Ashinda tuzo ya mwaka akiwa mahabusu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
Ashinda tuzo ya mwaka akiwa mahabusu.jpg

Kwa ufupi
Mgoba amepata tuzo hiyo ya mwaka kutokana na juhudi alizozifanya 2015 za kuwatetea vijana waliokuwa wanataka kuandamana kushinikiza Serikali kutoa ajira kwa vijana waliomaliza mafunzo hayo.


By Kalunde Jamal, Mwananchi kjamal@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THDRC) umempa tuzo ya mwaka George Mgoba, aliye mahabusu akikabiliwa na shtaka la kuandaa kinyume cha sheria maandamano ya vijana waliomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kushinikiza kupatiwa ajira.

Mgoba amepata tuzo hiyo ya mwaka kutokana na juhudi alizozifanya 2015 za kuwatetea vijana waliokuwa wanataka kuandamana kushinikiza Serikali kutoa ajira kwa vijana waliomaliza mafunzo hayo.

Mkurugenzi wa THDRC, Onesmo Ole Ngurumwa alisema suala la haki za binadamu linabaki pale pale bila ya kujali mhusika amefanya nini na anastahili adhabu gani iwapo itathibitika ana hatia.

Alisema utatuzi wa tatizo la ukiukwaji wa sheria kama upo uangaliwe ni kwa kiasi gani unafanyika bila kuathiri maisha ya binadamu na kumuondolea thamani yake.

“Kauli mbiu ya mwaka huu inasema “Tuwalinde Watetezi wa Haki za Binadamu”, ndiyo maana tumeona ni fursa ya kumkumbuka Mgoba ambaye hadi sasa anaumwa na bado ni mahabusu kwa zaidi ya mwaka kwa kuwa na alipata matatizo hayo akiwa anatetea haki za wengine na yake kama binadamu,” alisema Ole Ngurumwa.
Chanzo.Ashinda tuzo ya mwaka akiwa mahabusu
 
Back
Top Bottom