Asemavyo Bashir Yakub kuhusu ACACIA kutosajiliwa Tanzania kisheria

mimi nadhani sasa ifike mahali wanasiasa wasiojielewa waache kuongoza hii nchi, na wale wanaojielewa wanapopata nafasi wasitoe nafasi za kiuongozi kwa wengine wasiowazalendo. Sheria zote na taratibu zote za madini tunazolalamikia leo zilipitishwa na wanasiasa waliopewa nafasi na kuaminiwa, sasa walivyokuwa wanapitisha hawakuwa wanajielewa?

Kinachofanyika sasa hivi wanacheka wenyewe baada ya kujitekenya wenyewe, lakini wanasahau hakuna aliyewatekenya. Uzalendo uanzie kwa viongozi waliopewa dhamana ya kuisimamia hii nchi.
 
UFAFANUZI MUHIMU KUHUSU USAJILI WA ACCACIA.

Waraka wa BASHIR YAKUB
+255784482959.

Kwa kutumia kigezo cha usajili, Tanzania tunazo aina kuu mbili za kampuni. Kampuni za ndani(Local companies) na kampuni za kigeni ( foreign companies).

Kampuni za ndani ni zile zote zilizoanzishwa hapa nchini na kusajiliwa hapa nchini. Hata kama wanahisa wake wote ni raia wa kigeni kwasababu tu ya kuanzishwa hapa na kusajiliwa hapa zinakuwa ni kampuni za ndani.

Kampuni ya kigeni ni ile iliyoanzishwa na kusajiliwa nje ya Tanzania lakini ikaanzisha ofisi/biashara/tawi hapa Tanzania. Sheria Na. 12 Sheria ya Makampuni kifungu cha 433 kinasema hivyo. Kampuni kama imeanzishwa nje hata kama wanahisa wake wote ni Watanzania, hapa kwetu hiyo bado ni kampuni ya kigeni.

Kampuni ya ndani inaposajiliwa hupatiwa cheti cha usajili kiitwacho "Certificate of Incorporation" kwa mujibu wa kifungu cha 15(2) Sheria ya Makampuni. Kampuni ya ndani inapopata cheti hiki basi usajili wake huwa umekamilika na inatambulika rasmi kama kampuni ya ndani.

Kampuni ya kigeni inaposajiliwa hapa Tanzania hupatiwa cheti kiitwacho "Certificate of Compliance" kwa mujibu wa kifungu cha 435(1) Sheria ya Makampuni. Kampuni ya kigeni inapopata cheti hiki basi usajili wake huwa umekamilika na hutambulika rasmi kama kampuni ya kigeni.

Acacia ni kampuni ya kigeni. Kwa maana kuwa ilianzishwa nje ya Tanzania na kufungua shughuli zake hapa nchini. Kwa hiyo ili ihesabike imesajiliwa Tanzania ilitakiwa kuwa na cheti kiitwacho"Certificate of Compliance". Kutokuwa na cheti hiki maana yake ni kuwa haijasajiliwa Tanzania na haitambuliki.

Nimesikia mjadala BBC SWAHILI leo wanaojadili wakijiuliza inawezekanaje kampuni kubwa kama hii ikafanya biashara bila usajili. Watanzania wengi pia wanajiuliza swali hili.

Jibu lake ni hili. Acacia ni kampuni tanzu(Subsidiary Company) ya Barrick. Kampuni inakuwa tanzu pale ambapo zaidi ya nusu ya hisa zake zinamilikiwa na kampuni nyingine. Ile inayomiliki huitwa "holding company" na inayomilikiwa huitwa "subsidiary company". Kwahiyo Barick ni " holding" wakati Acacia ni "subsidiary".

Barrick inamiliki hisa za Acacia 63.9%. Kwa kusema hivi maana yake Barrick ndiye mwenye Acacia. Hata hivyo kwa mujibu wa sheria hizi zinahesabika kampuni mbili tofauti na kila moja inabeba wajibu na hatia zake yenyewe(its own responsibility& liability).

Basi kumbe kilichotokea ni kuwa Acacia walikuwa wakifanya biashara kwa jina la Acacia lakini wakibebwa na mgongo wa Barrick. Walijificha hapa na wakaweza kuishi bila usajili wa kwao kama wao. Walijibeba kwenye usajili wa Barrick.

Barrick wao wanao usajili na wanayo " Certificate of Compliance" ya kwao ambayo tayari wameitoa hadharani. Kwakuwa haya ni makampuni mawili tofauti kila moja inatakiwa kuwa na cheti chake kwa mujibu wa kifungu cha 487 Sheria ya Makampuni na kutokufanya hivyo ni kosa kabisa. Kwa hiyo hivi ndivyo ilivyowezekana kampuni hii kufanya biashara bila usajili miaka hii yote.

Adhabu ya kosa kama hilo ni kifungo jela. Sheria Na. 12 Sheria ya Makampuni iliyofanyiwa Marekebisho mwaka 2002, kifungu cha 472 kinasema hivyo.
Nimekupata vizuri sana Mkuu ahsante kwa weledi wako mzuri kwa kufafanua bila jazba.
 
Swali langu la msingi.

Ni wakati gani wanatakiwa kuomba Certificate of Compliance kutoka BRELA?

Je wakati wanaomba kazi(tenda) ya kuchimba madini, gesi, umeme au Ujenzi?

Kama ni wakati washapata kazi(tenda), ni muda gani wanatakiwa kuomba Certificate of Compliance toka walipopata kazi?
 
