sasa kama wewe CCM umefuata nini humu..usiwe unaongea kama muuza bar unaropoka ropoka tu bila facts...mliambiwa msome mkakimbilia madrasa sasa hayo ndo madhara yake ...ovyoooo
Umesikia JF ni yenu nyie tu? muuza baa anahishima zake kijana kwanini unamdharau?
 
Wewe unavyo hivyo vyote? Yaani kichwa na miguu? Maana hapa ni wazi inaonekana kichwa hamna maana hiki ulichoandika hapa tunajua kuwa kinatoka tumboni kuingia ktk uchafu.


Good, Huyo jamaa anavyo vyote ila tu anvitumia kinyume yaani anafikiri kwa miguu halafu anatembea kwa kichwa.
 
Sema asilimia 85 ya chadema.

Upo sahihi kabisa Foxy, hizi ni asilimia za CHADEMA, maana hao ndo wenye uchungu na nchi. Wewe utatoa wapi huruma kwa wananchi zaidi ya 80% wanaoishi maisha magumu na ya shida, ilihali unalishwa tu na mafisadi? Na unajua anayekulisha akiondoka kwenye system na wewe unapoteza? Ni haki yako utetee huu upumbavu, lakini siku zenu zinahesabika, hatuwezi sisi tukafanya kazi ya kuwachangia ninyi ili mneemeke na familia zenu wakati sisi tunaumia. Anzeni kucount down siku zenu za kuneemeka na uongozi huu wa kifisadi.
 
Upo sahihi kabisa Foxy, hizi ni asilimia za CHADEMA, maana hao ndo wenye uchungu na nchi. Wewe utatoa wapi huruma kwa wananchi zaidi ya 80% wanaoishi maisha magumu na ya shida, ilihali unalishwa tu na mafisadi? Na unajua anayekulisha akiondoka kwenye system na wewe unapoteza? Ni haki yako utetee huu upumbavu, lakini siku zenu zinahesabika, hatuwezi sisi tukafanya kazi ya kuwachangia ninyi ili mneemeke na familia zenu wakati sisi tunaumia. Anzeni kucount down siku zenu za kuneemeka na uongozi huu wa kifisadi.

Maisha magumu na ya shida unayajuwa wewe tu? sisi wengine hatuyajuwi? au unafikiri kila siku kinaambiwa "abracadabra" basi kinafata.

Sidhani kama kutakuwa na maisha bora bila kuweka mikakati muhimu, ambayo tunaiona Kikwete anaiweka, Elimu, Barabara, Zahanati, Uwekezaji wa kileo. Au mnajifanya hamjui chanzo cha kifo cha Tanzania? kama hamjui jiulizeni, Kikwete alichukuwa madaraka nchi ikiwaje na sasa ikoje? jibu utakuta Kikwete kafanya ajabu kwa muda mfupi aliopo madarakani, au hilo hulijui? Mashule zaidi ya awamu zote, intake ya vyuo vikuu zaidi ya awamu zote, walimu zaidi ya awamu zote, mabarabara zaidi ya awamu zote, mazahanati zaidi ya awamu zote, maji zaidi ya awamu zote, demokrasia zaidi ya awamu zote, usafiri zaidi ya awamu zote. Ni juzi tuu hapa (wakati wa toka Nyerere mpaka Mkapa) ilikuwa lazima twende tupite Kenya kwenda Mwanza tu, leo lipo hilo? biashara zaidi ya awamu zote. Sheria za madini kabadilisha na alimuweka mpinzani azisimamie. Yote hayo hamuyaoni? mna nini nyie?
 
Kama uchaguzi ungefanyika leo Tanzania, asilimia 85% ya watanzania wanasema kuwa hawaitaki serikali iliyopo madarakani. Ufumbuzi huu umetokana na mini survey niliyofanya kwa kutumia data (maoni) kutoka kwa JF members (kuanzia 2010 baada ya uchaguzi mpaka leo).

Sampling na survey design:

Hii ni qualitative descriptive analysis iliyohusisha random sample iliyochaguliwa toka JF population (which is currently =38,368). Swali lililoangaliwa ni mtizamo wa maoni (opinions), yaani: pro au against the government. Control ya comfounding factors kama udini na ukabila pia imefanyika ili kuondoa bias katika final results. Survey imehusisha idadi ya watu 3518 (sample size) ambayo imechaguliwa toka kwa population ya 38,368 JF members (current JF members). Sample hii imetokana na Confidence level = 99% at 3% error level. Data analysis imefanyika kwa kutumia current SPSS statistical software (for frequency statistics).

Matokeo:

• Asilimia 85% (2990) ya respondents wamesema hawaitaki serikali ya JK

• 10% (352) wamesema bado wanaitaka serikali ya JK

• 5% (176) wamekuwa neutral (hawakuonyesha wako upande gani kwa opinion zao)

My take (conclusion):

• Kwa wale wanaofanya social studies (kama kina Prof.Mukandara et al), we need these kinds of surveys more frequently to give a wakeup call to our lazy and corrupt leaders.

• Kuna wale watakao argue kuwa study hii sio representative of the countrywide opinions (kwa maana ya sample size ndogo), lakini wajue kuwa JF members wanawakilisha maoni ya watu from all parts of the country (and abroad).

• Kuhusu credibility yangu katika kufanya hili, be informed kwamba Nderi wa ngosha is a big time researcher. Nawasilisha.

stori nzuri sana ila inafaa zaidi kwenye jukwaa la utani/jokes
 
labda wapiga kura wa misikitini ndio wanaoitaka ccm

Sisi wa Msikitini tunamtaka sana tena sana kwa kuwa ni Muislaam mwenzetu, jee na nyinyi mnaomtaka Slaa ni kwa nini? kwa kuvunja amri za kanoni? kwa kuukimbia upadri? kwa ukosefu wa maadili (unaujuwa upi), au kwa ukiristo wake? semeni kweli msitafune maneno.

Wa msikitini mmoja ni bora kuliko mamilioni ya wasio wa msikitini, tumeona ya Osama.
 
Haka kamsomi kamenichosha pale kanapofanya sampling kwa confidence level 99 halafu kanachukua level of significance (error -
α) 3% sijui error pia ina error au test yake ni 102%
 
Ukibadili heading itakuwa vizuri ukituambia kwamba wananchi wamechoka na serikali. Hiyo ni kweli zunguka kila kona wananchi wanalalamika na kujiuliza jinsi hii miaka mitano itakavyokwisha. Japo no research no right to speak lakini ukipita kwa wananchi wa kawaida hauhitaji shule kubwa na research kujua kwamba wameichoka serikali. Kwanza ukienda kwa njia ya research watakudanganya wakijua mnafanya mambo yenu ya kiintelejensia. Lakini msitumie research zenu fake
 
Hao wanachama wa JF ni asilimia ngapi ya watanzania?

Hao wasiomtaka JK wanamtaka nani? (Pinda, Lipumba, Slaa?)

Ka Sample kako kapo biased sana maana umeangalia watu wanaojua kusoma na kuandika sio tu kusoma na kuandika bali kutumia computer, sio kutumia computer tu bali access ya Internet ambao wote karibu wapo mjini.

Umejitahidi lakini bado...


Hahaaaa kumbe ndio maana magamba hawataki wasomi...eehh?
 
KAULI YA KATIBU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU

VITENDO VYA JESHI LA POLISI KWA RAIA

NA

KUKAMATWA KWA WABUNGE WA CHADEMA


Katibu wa Wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na CHADEMA nalaani vitendo vinavyofanywa na Jeshi la Polisi kwa kusababisha mauji ya raia na kukwepa kufanya uchunguzi kamili na huru kuhusu wahusika wa vifo hivyo na kuingilia haki za msingi za jamaa za marehemu na wananchi wa eneo husika kushiriki katika maziko ya wakazi wenzao na hatimaye kupatiwa haki nyingine zinazostahili kutokana na madhila yaliyotokea.

Aidha nakemea hatua ya jeshi la polisi ya kuwakamata wabunge wa CHADEMA, Tundu Lissu na Esther Matiko wakiwa katika kazi ya kuwatumikia wananchi na natoa mwito waachiwe mara moja; wao pamoja na wote waliokamatwa nao.

Tundu Lissu (Mb) ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Sheria na Katiba aliitwa na wahanga wa tukio husika pamoja na chama kwenda kusimamia haki za msingi za familia za marehemu baada ya polisi kukataa kufanya uchunguzi na pia kuminya mazingira ya haki kupatikana.

Akiwa katika kutekeleza wajibu huo, jana (23 Mei 2011) alitaarifiwa na familia za marehemu na wananchi wengine kwamba polisi ina mpango wa kuchukua miili ya marehemu usiku na kuipeleka kusikojulikana na kuombwa kuungana nao katika kuwapa huduma za kisheria katika hatua zote. Aliambatana na familia za marehemu, wananchi na viongozi wa chama kufuatilia suala hilo ndipo alipokamatwa yeye na wengine na kuwekwa rumande kuanzia jana mpaka hivi sasa.

Esther Matiku ambaye ni mbunge wa viti maalum kupitia mkoa wa Mara anayetokea Tarime akiwa katika eneo lake la kazi leo (24/05/2011) alijulishwa na wananchi wa Nyamongo kwamba maiti ambazo walizichukua polisi kwa nguvu zingine wamezitelekeza njiani na kuitwa kwa ajili ya kushuhudia na kuchukua hatua zinazostahili kwa niaba ya wananchi. Akiwa katika kushughulikia suala hilo naye alikamatwa na jeshi la polisi na kuwekwa rumande mpaka hivi sasa.


Ifahamike kwamba matukio ya Nyamongo na Tarime kwa ujumla ni matokeo ya uongozi wa serikali kushindwa kusimamia vizuri sekta ya madini ikiwemo kuacha kuchukua hatua zinazostahili kwa wakati wa miaka kadhaa sasa kutokana na vitendo vya ukiukwaji wa sheria na mikataba vinavyofanywa na kampuni Barick Africa Gold na vile vinavyofanywa na polisi na vya kifisadi vinavyofanywa na viongozi wengine wa kiserikali wanaonufaika na hali hiyo yenye athari kwa wananchi katika maisha yao kutokana na mauji, uchafuzi wa mazingira, upotevu wa mapato ya umma na watanzania wa eneo husika kutokunufaika kwa rasilimali.

Naungana mkono na wananchi na wadau wote waliotoa mwito kufanyika kwa uchunguzi huru wa vifo (inquest) ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa na kwa nafasi yangu nyingine kama Waziri Kivuli wa Nishati na Madini nitatoa tamko karibuni lenye kueleza kwa kina udhaifu wa serikali ulivyosababisha mauji hayo na kutaka wahusika akiwemo waziri kuwajibika.

Aidha, kwa mara nyingine narudia tena kutoa pole kwa familia za marehemu ambao wanapitia kipindi kigumu wakati huu kutokana na matukio yanayoendelea; Mwenyezi Mungu awape uvumilivu wa kusimamia haki na ukweli kwa mustakabali wa taifa.

Imetolewa tarehe 24 Mei 2011 na:

John Mnyika (Mb)
Katibu wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Na Wabunge wa CHADEMA
 
labda wewe na familia yako ndio hao 85%, JF inajulikana kuwa wamejaa wanacdm ulitegemea nini kama kuna njemba zina kesha humu kuimba wimbo wa CDM.

Wangekuwa wamejaa wanachadema humu Jf basi mimi na wewe tusingekuwa na ID hapa JF
 
labda wewe na familia yako ndio hao 85%, JF inajulikana kuwa wamejaa wanacdm ulitegemea nini kama kuna njemba zina kesha humu kuimba wimbo wa CDM.

Washauri CCM wajiunge hapa nao watoe michango yao. Ila nina wasiwasi kuwa kama wewe ni true sample hawatahimili vishindo sana sana wataishia kujiondoa CCM.
 
Haka kamsomi kamenichosha pale kanapofanya sampling kwa confidence level 99 halafu kanachukua level of significance (error -
α) 3% sijui error pia ina error au test yake ni 102%

Hizi ni statistics ndugu yangu sio hesabu za kujumlisha na kutoa kama unavyotaka kufanya wewe. Mivilaza ya hesabu utayaona tuu yanavyohangaika na hesabu za kujumlisha na kutoa maana na kanuni pekee walizonazo vichwani
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom