Asili ya neno "salary" lenye maana ya mshahara

BigBaba

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
1,909
9,038
Asili ya neno "salary" (mshahara) linatokana na neno la Kilatini "sal' ama 'salarium' lililomaanisha "salt" (chumvi), zamani wakati wa Milki ya Warumi (Roman Empire) wanajeshi wa Kirumi walikuwa wakipewa pesa ndogo kwa ajili ya kununulia chumvi. Enzi hizo, chumvi ilikuwa bidhaa adimu na ya anasa, miaka ilivyozidi kwenda neno Salarium lilibadilika na kuwa Salary huku likitumiwa kumaanisha mshahara/ ujira wa kazi.
 
Ni hoja linalorudiwa mara nyingi lakini si kweli, angalau hakuna uthebitisho. Ni kweli ya kwamba neno "salarium" inahusiana na "chumvi" katika lugha ya kilatini. Lakini haijulikani jinsi lilivyohusiana nayo.
 
Mkuu,km sio Kweli,tuambie wewe sasa. Ili tujue kuwa alichokiandika mtoa post hakipo sahihi.
 
Anachosema iliwahi kuandikwa mara kadhaa na watu mbalimbali. Hata hivyo ukweli ni
1) kweli neno salary latokana na Kilatini salarium na maana yake kiasili ni "ki-chumvi" (salarium 'pertaining to salt'), baadaye pia "mshahara".
2) haijulikani jinsi gani gani maana hizi mbili zinahusiana. Hakuna ushuhuda wowote ya kwamba wanajeshi wao walilipewa chumvi.
3) Wakati mwingine ukweli ni "hatujui".

Labda (labda nyingine tena..) ilikuwa sawa na "chai" kwa Kiswahili. Chai ilikuwa neno la kudai hongo yaani malipo ya afisa nje ya utaratibu au kinyume ya sheria. Kama wanahistoria wanajadiliana maana ya neno "chai" baada ya miaka 1000 wanaweza kupata picha ya kwamba afisa wa polisi katika Afrika ya Mashariki alipokea sehemu ya mapato yake kwa "chai" - ila tu watashangaa kama ilimaanisha majani au kinywaji??

(kwa undani zaidi soma hapa: Kiwi Hellenist: Salt and salary: were Roman soldiers paid in salt?)
 
Chai pia ni uongo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom