Asilimia 80 ya ardhi ya umwagiliaji Tanzania inalimwa kwa njia za kienyeji, fursa kwa vijana kulima kilimo cha kisasa

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236
Kulingana na Benki ya Dunia (WB) katika ripoti yake ya Mapitio ya Uchumi wa Tanzania ya mwaka 2017, inaitaja Tanzania kutumia asilimia 80 ya maji yake yote katika shughuli za kilimo. Matumizi hayo ni makubwa ikilinganishwa na matumizi ya dunia ambayo yanafikia 70% katika kilimo.

Lakini ukuaji wa miji na viwanda unatishia kupungua kwa maji yanayotumika katika sekta ya kilimo. Ili kukabiliana na changamoto ya kupungua kwa maji, wakulima wanashauriwa kuitumia fursa ya mvua za msimu kuhifadhi maji ambayo watayatumia baadaye kuendeleza kilimo.

Hata hivyo, baadhi ya wakulima wanaendelea na kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia njia za kienyeji ambazo hazileti matokeo makubwa. Inaeleza kuwa Tanzania ina ardhi kubwa lakini ni asilimia 1.5 ya ardhi ya umwagiliaji ndio inatumika, huku 80% ya ardhi ya umwagiliaji inalimwa kwa njia za kienyeji na maji yanayotumika hayazidi 15% ya maji yote yanayopaswa kutumika katika kilimo hicho.

Kutokana na changamoto hiyo wakulima pamoja na wadau wa kilimo wanashauriwa kukibadilisha kilimo cha umwagiliaji kuwa cha kisasa na viundwe vyombo maalum vya kusimamia matumizi ya uzalishaji wa maji na njia sahihi za kilimo kulingana na maeneo waliyopo wakulima.

Zaidi, soma hapa => Asilimia 80 ya ardhi ya umwagiliaji Tanzania inalimwa kwa njia za kienyeji, kilimo cha kisasa kumkomboa mkulima | FikraPevu
 
Halafu utaambiwa hela ziko wapi za kuchimba yaani mtu anaona afadhali akakae kijiweni masaa 6 akihubiri Nani kasema nini badala ya kuchangamkia fursa

Acha manabii waongezeke tu na waganga wa kienyeji
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom