Wandugu majina ya maeneo mbalimbali hapa TANZANIA na asili yake hebu tukumbushane machache kati ya haya :-

-KARIAKOO-carrier cool
-MSASANI-musa hasan
-BAGAMOYO-bwaga moyo

eti kuna maeneo mengine mnayoyajua ama ni haya haya au yapo mengine.

bora ungelala usingizi kuliko kupost upongo huu.
 
Kariakoo ni Carier Cops
 
Kistaarabu wakuu hatusemi Umesema uwongo tunasema sio kweli,ambayo haimuzi sana.

Upanga -lilikuwa pori na majambazi yenye mapanga yalikuwa yanajificha huko.
 
bora ungelala usingizi kuliko kupost upongo huu.

haya utingo,cjui umekosa cha kusema ama vp?okey nadhani jina lako na kile ulichoandika vinaendana,okey wewe ni utingo wa daradara au wa mabasi ya mikoani.

-do u the origin of ur name utingo ama?
 
ILALA = Ni kutokana na sauti za misikitini wakati huo -- Lai la la aila (sijui ni hivyo?)
SHAURIMOYO = Ilitokana na ujambazi uliokuwepo maeneo ya mitaa hiyo wakati huo. Watu wakawa wanasema inabidi uushauri moyo wako kabla ya kukatiza eneo hilo.
 
Wandugu majina ya maeneo mbalimbali hapa TANZANIA na asili yake hebu tukumbushane machache kati ya haya :-

-KARIAKOO-carrier cool
-MSASANI-musa hasan
-BAGAMOYO-bwaga moyo

eti kuna maeneo mengine mnayoyajua ama ni haya haya au yapo mengine.

kariakoo=carry n go
 
buguruni=bupuruni yaani kwenye vibupuri.

vibupuri ni vibanda vya kuatamia ndege kwenye mashamba ya mpunga. inasemekana hapo zamani za kale buguruni ilikuwa sehemu maarufu kwa mashamba (majaluba) ya mpunga
 
ILALA = Ni kutokana na sauti za misikitini wakati huo -- Lai la la aila (sijui ni hivyo?)
SHAURIMOYO = Ilitokana na ujambazi uliokuwepo maeneo ya mitaa hiyo wakati huo. Watu wakawa wanasema inabidi uushauri moyo wako kabla ya kukatiza eneo hilo.

Nadhani mpaka sasa mtaa ule unaendeleza asili yake maana pale kwenye kona ya shauri moyo na nyerere ukizubaa tu unalizwa especial mida ya giza giza kisha wanatokomea kwenye miti ya relini au chini ya daraja.

Singida

Mitunduruni - Kulikuwa na miti ya mitunduru mingi
Kibaoni - Kulikuwa na kibao Karibu singida

Dodoma - idodomiya (tembo alidodomea sehemu ya kikuyu "shule ya mazengo")

Mnadani - kwasababu kulikuwa na mnada
Uhindini - kwa kuwa wanaoishi sehemu hiyo majority ni wahindi
Kilimani - kuna kilima kuelekea mlima wa mkalama
Kikuyu - Kwa sababu kuna miti mingi ya mikuyu
Mahemani - kwasababu kulikuwa na mahema enzi hizo

Tanga

Kwedikwazu - Kwa dikwazu mtu maarufu aliejulikana kwa jina la dikwazu
Majani mapana - asili yake ni mti ya mitiki
Mabanda ya papa linajieleza
Komesho - Chuo cha Commercial
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom