Asenga ashinda CCM Kilombero

ray jay

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
1,084
485
Hapa ifakara Jana jumapili wanaCCM walikuwa na mkutano wao wandani wa halmashauri kuu ya wilaya kujaza nafasi ya Mjumbe wao wa mkutano mkuu wa CCM Taifa ilioachwa wazi na Fredy Mwasakilale alieamia chama cha ACT Wazalendo wakati wa kampeni za ubunge 2015 Kabla ya kurudi tena CCM mapema

Uchaguzi ulionekana kuwa na mvuto wa aina yake hasa baada ya Vijana wa chadema kurudisha kadi ktk mkutano huo nakurudi CCM hasa Yule aliekuwa mpambe mkubwa wa mbunge wa kilombero Mr Lijualikali ktk stand ya mabus ifakara Mr Salum Akandu kurudi CCM nakumponda mbunge huyo na chama chake cha zamani

Baada ya taarifa hizo vijana wapambe Chadema walionekana wakizungukia uwanja huo wa ndani wa CCM wakishawishi Asenga asichaguliwe kwenye nafasi anayogombea ili kumshusha nguvu hasa ikizingatiwa Jimbo hilo linakesi ya uchaguzi itakayotolewa maamuzi july29 nakuwa tangu awe Ifakara vijana wengi wa chadema wamekuwa wakirudi CCM

Matokeo yalipotangazwa kati ya wagombea10 waliogombea na wajumbe 143
Asenga aliongoza kwa kura 97
Asha 64
Lukindo 48
Nk
My take Kama chadema imeanza kwa siasa mufilisi kiasi hiki
Kitazidi kuporomoka
b93e98b59d62fd69bf3d5b23b5eb56d8.jpg
db9fcc83a87078e70ad1799493e13b44.jpg
 
Huyo ambaye ameiga mpaka kuongea kwa Ridhiwan ndio ataimaliza chadema ya Lijualikali??
Mwambie Tumaini atulie,sisi tunamfuhamu kama Tumaini kabla ya kubadili jina na dini na kujiita Aboubakar Asenga pale alipochukuliwa kukaa na kuelelewa na familia ya JK
 
Aaah eti kalelewa na jk vp wewe mbona unalelewa na kijiji uongei..?
 
Hivi na huyu Asenga amekosa ukuu wa wilaya? Ni mmoja wale 46 walioombewa kazi na JK kwa JPM. Naona kaamua kuja kuanzisha uzi hapa kujifariji
 
Hivi si tulimsikia Mkuu wa nchi jana akiwaagiza Polisi kuhakikisha shughuli zote za kisiasa zinasitishwa hadi mwaka 2020?

Sasa iweje Polisi wa huko Kilombero washindwe kuusambaratisha mkutano huo wa CCM kwa magari ya washawasha?

Tunamsubiri Magu awatumbue majipu Askari wa huko ambao wamekatas 'kutii' agizo lake.

Iwapo Magu hatawatumbua maaskari hao tutagundua kuwa kumbe agizo lake limelenga kusitisha shughuli za kisiasa kwa vyama vya upinzani pekee!!!
 
Mikutano ya siasa ya wapinzani ndio iliyokatazwa hadi 2020...hao wa kijani wanasaidia kutimiza ilani ya chama.
Assenga hongera Sana.....na www soon utaula Kama wenzako.
 
Hivi si tulimsikia Mkuu wa nchi jana akiwaagiza Polisi kuhakikisha shughuli zote za kisiasa zinasitishwa hadi mwaka 2020?

Sasa iweje Polisi wa huko Kilombero washindwe kuusambaratisha mkutano huo wa CCM kwa magari ya washawasha?

Tunamsubiri Magu awatumbue majipu Askari wa huko ambao wamekatas 'kutii' agizo lake.

Iwapo Magu hatawatumbua maaskari hao tutagundua kuwa kumbe agizo lake limelenga kusitisha shughuli za kisiasa kwa vyama vya upinzani pekee!!!
Jifunze kujua tofauti kati ya kikao na mkutano ndiyo uje kuandika unachotaka kuandika.
 
Asenga hata udiwani hawezi kushinda Ifakara huo ndiyo ukweli. Yeye ataendelea kushinda uchaguzi ndani ya CCM lakini si uchaguzi wa vyama vingi.
 
Back
Top Bottom