Asha Mkwizu Hauli-Na kesi ya kumuua hawara wa mumewe

Mtambuzi, unaweza kuandika kitabu kizuri sana cha review ya imact ya mahusiano mabaya na athari kisheria na kisaikolojia... hizi cases zitatusaidia ku-cement athari mkuu. Nakumbuka nilikua primary, and i had to go stendi ya basi kumnunulia baba magazeti enzi hizo tulikua tunayapata kwa foleni na kugombania, ili tu asome hii kesi ya mkwizu....

I am touched!!

kila napokuwa bored huwa naanza kuchimbua archive ya jf, humu kuna treasure ya kutosha. miaka hiyo mimi nilikuwa primary pia, mzee alikuwa akiletewa magazeti ya kila siku ofisini, akirudi jioni ni kumendea tu akichukua hili mi nachukua lile, most of the time tulikuwa wawili tu hivyo nyumba nzima kimyaa! mkuu Mtambuzi, haujapakua zingine
 
Last edited by a moderator:
Nyc stori tupe y simbaulanga ile y kuiba 50m miaka ya 80.cz ilikua big story ila naskia alitoka huyo mama cz hela ilifanya kazu, 50m z nbc miaka hiyo ni bilionea hakimu au jaji akufunge atakua mjinga cz maisha yalikua tyt

Baada ya kusoma hii story Nilikuwa najiuliza huyu mama yuko wapi sasa , habari hii sikuisikia miaka hiyo pia kwa vile umri kidogo ulikuwa bado wa kuchezea makopo na Radio Tanzania kusikiliza ilikuwa ni mama na mwana natamani nijui huyu mama aliishia wapi
Mtambuzi kuja pande hii unichunguzie
 
Last edited by a moderator:
Hivi mpaka leo kesi ya mauaji kuna kuwa na jury wawili tu? Inashangaza sana kuwa Happiness amekubali kwenda kwa Asha, licha ya kuwa alikuwa akimchukulia mume wake ....
halafu nimeami ile kauli ya sikio la kufa...Nimejiuliza polisi ametangulia kuondoka polisi, badala ya kusepa kivyake, akawa anamsubiri israel...Sina jibu!
 
FirstLady1;

Kwa nchi za wenzetu jambo hili lingekuwa rahisi sana, lakini kwa hapa nchini ni vigumu sana kupata ushirikiano.

Nadhani pia ni kwa sababu za kiusalama, kumbuka kwamba ndugu zake Happiness Senzota hawakufurahia kifo cha ndugu yao, kwa hiyo inahitaji ujasiri kwa Asha Mkwizu kujitokeza na kuzungumza katika vyombo vya habari labda kama angekuwa anaishi ughaibuni.

Naona tuishie hapa maana maelezo ya kesi hii yamejitosheleza kabisa.

Dada yangu cacico aliwahi kusema tumuwache apumuwe.
 
Last edited by a moderator:
Mwita Maranya;

Kesi hii ni ya zamani lakini bado iko live kutokana na mambo yaliyojitokeza kuendelea kuonekana katika maisha yetu ya sasa,mtiririko wa kesi uko sawa na kesi imeonyesha ni jinsi gani kila upande unavyojitahidi kufanya kazi ili kupata kile kinachoitwa mafanikio.

Mwisho hata mimi naungana na Jaji kutoa hukumu ya kifo kwa muuaji kwani kilikuwa ni kifo cha kupanga.

Lakini pia mawakili wamefanya kazi nzuri kwani wanajaribu kuonyesha jinsi gani "Mteja"anavyosingiziwa kutenda kosa,wanaonyesha kuwa alichokifanya ni halali. Ni kazi ya mahakama kutafuta/kuonyesha haki ya kila mtu
 
Last edited by a moderator:
inasikitisha sana - dr hauli ndio pia aliyetoa ushahidi wa kidaktari kwenye kesi ya mke wa george liundi
Du hata mm imenitisha hii sentensi
lkn hawa Wangoni majina yao yanafanana tu kwani Hauli na Haule ni watu na koo tafauti hapo Mkuu
Katika ushahidi wa dr. Haule amesema kwamba katika uchunguzi wa kisasa, utofauti kati ya kurukwa na akili na kuondokewa kwa hali ya ubinadamu mkamilifu
Lkn wanaojua Mkwizu alipo au mtoto aliyebaki na mama kwa Mzee Liundi ni Taji atuhabarishe Mtambuzi ubarikiwe kwa kubaki JF hadi leo
 
Last edited by a moderator:
Verry interesting story miaka hiyo hata sijui Dunia ni nini,,,heshima yako mkuu Mtambuzi kutuletea kesi kama hizi naamini na mimi baadae nitawahadithia wajukuu zangu kesi za babu Seya na hila ya kufungwa kwao.
Note:-
Mapenzi mabaya sana hasa ukipenda na ukashindwa kuControl hasira zako.


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Last edited by a moderator:
Umenikumbusha mbali sana na ni jambo zuri sana unalolifanya...I doubt kama law schools za Tanzania wanatumia case zetu kufndisha au ni za kuimport tu bado...

Hizo zingine link iko wapi? Keep up doing the good work...

Hii case sikumbuki ilivyotoakea au wakati wa hukumu lakini nakumbuka jinsi huyo kaka yake Yahya Mkwizu alivyokua anahangaika kukusanya hela za kuappeal over and over again...Ndio mama akawa anatueleza ilitokea nini.

Kama sitakosea huyo Asha Mkwizu alishatoka jela nadhani na alibadislisha jina...I'm going to ask my mom about this.

But Mkwizu are really good people. Familia yao yote ni ya watu wazuri sana sana..Huyo kaka yake alihangaika sana sana kumshughulikia dada yake.

Ukiambiwa damu nzito kuliko maji hapo ndio unaelewa....Na alikua mswalihina sana lakini baada ya hizo trials and tribulations akaja kubadilisha dini..Sijui alichukia hiyo kitu ya kuoa wanawake wengi au ni something else. nadhani anaitwa hata jina lingine sio Yahaya tena.

Ila wanavyoelezea lakini huwezi kumjudge marehemu kwa vile hayupo kueleza upande wake lakini ni kuwa huyo mwanamke alikua anadharau nyingi sana na alishajifanya mke wa huyo Dr kabla hata hajaolewa na kijua fika alikua na mke mwingine. na hiyo kusema ugumba I don't think if it's true kwasababu walikua na watoto tayari. labda kama huyo baba alikua anataka watoto wengi. But nafikiria alikua ana watoto na huyu Asha tayari. Labda siku hiyo alisnap...

Na kama mtu unacheat na mwanamme wake kwanini uende nyumbani kwake tena? Na kama umeenda police kushitaki? Sasa iweje tena uwe so comfortable kwenda kwake peke yako? Some women!!!!!!!
 
Nchi hii rasilimali za Taifa zinatumika vibaya, hivi kweli kesi kama hii inachukua miaka miwili? Hii ingechukua mwezi mmoja tu! Kwa sababu:-

1: Mwanahamisi Happiness Senzota (Aliyeuawa) alilipoti Trh 19/11/1983 kuwa anatishiwa kudhuliwa na mtuhumiwa Asha Mkwizu. Na hii sijaiona sehemu yoyote imegusiwa either na mwendesha mashtaka, wazee wa baraza, mlinzi wa amani, mawakili wala Jaji! Walikuwa wanataka kuficha nini? Mtuhumiwa alikusudia kuua.

2: Majeraha matatu, mtuhumiwa mwanzo alisema alimpiga mara moja na chuma alipoanguka akajigonga na kusababisha majeraha mengine lakini baadaye alisema alimpiga zaidi ya mara moja na chuma! Huyu alikusudia.

3: Mussa alisema shimo lilichimbwa kabla hajatumwa sokoni, hivyo mauaji mpaka mzaishi yalipangwa mapema.

4: Mtuhumiwa alipomaliza kutekeleza mauaji, alikwenda kazini kama kawaida! Huyu hakurukwa akili wala hakuwa na hasira za kupindukia! Mtu akirukwa na akili au hasira za kupindukia hawezi kufanya shughuli zake kama kawaida! Huyu alikusudia kabisa!

Mimi ningekuwa ni Hakimu au Jaji, kesi za wazi kama hizi ni ndani ya mwezi tu kwishney. Huyu kitanzi ni halali yake.

NDIYO MAANA NAPENDA HUKUMU YA KIFO IENDELEE KUWEPO NA IWE INATEKELEZWA KWA KESI ZA WAZI KAMA HIZI.

Kumbe kesi zinazochukua muda mrefu hazina maana yoyote zaidi ya wanasheria na waendesha kesi kupoteza Muda na Rasilimali za Taifa kwa manufaa yao!
 
Anko Sam

ahsante kwa kuchambua hoja za kesi ya Asha

ingawa mswada huu ni kama umeisha pita lakini umenipitia mchoni kwa bahati tu niksema nikukumbushe jambo moja; upangaji wa kesi na vikao vya mahakama ni "sequence of events" huwezi kuwapata wapelelezi, majaji na mashahidi kwa wakati mmoja kama wabunge wanapatikana kwa muda maalum kwa kesi maalum hivyo ni muda! tofauti na court marshal inayoweza kukumaliza ndani ya siku 3!

na kama inavyosemekana Asha yuko nje basi tuamini msemo wa kisheria usemao "Law is an endless depth pitch" unaweza tumbukia either ufike chini ai usifike chini. Asha hakupatikana bayana akitenda kosa bali ni ushahidi wa kimazingira ambao ni kaburi. lakini sheria inatukumbusha kwamba, circumstantial evidence can convict when it has other supporting evidence. the evidence of Musa and that of Pw 10 makes the evidence congent against the acused where on other hand reveals the wilfulness of Asha to commit this offence whereby to exonerate her from the ditch was to make the charriot push the horse and not the horse pull the charriot.
 
Last edited by a moderator:
Kesi hii ina funzo, kwamba hapa duniani kila kitu ni ubatili.Ni bora kuangalia nafsi yako kwa maana kama Asha angeona kuwa haya maisha ni ubatili na kwamba Binadamu sio mtu wa kuweka tumaini kwake asingeua.

Asha yamkini alimpenda sana mumewe na kusahau Binadamu tu wanafiki.Hadi kufikia kufanya maamuzi magumu na yaliyomuharibiria maisha yake yote. Baada ya kugundua matatizo hayo, angeomba Mungu ampe moyo wa ujasiri kuyaona yote hayo ni sehemu ya maisha na kwamba yatapita tu.

Ahsante Mtambuzi kwa kumbukumbu.Maana umefanya kazi kubwa nikikumbuka majalada ya zamani yalivyo pale Mahakamani.
 
Dah kesi tam hii nilichopenda mahakama enzi hizo hazina ubabaishaji km Leo. Kesi hii leo ingeendeshwa miaka 5- 8. Lakini imetolewa hukumu ndani ya miaka 3 tu kweli nyerere ni baba wa taifa. Nafurahi huyo mama katumikia miaka 30 na kaachiwa huru baada ya miaka15.
 
F.y.i.... Prof Haule alikuwa daktari mtaalamu bingwa wa
magonjwa ya akili....yaani kama namuona na ndevu zake

Dr. Hauli, alikuwa daktari mwandamizi wa afya ya akili, lakini mpaka amestafu ajira ya serikali hakuwa amepata u-profesa, amefariki kama miaka minne iliyopita.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Dr. Hauli, alikuwa daktari mwandamizi wa afya ya akili, lakini mpaka amestafu ajira ya serikali hakuwa amepata u-profesa, amefariki kama miaka minne iliyopita.

May his Soul Rest In Peace.
Shukran kwa taarifa.
 
Back
Top Bottom