Asilimia 66% ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Umeme yaenda kwenye Mradi wa Stiglers. Je, imekaaje kiuchumi?

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
3,228
2,000
Naomba wachumi mje mtujuze athari za Bajeti ya 2020/21 kwenye sector ya nishati elekezwa kwenye mradi mmoja wa Nyerere Hydro Electric Power huko Rufiji. Kama siyo mchumi soma na upite.

Angalia kiambatisho hapo chini.

IMG_20200509_012159.jpg
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
9,962
2,000
Duh!

Wacha nipumzike kwanza...

Yaani SGR inatupiga huku na huku....
 
Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
1,468
2,000
Kwa kweli kwa mtu mwenye uelewa lazima tuishukuru Serikali ya awamu ya Tano. Changamoto nyingi zimerekebishwa. Mfano kukatikatika kwa umeme sasa imekuwa ni historia, Uimara ya shillingi ya Tanzania, Vituo vya Afya nchi nzima, Ubungo flyover ni machache tu yaliyotekelezwa na yanayoonekana. Mnyonge mnyongeni lakini mpeni haki yake.
 
Kyatile

JF-Expert Member
Feb 5, 2017
1,301

La umeme kutokatika katika ni baadhi ya maeneo. Huku kwetu umeme usiwaka usiku mzima mnajua kabisa kesho yake mchana hautakuwepo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
EZZ CHEZZ

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
724
1,000
Hii inamaanisha kuwa serikali inaupa kipaumbele mradi huo ambao kukamilika kwake kutaweka msingi imara kwenye sekta ya nishati. Hivyo pia sekta nyingine zitanufaika na kukamilika kwake kwani sekta zote zinahitaji umeme toshelezi na wa kuaminika.

Kikubwa ni serikali kuhakikisha inaboresha mifumo ya usambazaji sanjari na ujenzi wa miradi mipya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
5,255
2,000
Shida sio asilimia shida ni je imetengewa sh ngapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hujaiona kwenye wino mxito wa The Citizen? Is Tshs. 2.197 Trillions which is 66% of the Total Budget.

Lakini kwa uzoefu ujue kuwa pesa itakayopatikana ni 40% tu kutoka Hazina takribani Tshs. 0.8 T! Kumbuka Total cost ya Mradi Ni zaidi ya Tshs. 7+ Bilioni hivo kwa hesabu hizi mpaka mradi ukamilike utachukua miaka isiyopungus 10! Jiwe ataondoka bila ya ndoto yake kukamilika!
 
Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
3,228
2,000
Kwa kweli kwa mtu mwenye uelewa lazima tuishukuru Serikali ya awamu ya Tano. Changamoto nyingi zimerekebishwa. Mfano kukatikatika kwa umeme sasa imekuwa ni historia, Uimara ya shillingi ya Tanzania, Vituo vya Afya nchi nzima, Ubungo flyover ni machache tu yaliyotekelezwa na yanayoonekana. Mnyonge mnyongeni lakini mpeni haki yake.
Kuhusu umeme wa REA yawezekana ni 45% ya vijiji siyo 90% kama anavyosema Kalemani. Kumbuka Serikali ya awamu ya 5 ni Serikali ya kuchakachua au kupika takwimu.

Kuhusu hivyo vituo vya afya na zahanati vinavyojengwa havina wataalamu na hata dawa na vifaa tiba hakuna. Hospitali ni dawa na wataalamu wa afya siyo majengo.
 
Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
3,228
2,000
Hii inamaanisha kuwa serikali inaupa kipaumbele mradi huo ambao kukamilika kwake kutaweka msingi imara kwenye sekta ya nishati. Hivyo pia sekta nyingine zitanufaika na kukamilika kwake kwani sekta zote zinahitaji umeme toshelezi na wa kuaminika.

Kikubwa ni serikali kuhakikisha inaboresha mifumo ya usambazaji sanjari na ujenzi wa miradi mipya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli tulikuwa tunahitaji umeme mwingi na wa kuaminika kwa ajili ya viwanda na nishati zingine. Je huu umeme wa maji ndiyo bora kuzidi umeme wa gesi?

Ile miradi ya Kinyerezi 1 & 2 na sijui 3 kama ipo je hatma yake ni nini ?
 
Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
11,980
2,000
Hujaiona kwenye wino mxito wa The Citizen? Is Tshs. 2.197 Trillions which is 66% of the Total Budget.
Lakini kwa uzoefu ujue kuwa pesa itakayopatikana ni 40% tu kutoka Hazina takribani Tshs. 0.8 T!
Kumbuka Total cost ya Mradi Ni zaidi ya Tshs. 7+ Tshs hivo kwa hesabu hizi mpaka mradi ukamilike utachukua miaka idiyopungus 10! Jiwe ataondoka bila ya ndoto yske kukamilika!
Hakuna dam ya ukubwa huo iliyochukua chini ya miaka mitano kumalizika kujengwa. So hata kama budget ipo, bodo kuna hata miaka 10 mradi kumalizika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Masasaa

JF-Expert Member
Oct 23, 2015
452
500
Huo umeme kila kijiji si lazima uzalishwe, that stiglers gorge will do, so ni sawa kabisa, hata ingeenda 80% , the aerlier inakamilila the better

Stay home, stay safe
Corona kills
 
Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
3,228
2,000
Wewe ni bure kabisa unalinganisha teknolojia ya miaka ya sabini na sasa hivi.
Siyo suala la Teknolojia ya kujenga bali ni "Ability to Pay". Hazina ni muflis kwa kuwa Jiwe hajui planning. Anatekeleza miradi mikubwa kama 5 kwa wakati mmoja;
1. Ubungo Bridge
2. Coco Beach -AgaKhan Road
3. Kimara -Kibamba six lane highway
4. Kigongo -Busisi
5. SGR
6. Stiglers Hydro

Hiyo miradi yote ni pasua kichwa, kuna ambayo ina foreign na local component na kuna ambayo ni 100% local component tu.

Kuna miradi naona kama itasimama kama Barabara ya Kimara- Kibamba na SGR

Mtaka yote kwa pupa kukosa yote
 
PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
10,115
2,000
wizara ipo sawa, maana naona kama kwa sasa umeme unapatika karibia 90% vijijini. Hii ni kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na REA.

Ni muda sasa wizara ijikite kwenye huu mradi mkubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mnaposhiba bangi muwe mnajitahidi kutulia kwanza kabla ya kuanza kusumbua humu.

Hivi una uhakika 90% ya vijiji tanzania vina umeme ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom