Asili ya Ubaya wa Kila kiumbe upo ndani ya Maumbile yake

mjarrab

Senior Member
Nov 13, 2015
108
55
ASILI YA UBAYA NI NINI?.

****************************

Asili ya Ubaya wa Kila kiumbe upo ndani ya Maumbile yake.

Kwani hakuna kiumbe kilicho jiumba chenyewe,

Kwa kuzingatia hilo, kiumbe aliye umbwa ambaye ana Sehemu ya Ubaya katika maumbile yake ni wazi kuwa sifa za Ubaya huo zitakuwa zimewekwa na muumbaji.


kama utakataa kuwa muumbaji hakuweka sifa za Ubaya Kwa viumbe basi elezea sifa za Ubaya zilitokea wapi.?


Ukisema kuwa Ibilisi ndiye aliye leta Ubaya, basi jiulize Ubaya aliyo leta Ibilisi ulitoka wapi?


kumbuka kuwa Ibilisi nae ni kiumbe!,kama ndani ya Ibilisi kulikuwa na Tamaa,wivu,choyo basi jiulize sifa hizo zulitokea wapi?.

kama sifa hizo zilitokea ndani ya nafsi yake, basi ujue nafsi yake iliumbwa ikiwa na sifa hizo.


Je! ni nani aliiumba nafsi ya Ibilisi ambayo ndani yake kunaweza kukaa tamaa,Wivu,Ufisadi n.k?.

Utarudi pale pale kwenye Sorce ya maumbile yote ambaye ni Mwenyezi Mungu.



UBAYA KWA MTU NA VIUMBE VYA KIMADA.

***********

Kama ilivyo Kwa Ibilisi kunavyo patikana Ubaya,vile Vile ndivyo ilivyo Kwa Mtu na viumbe vingine vya kimada.

Kufanya kosa Kwa Adamu na mkewe kunadhihirisha kuwa ndani ya nafsi zao kuliumbika Ubaya,

Ubaya ambao ulikuwa unahitaji dereva ili uonekane:


Mfano.; Gari likiundwa na kukamilika,kisha likakosa dereva wa kuliendesha haliwezi kutembea.

Sasa kule kutokutembea Kwa gari Kwa sababu hakuna dereva hakumaanishi kuwa gari halikuundwa.


Sasa Ubaya upo na umeumbwa ndani ya nafsi za watu,Vile Vile Ubaya umeumbwa Kwa Kila kiumbe cha kimada.


Mimea isipo tunzwa hunyauka na kuharibika hiyo ndiyo kanuni ya maumbile yake,

hivyo aliye weka kanuni ya kuwa mimea isipo tunzwa huharibika,ndiye aliumba sifa ya kuharibika!

Na sifa ya kuharibika ni Ubaya,hivyo ina maana mimea ina sehemu mbili katika maumbile yake Ubaya na Uzuri

Na muwekaji wa kanuni hizo ni Mungu.

Hivyo Mungu ndiye aliye umba wema na Ubaya katika Kila kiumbe!.



Sasa hapa tunapata Ushahidi wa wazi kuwa IBILISI aliumbwa Kwa kanuni mbili katika nafsi yake wema na Ubaya.

Ila alishindwa kuutunza wema alio umbiwa mpaka ukanyauka na Ubaya alio umbiwa ukadhihiri ndani yake.

Kanuni ya Ubaya ni kuharibu,

Hivyo Ibilisi Kwa kuwa alishindwa kuutunza wema alio umbiwa , basi Ubaya alio umbiwa ulichukua nafasi na kudhihiri ndani yake na hivyo kubeba sifa ya kuharibu.


Kwa kawaida kile kilicho haribika hutupwa ili kisiharibu vingine!

Vile visivyo wezekana kutupwa huwekewa namna ya kuzuiliwa ili athari zake zisienee kwenye vitu vingine.


Mtu nae ana sehemu ya Wema na Ubaya katika maumbile yake kama Ilivyo Kwa Ibilisi.

Sehemu ya wema isipo tunzwa hutoweka na sehemu ya Ubaya hudhihiri ndani yake,hii ni kanuni iliyo umbwa na Mungu.


Mimea na Wanyama nao wameumbika katika Wema na Ubaya

Ila Wema wao na Ubaya Kwa viumbe hivyo haunaendeshwi Kwa Matakwa yao bali Kwa kanuni.

mmea usipo pata maji hunyauka na Ubaya hujitokeza!

Ubaya umejitokeza Kwa mmea si Kwa hiari ya mmea bali Kwa sababu zilizo nje ya Utashi wake!.


Hivyo Ubaya au Uzuri wa mmea utaonekana Kwa mwangalizi wake aliye nje ya mmea,

Mwangalizi asipo upa matunzo mazuri mmea hunyauka,

hivyo Ubaya ulio jitokeza Kwa mmea ni Ubaya wa Mtunzaji na Uzuri utakao jitokeza Kwa mmea ni Uzuri wa Mtunzaji.

Hivyo Mtunzaji ndiyo mwenye kubeba dhamana ya mmea.


Ibilisi na Mtu wamepewa hiari juu ya wema wao au Ubaya wao, wachague kuuthibitisha wema wao Kwa Matakwa yao,au kuudhihirisha Ubaya wao Kwa Matakwa yao,kwa hiyo Ubaya au wema utakao jitokeza kwao ni kwa utashi wao wala si Kwa utashi wa Muumba wao.Na Mwenyezi Mungu alifanya hivyo Kwa lengo maalum.

Ibilisi alichagua Kwa hiari yake Ubaya Kwa kuzifuata kanuni ziletazo Ubaya Kwa hiari yake.

Hivyo akawa Mbaya!.


Mtu kapewa hiari juu ya nafsi yake,juu ya wema wake au Ubaya wake!.Na akashawishiwa na Muumba wake kukiendea chema ili aufikie ukamilifu wake ambao ndiyo lengo kuu.


pia kapewa jukumu la Usimamizi na utunzaji wa vitu visivyo kuwa Yeye!

ili wema wake au uovu wake udhihiri katika hivyo!.


Kwa kuwa Mtu amepewa jukumu la kusimamia vitu vyote na kuviongoza hivyo ufanisi au uharibifu wa Utendaji katika kuviongoza utatoka kwenye utashi wake.

Uharibifu wa mazingira ni Ubaya ,na Ubaya huleta maafa.

Mazingira hayana Utashi wa kujifanya mabaya au mazuri.

utashi unatoka Kwa msimamizi wake ambaye ni Mtu aliye pewa Majukumu ya kusimamia.


hivyo kushindwa Kwa msimamizi kufanya kazi kusudiwa kunampokonya sifa ya kufikia lengo kusudiwa ambalo ni Ukamilifu.


KAZI YA IBILISI

****************

Kazi ya Ibilisi si kuumba Ubaya,!

kwani Yeye hana uwezo wa kuumba chochote!.

Ila anayo sifa za kuziendea kanuni za kuendea Uharibifu!.ambazo kanuni hizo zimeumbwa na Mwenyezi Mungu Kwa sababu maalum!.

Mfano: Uchafu huzalisha Mmbu,Inzi,funza n,k.

wote tunakubaliana kuwa uchafu umezalisha viumbe hai.

Huwezi Kusema kuwa Uchafu umeumba Mmbu,Inzi na Funza!.

Kwani hakuna mwenye uwezo wa kuumba Uhai zaidi ya Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu ndiye aliye umba kanuni za Kila kitu,zenye Matokeo mazuri na zenye Matokeo mabaya.

Hivyo uchafu kuzaa viumbe hai ni kanuni zenye kuleta Matokeo mabaya ambazo ziliumbwa na Mungu mwenyewe!.

Hizi ndizo kanuni zinazo tawala maisha yetu na tunaishi Kwa kanuni hizo!

Vitu tunavyo viunda wenyewe havitoki nje ya duara la kanuni hizo.

ukiunda gari au kitu chochote kinakuwa na kanuni mbili Uzuri na Ubaya! ukitumia Vile kinavyo takiwa kitumiwe kitaonyesha uzuri wake!

Kikitumiwa visivyo kitaonyesha Ubaya wake!.

Kwa hiyo Mwanaadamu anaunda Kwa kufuata kanuni zilizopo!.

Kwa hiyo Ibilisi alipo kwenda kinyume na kanuni ziletazo uzuri akaruhusu kanuni ziletazo ubaya zimuingie na kufanya kazi yake!.

Hivyo Ibilisi akawa mbaya Kwa kanuni zilizo wekwa.

Uchafu huleta magonjwa! hiyo ndiyo kanuni.!


kama Vile uchafuzi wa mazingira uletavyo magonjwa!

vile Vile uchafuzi wa nafsi huleta magonjwa ya kinafsi.

Hivyo Ibilisi alipata maradhi ya kinafsi Kwa sababu alichafua nafsi yake Kwa kuto zingatia kanuni za Usafi wa nafsi.

Ibilisi ndiye kiumbe wa kwanza kuzikiuka kanuni za Usafi wa kinafsi na kwa kukataa kwake kujisafisha alipata Maradhi mabaya ya kinafsi.

Na ndiyo Maana akaitwa baba wa uovu.!

Kama Vile Uchafuzi wa mazingira uletavyo Magonjwa mbali mbali!

Vile Vile Uchafuzi wa nafsi huleta Magonjwa ya kinafsi, Tamaa,wivu,choyo,Uongo,kutosikia kweli,kutoona kweli,na Ufisadi wa Kila aina!.

Kwa hiyo Ibilisi aliugua Maradhi hayo ya kinafsi!


Magonjwa ya kinafsi ni mfano wa Magonjwa ya cancer Yasipo tibiwa mapema yakikomaa hua hayana dawa!

Kwa hiyo Ibilisi baada ya kukataa kujisafisha ugonjwa wake wa kinafsi ukafikia kiwango cha kuto tibika!

hivyo umauti wa kinafsi haukwepeki kwake!.

Mgonjwa wa Maradhi ya kinafsi hubeba sifa ya kuwa mfano wa Bacteria asambazae Magonjwa!.

Hivyo Ibilisi anakuwa mfano wa Bacteria hatari asambazae Magonjwa ya kinafsi!.

Na Bacteria haji isipo kuwa Kwa kanuni,

Kama Vile uchafu wa mazingira hukaribisha Bacteria hatari!

Vile Vile uchafu wa kinafsi humkaribisha Bacteria hatari Ibilisi.


Hapo utakuwa umeelewa Jinsi Shetani Ibilisi asili yake na sifa alizo nazo.


Usafi wa mazingira huanza Kwa mtu mmoja mmoja hiyo ndiyo namna ya kupambana na adui bacteria asambazae Magonjwa.

Kila mtu anao Uwezo binafsi wa kusafisha Mazingira yake!

Akitekeleza jukumu lake ambalo lipo ndani ya uwezo wake Kwa kusafisha Mazingira yake uchafu hauto onekana katika Mazingira yake!

Bacterias hatari wa Mgonjwa hawatasogea katika Mazingira yake Kwa sababu kanuni za kuwafanya waje hazipo.


Kwa maana hiyo Ibilisi hasogei kwenye nafsi safi Kwa kuwa kanuni alizo ziweka Mungu zinamzuia!


Kwa hiyo uwezo wa mtu kujikinga na Shari za Ibilisi upo mikononi mwa Mtu mwenyewe!

Hivyo Nadharia ya kumfanya Ibilisi kuwa ni adui ambaye binaadamu hawezi kupambana nae bila msaada wa Mwenyezi Mungu ni kujidanganya.


Mungu ametengeneza sababu na kanuni za Kila kitu Kwa ajili yako,na amekupa akili ya upambanuzi, amekujaalia macho ya kuona Kwa Utambuzi,amekujaalia Masikio ya kusikia kwa kutambua,

kisha amekufundisha kanuni za Kila kitu! kwamba ukifanya hivi itakuwa hivi! Na usipo fanya hivi itakuwa hivi!


Kisha akakwambia ili ufikie ukamilifu wako fuata kanuni hii ya Usafi wa kinafsi na akakuonyesha usipo zifuata kanuni za Usafi ,uchafu utakuingia na kusababisha usifikie ukamilifu wako!

Kisha akakuletea msaada wa Vitabu na mitume wakuhamasishe utii na kufuata kanuni za Usafi ili ufikie ukamilifu wako!.


Baada ya msaada huo,Mungu ameiachia nafsi yako yenyewe ijifikishe katika lengo alilo kusudia

la Mtu Kwa uwezo wake na utashi wake ajifikishe katika daraja la utiifu Kwa Muumba wake Kwa akili huru bila kusetiwa kama viumbe vingine!.


Na mwanaadamu akifaulu katika kuisafisha nafsi yake na kuzifuata kanuni zote za Usafi wa kinafsi katika maisha yake yote,atakuwa ametii na kuifuata njia aliyo takiwa kuifuata na Muumba wake!.

Hivyo atakuwa ni kiumbe aliye fikia Daraja kubwa ambayo ni Twaa(utii) Kwa Muumba wake Kwa akili yake huru na utashi huru.


HIVYO UWEZO NA SABABU ZA KUPAMBANA NA IBILISI ZIPO KWA KILA MTU NDANI YA NAFSI YAKE.


HIVYO EPUKA NADHARIA ZA UVIVU WA KUFIKIRI NA KUKWEPA MAJUKUMU YAKO.


USAFI WA NAFSI NDIYO UMKINGAE MTU NA SHETANI,

MMBU NA INZI HAWAONDOKI KWA KUKEMEWA NA KUFUKUZWA!

WANAONDOSHWA KWA KUWEKA MAZINGIRA SAFI.

KAMA MAZINGIRA NI MACHAFU HATA MPEWE SILAHA ZA KUWAUA WATAZALIWA WENGINE KWA KUWA MAZINGIRA YANARUHUSU.


SILAHA YOKO NI USAFI WAKO


UCHAFU WAKO HAUONDOSHWI NA MTU MSAFI!

MTU MSAFI ATAKUJA KUKUONYESHA NAMNA YA KUSAFISHA MAZINGIRA YAKO ILI AWE NI MFANO KWAKO!


AKIONDOKA KAKUACHIA ELEMU YA KUJISAFISHA.

JUKUMU LITARUDI KWAKO TENA! KWAMBA UNATAKIWA UFANYE NA KUIGA MFANO WA MTU SAFI ILI NAWE UWE SAFI.

ILA USIKAE UKIJIDANGANYA KUWA MSAFI ALIYE KUJA KUKUFUNDISHA KUSAFISHA MAZINGIRA AMECHUKUA UCHAFU WAKO WOTE NA KWENDA NAO.


UTAKUWA MSAFI UKIFANYA NA KUTENDA KAMA ALIVYO KUELEKEZA,

USIPO FANYA KANUNI ZA UCHAFU ZITARUDI NA KUFANYA KAZI KAMA AWALI!


ACHANA NA NADHARIA ZA KUTUNGWA UTAPOTEA!


AKILI KICHWANI MWAKO.

***********


UPANDE ULIO SAHAULIKA

**************************

Mwanaadamu anamaisha ya ndani ya kinafsi na ya nje ya kimwili!.

Mwanaadamu anatumia muda wake mwingi kuyashughulikia maisha yake ya nje ambayo yana muda maalum!

Na kuyapuuza Maisha yake ya ndani ambayo ndiyo yanayo beba dhamana ya maisha yake ya milele!.

Mwanaadamu anapoteza Muda mwingi kuhangaikia chakula cha mwili wake ambao una muda maalum!

Anashindwa kuitafutia nafsi yake chakula cha kinafsi, nafsi ambayo imebeba dhamana ya maisha yake ya milele!.

Chakula cha kimwili huhitajia gharama nyingi, Pesa,nguvu, na Muda mwingi!

Wakati chakula cha kinafsi ni Bure kabisa!

Vyakula vya kimwili vipo wazi Kwa Kila Mtu, Ila vyakula vya kinafsi vinahitaji ukumbusho!

kama ilivyo kuwa kuna vyakula bora vya kimwili,pia kuna vyakula bora vya kinafsi.

Kuna vyakula vya kimwili viletavyo madhara Kwa Mwili,na kuna vyakula vya kinafsi viletavyo Madhara Kwa nafsi.

Chakula bora cha mwili,huufanya mwili kuwa bora na afya njema,na Chakula bora cha kinafsi huifanya nafsi kuwa bora na Imara.

Chakula bora cha nafsi Kwa uchache ni Imani ya kweli Kwa Mwenyezi Mungu,Elimu Yenye manufaa.

Ndani ya vyakula hivi kuna virutubisho vote Muhimu Kwa afya ya kinafsi.


N.B:. SOMO HILI NIMELIWEKA BILA KUWEKA ANDIKO LOLOTE KATIKA VITABU VYA MWENYEZI MUNGU.


ILA NIMELIANDIKA KUTOKA KWENYE MSINGI WA MAANDIKO YA VITABU HIVYO.

DALILI ZA AYA ZIPO KUTHIBITISHA HILO IKIWA ZITAHITAJIKA.
 
Ila mkuu chakula cha nafsi si bure hapo mimi nitakataa na nitaenda kinyume na wewe kuwa chakula cha mwili ndio bure ila baadhi ya wanadamu wameamua kukifanya kisiwe bure kwa mpango wa New Order
 
Back
Top Bottom