Asili ya nguvu za mafisadi Tanzania

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,079
28,733
Tunasoma maandiko matakatifu kitabu cha Waamuzi habari za Samsoni alivyotoa siri ya asili ya nguvu zake kwa mke wake mfilisti [Palestine] mrembo Delila.Delila alitumia udhaifu wa Samsoni hadi akafanikiwa kujua asili ya nguvu za Samsoni hatimaye Wafilisti wakatumia nafasi hiyo kumwadhibu Samsoni.

Tanzania inasumbuliwa na mafisadi kama wafilisti walivyokuwa wakisumbuliwa na nguvu za Samsoni miaka mingi iliyopita kabla kristo hajazaliwa.Nimejaribu kutafakari kidogo hizi nguvu za mafisadi asili yake nini yamkini tukijua asili ya nguvu za mafisadi tutaweza kupata namna bora ya kuziondoa nguvu walizo nazo.

Tanzania imemaliza uchaguzi wake mkuu siku chache zilizopita wote tumeshuhudia nguvu walizonazo mafisadi ndani ya CCM na baadae tumeziona zikifanyakazi nje ya CCM.Ndani ya CCM wapo waliokuwa wakijiita wapiganaji Seleli,Mwakyembe,Shelukindo Mr & Mrs,Tingatinga,A Kilango,Ole Sendeka na wengine wengi walikumbana na nguvu hizo kiasi kwamba wengine walishindwa kurejea mjengoni na waliofanikiwa kurejea walirejea na makovu kibao.Uchaguzi wa spika wa bunge la JMT mafisadi hawakubaki nyuma walihakikisha Samweli Sitta hafurukuti kwa namna yoyote.Hawakutaka jina lake liwafikie waheshimiwa wabunge pengine walijua nini kingetokea.

Shina kuu la Mafisadi ni uongozi wa juu wa CCM,nina maana kamati kuu na Halmashauri mkuu ya CCM taifa.Wajumbe wa kikao cha kamati kuu hawazidi 37 lakini maamuzi yao mabaya au mazuri yanagusa moja kwa moja maisha ya watanzania 43 milioni.Mafisadi wako mbele ya wakati kwa kutambua umuhimu wa kamati kuu walihakikisha wanajipenyeza na kuwa sehemu ya wajumbe.Wapo wajumbe wengi ambao majina yao yakitamkwa mbele ya jamii wanajulikana kujihusisha na kashfa mbali mbali.Kwenye kamati kuu ya CCM taifa wapo A Chenge,E Lowasa na Rostam Aziz.Wote watatu wamepata fedha nyingi kupitia serekali inayolea,kukuza,kulinda wala rushwa.

Siri ya asili ya nguvu walizonazo mafisadi ni kukata vyanzo vyote vya rushwa [Mikataba mibovu].Kazi hii inatarajiwa kufanywa na kambi mahiri ya upinzani ikiongozwa na Mbowe,Zitto,Tindu Lisu,Halima Mdee na wapiganaji wote walio tayari kuipigania Tanzania ya vizazi vijavyo.Fedha zote walizo nazo mafisadi wamezipata kupitia serekali dhaifu zilizopita na serekali iliyoko madarakani sasa.
 

Asili ya nguvu ya mafisadi ...

.... ni Udhaifu wa Ali Hassan Mwinyi + Unyonge wa Benjamin Willam Mkapa + Utoto wa Mrisho Jakaya Kikwete = UONGOZI USIO NA UADILIFU WALA MIIKO!!!
 

Asili ya nguvu ya mafisadi ...

.... ni Udhaifu wa Ali Hassan Mwinyi + Unyonge wa Benjamin Willam Mkapa + Utoto wa Mrisho Jakaya Kikwete = UONGOZI USIO NA UADILIFU WALA MIIKO!!!


Ewaah mkuu hapo tuko pamoja.
 

Asili ya nguvu ya mafisadi ...

.... ni Udhaifu wa Ali Hassan Mwinyi + Unyonge wa Benjamin Willam Mkapa + Utoto wa Mrisho Jakaya Kikwete = UONGOZI USIO NA UADILIFU WALA MIIKO!!!

Usisahau na "kulala kwa watanzania" maana sisi kila siku tunawapa madaraka kwa kura zetu huku tukijua ni mafisadi!
 
Elimu ya uraia ni muhimu sana wapinzani waanze kutoa darasa la nguvu kuanzia kusini mpaka kaskazini mashariki hadi magharibi uchaguzi wa vitongoji mwaka 2013 utatoa picha nzuri uchaguzi wa mwaka 2015.
 
richmond+lowassa.jpg
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom