Asili ya maneno "ball boy" na "clean sheet" kwenye mpira wa miguu

Srinivan Ramanujan

Senior Member
Nov 1, 2019
159
201
KIJUE CHANZO CHA MANENO "BALL BOY" NA "CLEAN SHEET"

☆Mwaka 1905,tajiri mmoja wa jiji la London huko England,alieitwa Gus Mears alianzisha klabu yake ya soka alioiita Chelsea Football Club.Klabu hii ikaanza kusajili wachezaji na mmojawapo alikuwa golikipa kutoka klabu ya Sheffield United alieitwa William Foulke ambaye alifahamika zaidi kama Fatty Willy au Amazing Bill.

☆Willy na Bill ni kifupisho cha jina William ambalo ndio jina lake rasmi.Aliitwa Fatty Willy au Amazing Bill kwa sababu ya umbo lake kubwa.Jamaa alikuwa bonge la pande mwenye kilo 150.

☆Kutokana na umbo lake kuwa kubwa,alikuwa mzito na mvivu sana.Aliposajiliwa huko Chelsea uzito wake uliongezeka zaidi na akawa mvivu zaidi.Hivyo alikuwa na vijana wadogo kwenye mechi ili wamsaidie kuokota mipira iliyotoka nje.Vijana hawa ndio wakasababisha kuwepo kwa "Ball Boys" kwenye mpira.

☆Alidumu Chelesea kwa msimu mmoja tu wa 1905/1906 na msimu uliofuata wa 1906/1907 akajiunga na klabu ya Bradford City.February 1907 kukawa na mechi dhidi ya Accrington Stanley, jezi ya Fatty Willy ilifanana na zile jezi za wapinzani, hivyo alitakiwa abadilishe.Kwa bahati mbaya hapajakuwa na jezi inayomtosha kwa sababu ya unene wake,hivyo akawa anaelekea kucheza kifua wazi, jambo ambalo lilionekana ni la kiungwana.

☆Ikabidi waende kuomba shuka kwenye nyumba za jirani na uwanja ili kumsaidia Fatty Willy ajistiri,likapatikana shuka jeupe, akajifunika na mechi ikachezwa, ilitarajiwa kuwa shuka lingechafuka sana kutokana na asili ya golikipa, kujirusha kudaka mipira.

☆Lakini shuka lile lilibaki safi hadi mwisho wa mchezo na Fatty Willy hakufungwa hata bao moja. Na hapo ndio pakapatikana msemo "Clean Sheet" yaani Shuka Safi. Na ndipo neno hilo likaingia kwenye mpira likimaanisha timu kutoruhusu bao kama timu ya Fatty Willy.

Nadhani hapo kila mtu kaelewa hayo maneno yametokana na nini.
 
Back
Top Bottom