Asilimia 50 ya Madeni ya Walimu ni ya Kughushi

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
863
Ukaguzi wa hesabu za Serikali wabaini madudu mengi katika madeni ya walimu,zaidi ya aslimia 50 ya madeni hayo ni yakughushi.Walimu hao wamefanya ufisadi huo ili walipwe vinono katika kupambana na misha duni waliyonayo. Wameambiwa wasioridhika na malipo yao waruhusiwa kukata rufaa.
progress.gif

progress.gif
 
Mishahara midogo sana hebu fikiria mwalimu Mwandamizi analipwa 210,000 kwa mwezi maisha ya mjini Dar! Nadhani wakipata nafasi lazima wagushi madai, ukizingatia hata posho mbili mbili hawana.....poleni waalimu!
 
Zaidi ya bilioni 13 zimeghushiwa( 10% ya pesa za EPA!). Na hao ndio walimu wetu wanaotuandalia VIONGOZI wa kesho wa Taifa letu.
 
Zaidi ya bilioni 13 zimeghushiwa( 10% ya pesa za EPA!). Na hao ndio walimu wetu wanaotuandalia VIONGOZI wa kesho wa Taifa letu.

Sidhani kama ni sahihi kuwalaumu walimu kwa hili. Swala la kujiuliza ni kwanini wasilipwe ontime? Wangelipwa ontime mambo mengi sana yasingejitokeza. Huu ni uzembe wa serikali kutokujali wafanyakazi wake kwa muda mrefu sasa.
 
Jamani watanzania, tukumbuke wanao-process hayo madai siyo waalimu wenyewe, ni wahasibu na viongozi husika!! Kazi ya mwalimu ni kuwakilisha uthibitisho wa madai, tujiulize, Je inawezekana kwamba kuna madai genuine, na wajanja wakachomeka yakwao?

tuangalie upande wa pili wa shilingi
 
Ni kweli wana collude na wahasibu wetu serikalini. Mambo haya yanafanyika kwa makubaliano. Ukishakubali wewe ni mwizi tu. Wala kuchelewa kulipwa sio sababu kukufanya uwe mwizi. Tukubali tu kwamba Nchi imeoza hii.
 
Nimekusoma mkuu
 
Kugushi ndio mtindo wa maisha katika ofisi za Serikali, mashirika n.k. na nchi nzima kwa ujumla maana wakubwa ambao ndio wanaopaswa kuonyesha mfano mwema nao wanagushi! Hebu fikiria hata watu ambao wamepewa dhamana ya kuliongoza taifa hili Mawaziri wanaweza kugushi vyeti je watu wa chini kama walimu na wahasibu tutawalaumu? Tunaambiwa Rais wa Awamu ya Tatu aliidhinisha Benki kuu 'wagushi' ili fedha za EPA zitoke kusaidia campaign za CCM, tutawalaumuje walimu na wahasibu ambao wanafuata nyayo?! The whole system is wrotten. Tujisahihishe!
 
Serikalini kama haina fedha za kuwalipa WALIMU ni bora wakakaa kimya kuliko kuja na sababu zisizo na msingi wowote, walimu wana madai mengi sana
 
Sidhani kama ni sahihi kuwalaumu walimu kwa hili. Swala la kujiuliza ni kwanini wasilipwe ontime? Wangelipwa ontime mambo mengi sana yasingejitokeza. Huu ni uzembe wa serikali kutokujali wafanyakazi wake kwa muda mrefu sasa.
Haki iliyocheleweshwa ni haki iliyonyimwa
 
Back
Top Bottom