Elections 2010 Asha Rose Migiro for President 2010

Nyani Ngabu said:
Okay, si alikuwa waziri huyu? Kama ni hivyo basi pia alikuwa mbunge. Huko bungeni mchango wake ulikuwa nini? Alisimamia nini? Vipi kuhusu ufisadi? Aliupinga kwa kadri ya uwezo wake? Alipendekeza bill ngapi na zipi?


Nyani Ngabu,

..Dr.Migiro alikuwa mbunge wa viti maalum kupitia CCM. pia baada ya kupata nafasi ya ubunge moja kwa moja aliteuliwa kuwa Waziri wa Maendeleo ya Wanawake na Watoto.

..mchango wa Dr.Migiro kama mbunge ni tofauti na ule wa kina Dr.Slaa,Zitto,Selelii,Kilango, katika masuala ya ufisadi. kama tunataka kumpima kuhusu alivyopambana na ufisadi tuangalie utendaji wake kama Waziri ktk wizara ya wanawake na maendeleo ya Jamii, na wizara ya mambo ya nje.

..mpaka sasa hivi sijasikia kuwa Dr.Migiro alikuwa na kashfa yoyote ile akiwa Waziri wa wanawake na maendeleo ya jamii, au waziri wa mambo ya nje. nadhani huo ni mwanzo mzuri. kitu ambacho nitapenda kukisikia ni mabadiliko gani aliyasimamia akiwa waziri ktk wizara hizo mbili.

..kwa upande mwingine, Dr.Migiro ni mmoja kati ya kina mama wanaharakati waliokuwa wakifanya kazi ya uanasheria wa kujitolea kusaidia wanawake wasiojiweza waliohitaji msaada wa kisheria. nadhani rekodi hiyo inaweza kutoa mwanga, kwamba linapokuja suala la HAKI haswa za wanyonge, UTAWALA WA SHERIA NA KATIBA, mama Migiro atasimamia wapi.

NB:

..nchi za magharibi zinai-undermine UN halafu wanazunguka na kudai it is an irrelevant institution.

..naamini UN imefanya kazi kubwa sana, and it is relevant, katika masuala kama elimu[unicef], afya[who], maji na makazi[habitat], and relief operations[unhcr].
 
Nyani Ngabu,..mchango wa Dr.Migiro kama mbunge ni tofauti na ule wa kina Dr.Slaa,Zitto,Selelii,Kilango, katika masuala ya ufisadi.

Kwa nini mchango wake uwe tofauti? Ina maana wabunge wa kuchaguliwa na wale wa kuteuliwa wana masharti, majukumu, na job description tofauti? Sijaelewa hapo

kama tunataka kumpima kuhusu alivyopambana na ufisadi tuangalie utendaji wake kama Waziri ktk wizara ya wanawake na maendeleo ya Jamii, na wizara ya mambo ya nje..

Mimi nasema tuangalie kote alikopitia. Tusichague ya kuyaangalia hususan kama tunataka kuchagua kiongozi ambaye atakuwa kiongozi wa wote.
 
Nyani Ngabu,

..Dr.Migiro alichaguliwa ubunge na moja kwa moja akateuliwa kuwa Waziri.

..majukumu na michango ya Mawaziri Bungeni ni tofauti sana na yale ya Wabunge wa majimbo au wasio na wadhifa wowote serikalini.

..sijawahi kusikia Waziri akimuuliza Waziri mwenzake maswali ndani ya bunge. au kusikia Waziri akiuliza swali la nyongeza. sana sana Waziri anaweza kuchangia kwa kutoa mapendekezo, au kumsaidia Waziri mwenzake ktk kujibu maswali na kutoa ufafanuzi pale unapohitajika.

NB:

..Mawaziri wetu wanabanwa na utaratibu unaoitwa COLLECTIVE RESPONSIBILITY. ikitokea Waziri hakubaliani na uamuzi fulani wa serikali anapaswa kujiuzulu. Waziri akipinga uamuzi wa serikali hadharani[kama Lyatonga Mrema] ni sawa na amejifukuzisha kazi.
 
Nyani Ngabu,
..Dr.Migiro alichaguliwa ubunge na moja kwa moja akateuliwa kuwa Waziri.

..majukumu na michango ya Mawaziri Bungeni ni tofauti sana na yale ya Wabunge wa majimbo au wasio na wadhifa wowote serikalini.

Huu mfumo wa mawaziri kuwa wabunge ni flaw kubwa sana ktk serikali yetu. Sasa kwa mtu aliye waziri (ambaye pia atakuwa mbunge) atawakilisha vipi maslahi ya jimbo lake kama anabanwa na huo upuuzi wa collective responsibility. It makes no damn sense.
 

- Hizi dataz zako hazina ukweli wowote, Mama Miigiro na Baki-moon ni damu damu sana, haendi kokote yupo UN mpaka katibu wake atakapotoka, wabongo UN walidhani kwamba kwa sababu mbongo ameingia basi watapanda vyeo na kutesa kama vile siasa za bongo,

- Kumbe huko UN kuna miongozo ya sheria sasa ndio wamebaki kumzushia maneno ya uongo kila kukicha aibuu, inatia kichefu chefu sana kwa tunaoujua ukweli na tunaowajua wanaozusha haya maneno ya uongo na majungu! Mimi ninayo mpaka barua ya majungu aliyoiandika mtu mmoja huko UN na kunipa niiweke kwenye mitandao ili kumchafua huyu mama, wabongo bwana hata nje bado roho za kimasikini tu!

Respect.

FMEs!


Ukimtoa Nyani katika msitu wa Tanzania na kumweka katika msitu wa Marekani atabakia nyani yuleyule, kwa hiyo usitegemee mabadiliko.bado ni watanzania wale wale na asili yao bado ni ileile.
 
We are young nation with many problems.. some are the consequential of our encounters with foreign peoples, some are of our own corruption and wishes of our leaders to be like them and emulating their image of opulence and power.. to our general demise.. Lakini muamko ndio kama hivi... wananchi tunaongea... Dont underestimate the power of the internet...Nyerere never got this much criticism (mainly because he controlled information.. which was necessary to maintain control amidst the arm of foreign influence.. but it must also be said that it was convenient for him), mzee mwinyi the same and even mkapa.. we are getting a new voice to awake those that have access to it and in time they (or rather we) will awake a good portion of our society to stur a wave of consciousness about our current state of affairs and the future of our Nation, and then democracy will begin to take a life of its own and then we will have evolved in terms of being able to act (vote) in a manner that is in our best interest rather than the preservation of the status quo.. for reasons unbeknown to us!
 
Back
Top Bottom