Asilimia 29% ya pato la taifa inatokana na kilimo

singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
5,308
6,884
Asilimia 29% ya pato la taifa inatokana na kilimo. Asilimia 65 ya watanzania ni wakulima.Kwa miaka 5 iliyopita wizara ya kilimo imetengewa budget ya 250 Billions.

Itachukua miaka mitano budget ya kilimo kulingana na gharama ya madarasa ya COVID-19(ya Samia).
Daraja la Tanzanite ni sawa na bajeti nzima ya kulimo kwa mwaka mmoja.

Umewahi kutafakari ingekuwa vipi kama kilimo kingekuwa na budget ya 1Trillion?

Tungetatua tatizo la ajira kwa asilimia kubwa kuanzia wakulima, wasafirishaji, wazalishaji mbegu na mbolea, ma bwana kilimo, wafanyabiashara na vijana wa carrier mbali mbali watakao ajiriwa viwandani baada ya viwanda kupata malighafi, vijana wengi wangeelekea kwenye uzalishaji na kuachana na uchuuzi wa bidhaa za kichina.

Tungekuwa na viwanda vingi maana malighafi ingetosha kuviendeaha hivyo uchumi wa nchi ungekuwa kwa kasi.

Tungeweza kubargain, kupunguza uhalifu na kucontrol mfumuko wa bei, watu wakishiba akili zinakuwa na utulivu
Tuna nguvu kazi zaidi ya 60% ya wananchi ni vijana, tuna ardhi kubwa nzuri, vyanzo vingi vya maji kama mito, maziwa na mabwawa.
Tuna soko kubwa la bidhaa zetu kwa idadi ya nchi zinazotuzunguka na soko la ndani.

Kwanini tunaagiza vyakula kutoka nje? Hali tuna kila kitu cha kutufanya tuwe nacho cha kutosha na kuuza kwa wengine.

JK alikuja na "kilimo kwanza". Ndio ulikuwa mwanzo wa vijana wengi kuona kilimo kina tija. Ruzuku za mbolea na vifaa kama powertiler vilirahisisha sana.

Kilimo kilifanikiwa sana tatizo pekee ilikuwa soko la mazao. Nadhani tukitumia approch ile na kumodify sehemu ya upatikanaji wa masoko au ufunguzi wa

viwanda tutakuwa tumelipeleka taifa mbele.
 
Wewe unaona kuwekeza kwenye kilimo ni kitu cha kienyeji? Kwa Tanzania kilimo kina ajira nyingi sana
Ni kienyeji Sana ,hicho kilimo Ili kiwe na tija lazima kuwe na value addition ambayo ni viwanda..

Sasa jiulize unadhani kwa nini wawekezaji hawapendi kuwekeza kwenye kilimo ?
 
Ni kienyeji Sana ,hicho kilimo Ili kiwe na tija lazima kuwe na value addition ambayo ni viwanda..

Sasa jiulize unadhani kwa nini wawekezaji hawapendi kuwekeza kwenye kilimo ?
Mtu Kama mo anayenunua mazao na halimi,anaogopa risk za ukosefu wa mvua,lakini kilimo mfano mpunga unaajiri anayewekeza,opereta wa Kubota/trekta,fundi,vibarua shambani,combine harvester,mama ntilie,vibarua wa combine,muuza speak,muuza pembejeo,mkoboa mpunga,mwenye mashine ya kukoboa,dereva na utingo wa kubeba mpunga/Michele,mchoma vitumbua,mwenye duka la nafaka....
 
Hujajibu swali kwa nini wawekezaji hawashobokei kilimo?
 
Kuna vitu ambavyo kamwe mkoloni mweusi au kwajina lingine muote ccm..ambavyo hatokubali viendelee..moja ni kilimo na elimu..mkulima akitajirika ccm hawana cha kumlaghai tena..mkulima akiwa na elimu bora ccm hawana pa kupenya.

Shida na matatizo yote nchi hii ni kwa sababau ya ccm msijidanganye...siku mkiweza kuitoa ccm madarakani basi ndio mwanzo wa maendeleo makubwa ya nchi.

Ccm wanatumia matatizo na ujinga wa wananchi kama mtaji wa kisiasa..siku hivyo vikaondoka katika jamii jua na ccm imeondoka.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom