Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 34,668
- 40,916
Hivi majuzi ikabuka hoja jamaa anadai mwanae anataka kubadili jina kisa hajavutiwa na aina ya matukio aliyokuwa nayo mwenye jina kama lake.
Mzazi anadai aliamua kumpa jina hilo mwanae baada ya kusoma hadithi za mhusika kwenye biblia.
Kwa muda mrefu sasa wazazi wamekuwa na haki ya kwanza ya kuwapa watoto wao majina.
Lakini je ni wote ambao wanayafurahia majina waliyopewa na wazazi wao? Je, kubadili jina ni kuwakosea wazazi heshima??
Mimi langu naambiwa kilifanyika kikao cha familia ikapigwa kura, jina lililopendekezwa na wengi ndio nililopewa, kwa kuzingatia hilo na kwa maana ya jina lenyewe nikaona ni sahihi kuwa nalo.
Majina hubeba maana kubwa sana kimaisha hivyo ni mihimu anayelibeba aridhike nalo. Je jamii iendelee na utaratibu huu huu wa kuwapa wazazi haki ya kuendelea kuwapa majina watoto wao, au majina wanayopewa watoto yawe ya muda tu kusubiria kuidhinishwa na mhusika pale anapofikia umri wa kufanya maamuzi??