Mtu yoyote anayepingana na Lisu ana akili za kushikiwa, Lisu na Lugemeleza Mshala waliteswa na Serikali ya Maccm kwa Ajiri ya Madini, Zitto Kabwe alifukuza Bungeni na Anna Mkinda kwa sababu ya utetezi wa sheria ya madini, Akaja Mh. Mku aliwakingia kifua kuwa HATUFUKUI Makabuli, leo sasa anaanza na Marehemu Kigoda hapo walio hai vipi?
 
Hapo Kuna magazijuto mengi sana...
What is acacia,
What is Barrick
What is bulyanghulu gold mine limited
What is buzwagi gold mine
Who and what is pangea gold mine
Kuna uhusiano au muingiliano gani Kati ya hivyo vitu hapo juu kisheria...

Hiki kimbunga CCM na serikali yake kama bila unafiki kitawakumba wengi sana humo ndani.
 
Mimi na muunga mkono Raisi,ila namaswali mengi sana kichwani kwangu.Kama haikusajiliwa kwa nini serekali haijaenda kuwashtaki mahakamani kwa uvunjaji wa sheria?Je tumeangalia sheria zetu zinasemaje kuhusu usajili wa makampuni?loopholes za usajili wa makampuni ya kigeni na uwekezaji upo?na tunarekebishaje.Je kwa nini tunawaomba Accacia watubu ndio tuwasamehe waendelee na uchimbaji.Je tuna create mazingira ya kiwatishia na hofu ili waogope?kwa nini kama wamevunja sheria zote hizo za nchi isifutwe kabisa na kushitakiwa.Mwenye majibu anisaidia jana nilokuwa busy sana natafuta mlo wa familia sikusikiliza sana




bora ulikua unafatilia mlo wa familia atleast, watu tulisimamisha kazi na walivyoanza kwa mbwembwe tulijua jana kuna mtu atanyongwa HADHARANI,matokeo yake ndo hayo ndugu yangu kwa KINYWA chake akasema waje watubu watulipe hela yetu,can u imagine?nilizima tv palepale
 
Hili ni aibu kwa viongozi changanya na wabunge wa ccm..wanapaswa kunyongwa hadharani...nawe rais ulikuwepo zaid ya miaka 15 mjengoni..tunakuunga mkono kaz hii lakini acha mbwembwe..ulishiriki dhhluma hii pamoja na maccm wengine huna cha kujitetea..usifanye nuru kuwa giza wala giza kuwa nuru. Ingawa wengine sisi hatuna vyama lakini tynakumbuka wapinzani walivyopinga jambo hili hadi wakafukuzwa bungeni ndo wale wazee wa ndiooooo wakapitisha uchafu huu. So rais ungekuwa na busara ukaonyesha appriciation hata kidogo kwa wapinzani kwa uzalendo wao kwanza ndo utaeleweka. Ukiendelea kuwaita si wazalendo eti ninyi ndo wazalendo huwezi someka. Utabak unapigiwa makofi na hao hao waliharibu nchi sisi wenye akili tutakuona unafanya siasa tu.
 
Ningependa huyu jamaa Bashir Yakub amfundishe Tundu kwani yuko juu sana na Tundu atafarijika sana kusomeshwa na huyu jamaa na heshima yake itarudi.
 
Umesomeka Mkuu. Umemzidi uwezo Tundu Lissu kwa mbali sana
Lissu ndo aliwaambia msifanye kazi yenu diligently? BRELA, TRA, TMAA, DSE hawa woote hawakuona ACACIA wanafanya kazi kinyume cha sheria?
Sielewi kwa nini mnautumia nguvu nyiingi kuhamiishia lawama kwa Lissu?
 
Adhabu ya kosa kama hilo ni kifungo jela. Sheria Na. 12 Sheria ya Makampuni iliyofanyiwa Marekebisho mwaka 2002, kifungu cha 472 kinasema hivyo.
Ni nani sasa anayefungwa jela? Kampuni au shareholders au ni nani? Naomba kueleweshwa maana mie mweupe kwenye sheria.
 
Kama Barick walitoa taarifa kuwa wanabadili jina,je sheria inasema kuwa waombe upya hiyo certificate of complience?.
Kama jibu ni ndio,watakuwa walichemsha na watang'ang'aniwa hapo hapo.
Kama wanapotoa taarifa automaticaly usajili unakuwepo based on ile certificate ya mwanzo watachomoka.
Lakini tena kama walitoa taarifa na BREAL wakatakiwa kuwapa usajili upya ila ukawepo urasimu mpaka Acacia ana operate kwa miaka 3 bila maofisa wa serikali kushituka na kufuatilia,then msajili wa makampuni analo la kujibu pia
 
Mimi na muunga mkono Raisi,ila namaswali mengi sana kichwani kwangu.Kama haikusajiliwa kwa nini serekali haijaenda kuwashtaki mahakamani kwa uvunjaji wa sheria?Je tumeangalia sheria zetu zinasemaje kuhusu usajili wa makampuni?loopholes za usajili wa makampuni ya kigeni na uwekezaji upo?na tunarekebishaje.Je kwa nini tunawaomba Accacia watubu ndio tuwasamehe waendelee na uchimbaji.Je tuna create mazingira ya kiwatishia na hofu ili waogope?kwa nini kama wamevunja sheria zote hizo za nchi isifutwe kabisa na kushitakiwa.Mwenye majibu anisaidia jana nilokuwa busy sana natafuta mlo wa familia sikusikiliza sana

You simply can't sue somebody who doesn't exist.
Acacia is an Unregistered Corporation therefore it does not exist de jure within our jurisdiction.

NB: The whole Process of registering a Corporate Entity ordains it with what we call LEGAL PERSONALITY. (The Company Becomes a person in law)

Legally Speaking, Acacia is not a Company but a caboodle of swindlers and economic saboteurs who vehemently work against the Strategic Interests of our Nation.
 
Back
Top Bottom