Asha Rose Migiro Simama ujitetee mwenyewe! Kumbe Bibie umeng'olewa UN!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Asha Rose Migiro Simama ujitetee mwenyewe! Kumbe Bibie umeng'olewa UN!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Honolulu, Jul 13, 2012.

 1. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  Barely a week after the immediate former Deputy Secretary-General, Dr. Asha Rose Migiro returned to Tanzania after serving a five-year term at the helm of the world body, sources within the UN have hinted that poor performance and failure to fit "in the diverse and complicated body" were some of the reasons she was refused a contract renewal.

  "The position of the Deputy Secretary-General is complicated and demanding; it requires somebody who is experienced to efficiently run the Secretariat. Her biggest challenge was not understanding the politics at the world body and creating
  alliances," the source told Vox Media in a telephone conversation.

  Dr. Migiro is understood to have approached the African Group, the largest regional group comprising of 28 percent of all UN members, to ask for help in lobbying for her re-appointment, but her quest was rejected. "She wasn't popular amongst diplomats; so nobody listened to her. You should also recall that her appointment was widely criticized."


  In Dar es Salaam, a former senior ruling party secretariat member who worked closely with her in the same team before she assumed the UN post said her appointment was influenced by her personal relationship with President Jakaya Kikwete. It is understood that President Kikwete and UN Secretary-General Ban Ki-moon cultivated a close relationship when serving as foreign ministers for their respective governments.

  When it came for Ban Ki-moon to canvass for votes toward his UN bid, Tanzania's vote was predominant; Dr. Migiro was apparently battered with Kikwete's vote. But when Ban Ki-Moon recently decided to review his entire team in a bid to control growing criticism of his team, Dr. Migiro had to go for "poor performance and lack of experience required of staff with the top UN mandate."  SOURCE: Why Dr. Migiro lost her UN job | Vox Media | Get Informed, Inform others


  Translation:

  Kama juma moja baada ya aliyekuwa naibu katibu mkuu, Dr Asha rose Migiro kurejea Tanzania baada ya kutumika kwa muda wa miaka mitano katika Chombo cha umoja wa mataifa, vyanzo vya ndani vya umoja huo vimedokeza kwamba, udhaifu wake katika utendaji na kupwaya kwake katika kazi ni baadhi ya sababu zilizoletelezea akataliwe kuweka mkataba wa pili.

  Nafasi ya naibu katibu mkuu ni ngumu na inahitaji mtu mzoefu na mwenye ufanisi katika kuendesha sekretarieti. Changamoto kubwa iliyomkabili ilikuwa ni kukosa uelewa katika siasa za kimataifa na kujenga mshikamano, kimedokeza chanzo cha habari cha Vox Media katika mazungumzo ya simu.

  Imedhihirika pia kwamba, Dr Migiro alijaribu kujipigia debe kwa kundi la Afrika ambalo lina asilimia 28 ya wanachama wote wa umoja wa mataifa, akiwashawishi wamuunge mkono katika uteuzi wake mpya, lakini harakati zake zikakataliwa.
  Hakuwa na umaarufu wowote miongoni mwa wanadiplomasia, na hivi hakuna aliyemsikiliza. Pia ikumbukwe kwamba uteuzi wake wa awali ulikosolewa na wengi.

  Huko Dar es salaam, kiongozi mmoja mwandamizi wa zamani katika chama tawala aliyefanya kazi kwa karibu naye alisema kuwa uteuzi wa Dr Migiro ulisukumwa na uhusiano wake binafsi na rais Jakaya Kikwete.

  Inafahamika kwamba rais Kikwete na katibu mkuu Ban Ki-moon walikuwa na mahusiano ya karibu walipokuwa wote wakihudumu kama mawaziri wa mambo ya nje katika serikali zao.

  Hivi ulipofika wakati wa Ban Ki-moon kutazama sifa ya waombaji, ikaonekana kuwa mwombaji wa Tanzania yuko juu kwa sababu alisindikizwa na debe la rais Kikwete mwenyewe.

  Lakini hivi karibuni, Ban Ki-moon aliamua kupitia upya timu yake yote kwa nia ya kudhibiti malalamiko yaliyojitokeza katika timu yake, ndio maana ikabidi Dr Migiro aondoke kwa sababu ya utendaji mbovu na ukosefu wa uzoefu ambao unahitajika kwa wafanyakazi wa mamlaka ya juu ya umoja wa mataifa.
   
 2. sinafungu

  sinafungu JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2012
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 1,405
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  duuh inafanana na mhe mbunge wa ukerewe enzi hizo G MONGELA,aliaminiwa akapata nafasi kubwa kiuongozi ngazi ya kimataifa,kilichotokea ni aibu kwa taifa. ingawa tofauti ipo. hawa wanawake wa tanganyika watakuwa fit hadi pale watakapoweza kujitambua na kusimama wenyewe bila upendeleo. na kwa kuanzia kupata uzoefu wao wenyewe wanapaswa kwanza kuukataa upendeleo ktk nafasi zooote za uongozi(UONGOZI WA KUPEWA)
   
 3. Mangimeli

  Mangimeli JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  mshaaza majungu,wabongo bana.
   
 4. m

  markj JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  uyo ban ki-moon yy mwenyewe anafanya nini! ye si ndo mkuu! nisawa na yale yale ya kuvunja baraza la mawaziri tu! wakati UN inaendeshwa ki maslahi ya taifa fulani hapa duniani!mama huyo asingewafiti kwenye masilahi yao. si mnamuona koffi annan sasa ivi anavyowafiti kwenye masilahi yao! UN sawa na chama fulani hapa TZ
   
 5. m

  markj JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  huyu mama yupo vizuri tu! wazungu wafki tu!
   
 6. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Acha tukuchambue tuu mpaka tuchoke. Wewe mama migiro kaa kimyaaa! tumia busara ya malecela alisingiziwa kuwa kachukua hela ili kuwa kibara raisi wa Iran. Yeye hakujibu mpaka leo nawe fanya hivyox2. ukijifanya kujibu tuu watu watakusekilojo mpaka maisha yako ya shule ya msingi!
   
 7. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  acha mafumbo ya kuilaani marekani !maslahi ya marekani yanafaida kubwa kwa dunia kuliko maslahi ya Urusi(mlezi baba wa madikiteta duniani)! uwe na shukurani, unapata watalii wengi baada ya marekani kuitanganza serengeti, mlima kilimanjaro na zanzibar ktk CNN. huyo mrusi kakusaidia nini kama siyo kukuletea siasa zisizo jenga secondarina vyuo vikuu!
   
 8. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Toeni mifano jinsi alivyoshindwa ku perform elezeni kwa ufasaha jambo hata moja aloshindwa kuperform,mkiona kitu kwenye website basi mnajua ni Fact 100% CIA si iliipeleka America vitani Ghuba kwa taarifa za kuchonga itakuwa ya Migiro?.hana nia ya Urais msitanuke mishipa bure!
   
 9. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #9
  Jul 13, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  sema hivi; ameachia ili kujiandaa na duru za urais za Tanganyika.
   
 10. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #10
  Jul 13, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mimi kwa upande wangu sioni hata huyo Ban Kimoon anafanya nini huko UN, bora angemwacha mama wa watu amalizie hiyo miaka mitano maana wote hakuna wanachoweza kusimama na kusema wameisaidia dunia so kwangu wote ni WADHAIFU tu
   
