Asilimia 20 ya kahawa inauzwa kwa magendo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Asilimia 20 ya kahawa inauzwa kwa magendo

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by jamadari, Jan 30, 2011.

 1. jamadari

  jamadari JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2011
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 295
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Saturday, 29 January 2011 09:50 0diggsdigg

  [​IMG]Daniel Mjema,Moshi
  SEKTA ya kahawa inakabiliwa na matatizo mbalimbali, ikiwemo usafirishaji wa kahawa kwa magendo kwenda nje ya nchi na asilimia 20 ya kahawa mkoani Kagera imekuwa ikiuvushwa kimagendo kwenda nchi jirani.

  Matatizo hayo, yameainishwa katika mkakati wa miaka mitano wa maendeleo ya sekta ya kahawa 2011/2016, ulioandaliwa kwa pamoja na Bodi ya Kahawa Tanzania(TCB) na Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TaCRI).

  “Kahawa ya Robusta mkoani Kagera inanunuliwa na wanunuzi haramu na inakadiriwa asilimia 20 ya kahawa yote inayozalishwa mkoani humo imekuwa ikisafirishwa kimagendo kila mwaka kwenda nchi jirani,”ilisema taarifa hiyo.

  Taarifa hiyo ya kimkakati ambayo Mwananchi inayo nakala yake, imeeleza matatizo mengine ni magonjwa sugu ya kahawa na wadudu ambao wamekuwa wakishambulia mibuni.

  Tatizo kubwa linalokabili uzalishaji wa kahawa aina ya Robusta ni kuukabili ugonjwa wa mnyauko fusari (CWD) wakati matatizo katika kahawa ya Arabika ni ugonjwa wa chule buni (CBD) na kutu ya majani (CLR).

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mkakati huo, unaeleza kuwa uzalishaji wa kahawa unatarajiwa kuongezeka hadi kufikia tani 80,000 ifikapo mwaka 2016 na malengo ni kufikia uzalishaji wa tani 100,000 ifikapo mwaka 2020.

  “Uzalishaji utaongezeka kama wakulima na wadau wataitikia wito wa kupanda miche mipya ya kahawa, kuongeza maeneo ya uzalishaji, matumizi ya mbolea, kuboresha miundombinu na kudhibiti magonjwa”ilisema ripoti hiyo.

  Mkakati huo una lengo la kusaidia utekelezwaji wa sera mbalimbali za kitaifa, ikiwemo mpango wa kuondoa na kupunguza umasikini (Mkukuta), mpango wa maendeleo ya kilimo (ASDS) na mpango wa kilimo kwanza.

  Mapema mwezi huu, Waziri wa Kilimo,chakula na ushirika, Profesa Jumanne Maghembe alitembelea TaCRI na TCB na kuziagiza zifanye juu chini kuongeza uzalishaji wa kahawa na pia kutafuta masoko mapya nje ya nchi.

  Chanzo: Asilimia 20 ya kahawa inauzwa kwa magendo

  Hii Nchi yetu jamani haina serikali? Serikali haiashughulikii wauza mali ya Umma kimagendo? Tutafika kweli huku tunakokwenda jamani?
   
Loading...