 11. m

  markj JF-Expert Member

  #11
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  marekani kakusadia nini wewe! kweli we hujielewei! yani vyandarua feki ulivyoletewa kwenye dhiara ya bush ndo vimekuadaah! sasa hao watalii wamekusaidia nini wewe kama mtanzania? zaidi zaidi wamewaingizia fedha mafisadi wa mali asili tu! zanzibar wanafaidika na kitu gani kwa watalii zaidi yakuwa masikini tu! marekani ni tango tu! tena hapo anamasilahi yake ya kuiba iba tu! mmarekani hakusaidiii mapaka uwe na ndoa ya jinsia moja? we wa wapi mkuuu! mmarekani hana chochote alichoisadia tanzania cha maaana! zaidi ya kutuletea milipuko tu ya alozi zake hapa tz na kubadilishana ardhi kwa vyandarua! kumbe boya wewe eeeh! na gharama za maisha zinazidi panda sababu ya dola ya mmarekani! kumbe wewe huna uelewa wa kutosha eeeh! pamoja na kubalehe kwako bado unasema mmarekani kakusaidia! haya iyo CNN embu angalia kama hata kwenye utabiri wa hali ya hewa tu TZ inatajwa? mkuuu huna mashiko hata kidogo! na hao watalii asilimia kubwa hawatoki marekani nini! na kama CNN WANATANGAZA ML KLM WHY mpaka leo wazungu wengine wanajua uko kenya na wakija wanaingilia mawakala wa utalii huko kenya! soma mkuuu! itafute elimu vizuri upate uelewa! ukita kujua wanammasilahi yao mbona hawakujenga reli hadi ipitie kwenye mbuga kama sio wizi tu! wao wenyewe wanakuambia HAWANA ADUI WA KUDUMU WALA RAFIKI WA KUDUMU, WAKO KWA AJILI YA MASILAHI YAO BINAFSI. upo hapo. ni hayo tu....
   
 12. m

  markj JF-Expert Member

  #12
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  mkuu! ndio yaleyale ya kuvunja baraza la mawaziri tu! UN hawana kazi yyt kazi kujali taifa fulani tu! uyo ban ni moon kibaraka tu ni dhaifu
   
 13. owawajr

  owawajr Member

  #13
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 30, 2009
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Migiro jitokeze utuambie ukweli kuhusu mkataba wako na uwakilishi wa Taifa letu katika chombo hiki
   
 14. K

  Kidogo chetu JF-Expert Member

  #14
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 771
  Trophy Points: 280
  heri wewe ylopewa upeo ukayajua haya !!!
   
 15. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #15
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu mazaa ana nywele kweli? Nasihi ni kipara maana miaka yote yuko kwenye hili wigi. Shee!
   
 16. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #16
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,631
  Trophy Points: 280
  bankimoon ni mshenzi tu mwingine
  amekula matapishi yake mwache yamkute ...sidhan cheo kikubwa cha UN kinaitaji Technical Know "WHO"
  Na sidhani Asha anaitaji kulalamikiwa mlaumu raisi wako aliempendekeza na kuona anafaa ama kwa namna moja ama nyingine so sidhan wakati muafaka wa kumshambulia bibie tuanze kumshambulia mh anaechagua watu .....na ningeona nivyema ungenza na wale watoto wanaojiita ma DC
   
 17. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #17
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,631
  Trophy Points: 280
  achague hiko kichwa kikistaafu aone shuguli yake
   

  Attached Files:

 18. wehoodie

  wehoodie JF-Expert Member

  #18
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 780
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 80
  wazungu wanajua kupiga vita sana muafrika akishika mashirika yao makubwa yenye ulaji. Mama Tibaijuka alipigwa vita sana UN habitat Nairobi mpaka wafanyakazi wakenya wakawa wanamtetea. Anyways atleast amekaa miaka mitano si haba.....lakini kuna kajiukweli hapo kwa ****** kuendeleza sera za kirafiki.
   
 19. p

  piason New Member

  #19
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani mliambiwa huyo Asharose ni malaika wa mbinguni mwenye uwezo wote? Uwezo wa binadamu una mipaka na mpaka wa Asharose ndio huo, hivi ungepelekwa wewe ungemaliza hata wiki? Acheni hizo tumpongeze mwenzetu hata kwa kule kuthubutu na kudumu hiyo miaka mitano.
   
 20. m

  mullay Member

  #20
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Me mwenyewe nampongeza mwanamke mwenzangu. huyo ban kimoon kafanya nin? kwanza baadhi ya watu wakajua koffi bado yupo kwenye nafasi maan yeye hata hasikiki kabisa.
   
Loading...