SoC01 “Asbestos” kemikali yenye madhara makubwa kiafya iliyosahaulika katika mazingira yetu

Stories of Change - 2021 Competition

genman

Member
Jul 14, 2021
37
100
ASBESTOS NI NINI?
Asbestos ni madini yanayochimbwa ardhini kama madini mengine. Kwa miaka iyoyopita asbsestos ilikuwa na bei nzuri katika soko la dunia kwa sababu ilikuwa na matumizi mengi katika viwanda. Tanzania asbestos inapatikana Ikorongo (Musoma), mbembe (Morogoro), Rubeho(Mpwapwa) na Haneti (Dodoma) lakini madini haya hayakuchimbwa kutokuwa na soko na hii ilitokana na kuzuiliwa kwa matumizi yake katika nchi mbalimbali duniani.(1)

KWA NINI ASBESTOS NI HATARI?
Asbestos ni mojawapo ya chemikali au taka hatarishi kama ilivyoelezwa katika repoti ya Sensa ya Mazingira Tanzania bara ya 2017,

(2) na katika report ya Mpango wa Taifa wa uthibiti wa taka ngumu Tanzania ya mwaka 2018.
(3) Asbestos ni hatari kwa sababu huwa ina uwezo wa kuvunjika kwenye vinyuzi vidogo sana ambavyo hunasa kwenye njia ya hewa kwa muda mrefu. Vinyuzinyuzi hivi vidogo huendelea kuingia kwenye njia ya hewa kadiri mtu anavyozidi kupumua na baadae hufika kwenye njia ya mapafu. vinyuzivinyuzi vikitua kwenye mapafu huweza kusababisha madhara kama vile kansa ya mapafu, asbestosis (seli za mapafu kudhurika) na “mesothelioma” kansa ya mfuko wa mapafu
(4). Kansa ya mapafu huweza kutokea ndani ya mwaka mmoja kwa mtu aliyepo katika mazingira yenye asbestos lakini pia yaweza kuchukua miaka 10 na zaidi kwa mtu kupata madhara.
(5)Kiasi kidogo sana cha asbestos huweza usababisha ugonjwa wa mesothelioma. Wanafamilia wa wafanyakazi wanaofanya kazi sehemu zenye asbestos waliweza kupata ugonjwa huu kutokana na mabaki ya asbestos katika nguo zao(5).Sio kila mtu aliye katika mazingira yenye asbestos anaweza kupata magonjwa yatokanayo na asbestos. Ingawa mtu yeyote aliye katika mazingira yenye asbestos ana uwezeano mkubwa wa kupata magonywa yanayosababishwa na asbestos. Magonjwa yatokanayo na asbestos ni vigumu kuyatibu na ni vigumu kupona.

Hivyo ni muhimu zaidi kujizuia kuwa katika mazingira yenye asbestos.

KWA NAMNA GANI VINYUZINYUZI VYA ASBESTOS HUINGIA HEWANI?
Vinyuzinyuzi vya asbestos huingia hewani wakati vifaa au vitu vilivyotengenezwa kwa asbestos vinapoharibika, kusuguana kwa kusogezwasogezwa au kuondolewa sehemu bila uangalifu. Asbestos inaposagika haitoi vumbi la kawaida, hutoa vinyuzinyuzi vidogo sana ambavyo siyo rahisi kuviona, kuhisi au kupata ladha/harufu yake. Kuna vifaa maalum ambavyo huweza utumika kugundua uwepo wa vinyuzinyuzi vya asbestos kwenye hewa.

Mtu yeyote ambaye yupo katika mazingira yenye vinyuzinyuzi hivi huweza kuvipumua na kuingia katika mfumo wake wa hewa. Madhara ambayo humtokea mtu hutegemea kiasi cha vinyuzinyuzi kilichopo hewani, muda ambao huyo mtu amekaa katika hayo mazingira na uwepo wa chemikali nyinginezo. Pia madhara hutofautiana kutokana na umri, jinsia, lishe, kinga ya mwili, mtindo ya maisha na afya ya mtu kwa ujumla.4)

UNAWEZA KUJUA KAMA UMEPUMUA VINYUZINYUZI VYA ASBESTOS?
Wataalam wanasema ni vigumu sana kujua kama umeathirika na vinyuzinyuzi vya asbestos kwa sababu havisababishi kupiga chafya au kukohoa mara na havina madhara kwenye ngozi.

KWA NAMNA GANI UNAWEZA KUJUA UMEATHIRIKA NA ASBESTOS?
Njia inayotumika kujua kama umeathirika na asbestos ni x-ray ya kifua au CAT scan. X-ray hutumika kugundua dalili za mwanzo za magonjwa yanayosababishwa na asbestos.

ASBESTOS INAPATIKANA WAPI KATIKA MAZINGIRA YETU?
Asbestos ipo kwa kiasi kikubwa Tanzania kwani vitu vyenye asbestos vinapatikana sehemu mbalimbali Tanzania nzima. Asbestos ilitumika katika kuezeka nyumba, kutengenezea mabomba, nguzo, vifaa vya umeme na vitu vingine vingi. Asbestos ilipendwa sana kutumika kwa sababu ni ngumu, haiozi au kupata kutu ikilowa pia haishiki moto. Hadi sasa asbestos iliyotumika miaka mingi iliyipita bado ipo katika mazingira yetu. Asbestos inapatikana katika majengo mengi ya zamani ya serikali kama vile ya shule na na hospitali na ya watu binafsi. Wananchi wameendelea kutumia mabaki ya bati za asbestos katika kuweka uzio na kujengea mabanda ya mifugo. Pia kuna mabomba yaliyotengenezwa kwa asbestos yamezikwa ardhini. Haya yalitumika katika mifumo ya maji safi na maji taka ambayo kwa sasa imekufa na haitumiki tena.

IMG_20210729_040758.jpg

Mabomba ya asbestos yaliyofukuliwa katika eneo la ujenzi wa barabara za mwendokasi awamu ya pili Dar es Salaam.

Asbestos imetumika sana katika kuezeka nyumba Tanzania. Katika report ya Makazi na Hali ya Jamii Kiuchumi Tanzania Bara (Basic Demographic and Socio-Economic Profile Report Tanzania Mainland) ya mwaka 2014 inaonesha kwamba asbestos ipo kwa asilimia 0.3% katika uezekaji wa majengo Tanzania bara ukilinganisha na mabati, zege na vigae6. Watu huvuna maji ya matumizi ya nyumbani katika maezeko haya ya asbestos. Hii ni kutokana kukosekana kwa elimu ya madhara ya asbestos katika jamii.

Screenshot_20210714-133918.jpg

Nyumba ambayo imeezekwa kwa asbestos
Chanzo: British lung cancer foundation

Kwa sasa haijalishi upo sehemu gani, kwa sababu katika mazingira yetu kuna vitu vingi au mabaki ya vitu ambavyo vimetengenezwa kwa asbestos. Hivyo mabaki ya asbestos yapo kwa kiasi kikubwa katika udongo. Pia watanzania wengi hawana uelewa kuhusu madhara ya asbestos hivyo wamekuwa wakikaa nazo katika mazingira yao bila kujua madhara yake. Watu wengi wamekuwa wakitumia vitu vyenye asbestos bila kujua hivyo kutochukua tahadhari yoyote.

IMG_20210728_160828.jpg

Bati za asbestos zilizoaribika zikiwa zimetupwa hovyo eneo la Mbagala

KWA NAMNA GANI ASBESTOS INAWEZA KUONDOLEWA KATIKA MAZINGIRA?
Katika nchi nyingi zilizoendelea kuna makampuni kadhaa yanayofanya kazi ya kuondoa asbestos katika mazingira. Kampuni hizo huwa na wataalamu na vifaa vya kugundua asbestos katika mazingira. Taasisi mbalimbali za kiserikali na binafsi huajiri kampuni hizi kuondoa asbestos katika mazingira yao.

JUHUDI ZA MATAIFA DUNIANI KUONDOA ASBESTOS KATIKA MAZINGIRA
Shirika la kazi duniani lilifanya mkutano wa makubaliano ya kimataifa mwaka 1986 ya kuthibiti uwepo wa asbestos katika mazingira. Nchi kadhaa kama vile Uganda na Zimbabwe ziliridhia makubaliano hayo lakini Tanzania ni mojawapo ya nchi ambazo hazijaridhia katika utekelezaji wa makubaliano hayo.
Kwa nchi nyingi kwa miaka kadhaa wamekuwa na kampuni mbalimbali ambazo hufanya kazi ya kuondoa asbestos katika mazingira lakini kwa Tanzania bado hatujaweza kufanya hivyo.

HITIMISHO
Katika nchi zinazoendelea kama Tanzania kumekuwa na maradhi mengi yatokanayo na taka hatarishi ambayo yanapunguza umri wa watu kuishi. Ni vyema serikali hasa kupitia vyombo vyake kama vile NEMC ikaongeza mikakati ya kuthibiti taka hatarishi hasa zilizosahaulika kama asbestos ili kulinda afya za watanzania. Wananchi wanatakiwa wapate elimu ya uelewa wa taka zote hatarishi ambazo zinapatikana katika mazingira yao na namna ya kujikinga nazo. Pia kuwe na mkakati wa kuondoa asbestos katika mazingira yetu. Juhudi hizi zikifanyika zitasaidia kulinda kizazi hiki na vijavyo.

REJEA
1. Jordan, P 1990. Mineral Industry Tanzania. Institute of Mineral Research of Zimbabwe. Report Number 119
2. United Republic of Tanzania, 2017, National Environment Statistics Report, Tanzania Mainland
3. United Republic of Tanzania, 2018, The National Solid Waste Management Strategy
4. Minnesota Department of Health. Environmental Health Division. Asbestos
https://www.health.state.mn.us/communities/environment/asbestos/homeowner/heffects.html
5. Boffetta P. 1998. Health effects of asbestos exposure in humans: a quantitative assessment. Med Lav.
6. United Republic of Tanzania, 2014, Basic Demographic and Socio-Economic Profile Report Tanzania Mainland.
 
ASBESTOS NI NINI?
Asbestos ni madini yanayochimbwa ardhini kama madini mengine. Kwa miaka iyoyopita asbsestos ilikuwa na bei nzuri katika soko la dunia kwa sababu ilikuwa na matumizi mengi katika viwanda. Tanzania asbestos inapatikana Ikorongo (Musoma), mbembe (Morogoro), Rubeho(Mpwapwa) na Haneti (Dodoma) lakini madini haya hayakuchimbwa kutokuwa na soko na hii ilitokana na kuzuiliwa kwa matumizi yake katika nchi mbalimbali duniani.(1)

KWA NINI ASBESTOS NI HATARI?
Asbestos ni mojawapo ya chemikali au taka hatarishi kama ilivyoelezwa katika repoti ya Sensa ya Mazingira Tanzania bara ya 2017,(2) na katika report ya Mpango wa Taifa wa uthibiti wa taka ngumu Tanzania ya mwaka 2018.(3)
Asbestos ni hatari kwa sababu huwa ina uwezo wa kuvunjika kwenye vinyuzi vidogo sana ambavyo hunasa kwenye njia ya hewa kwa muda mrefu. Vinyuzinyuzi hivi vidogo huendelea kuingia kwenye njia ya hewa kadiri mtu anavyozidi kupumua na baadae hufika kwenye njia ya mapafu. vinyuzivinyuzi vikitua kwenye mapafu huweza kusababisha madhara kama vile kansa ya mapafu, asbestosis (seli za mapafu kudhurika) na “mesothelioma” kansa ya mfuko wa mapafu(4). Kansa ya mapafu huweza kutokea ndani ya mwaka mmoja kwa mtu aliyepo katika mazingira yenye asbestos lakini pia yaweza kuchukua miaka 10 na zaidi kwa mtu kupata madhara.(5)
Kiasi kidogo sana cha asbestos huweza usababisha ugonjwa wa mesothelioma. Wanafamilia wa wafanyakazi wanaofanya kazi sehemu zenye asbestos waliweza kupata ugonjwa huu kutokana na mabaki ya asbestos katika nguo zao(5).
Sio kila mtu aliye katika mazingira yenye asbestos anaweza kupata magonjwa yatokanayo na asbestos. Ingawa mtu yeyote aliye katika mazingira yenye asbestos ana uwezeano mkubwa wa kupata magonywa yanayosababishwa na asbestos. Magonjwa yatokanayo na asbestos ni vigumu kuyatibu na ni vigumu kupona. Hivyo ni muhimu zaidi kujizuia kuwa katika mazingira yenye asbestos.

KWA NAMNA GANI VINYUZINYUZI VYA ASBESTOS HUINGIA HEWANI?
Vinyuzinyuzi vya asbestos huingia hewani wakati vifaa au vitu vilivyotengenezwa kwa asbestos vinapoharibika, kusuguana kwa kusogezwasogezwa au kuondolewa sehemu bila uangalifu. Asbestos inaposagika haitoi vumbi la kawaida, hutoa vinyuzinyuzi vidogo sana ambavyo siyo rahisi kuviona, kuhisi au kupata ladha/harufu yake. Kuna vifaa maalum ambavyo huweza utumika kugundua uwepo wa vinyuzinyuzi vya asbestos kwenye hewa. Mtu yeyote ambaye yupo katika mazingira yenye vinyuzinyuzi hivi huweza kuvipumua na kuingia katika mfumo wake wa hewa. Madhara ambayo humtokea mtu hutegemea kiasi cha vinyuzinyuzi kilichopo hewani, muda ambao huyo mtu amekaa katika hayo mazingira na uwepo wa chemikali nyinginezo. Pia madhara hutofautiana kutokana na umri, jinsia, lishe, kinga ya mwili, mtindo ya maisha na afya ya mtu kwa ujumla.4)

UNAWEZA KUJUA KAMA UMEPUMUA VINYUZINYUZI VYA ASBESTOS?
Wataalam wanasema ni vigumu sana kujua kama umeathirika na vinyuzinyuzi vya asbestos kwa sababu havisababishi kupiga chafya au kukohoa mara na havina madhara kwenye ngozi.

KWA NAMNA GANI UNAWEZA KUJUA UMEATHIRIKA NA ASBESTOS?
Njia inayotumika kujua kama umeathirika na asbestos ni x-ray ya kifua au CAT scan. X-ray hutumika kugundua dalili za mwanzo za magonjwa yanayosababishwa na asbestos.

ASBESTOS INAPATIKANA WAPI KATIKA MAZINGIRA YETU?
Asbestos ipo kwa kiasi kikubwa Tanzania kwani vitu vyenye asbestos vinapatikana sehemu mbalimbali Tanzania nzima. Asbestos ilitumika katika kuezeka nyumba, kutengenezea mabomba, nguzo, vifaa vya umeme na vitu vingine vingi. Asbestos ilipendwa sana kutumika kwa sababu ni ngumu, haiozi au kupata kutu ikilowa pia haishiki moto. Hadi sasa asbestos iliyotumika miaka mingi iliyipita bado ipo katika mazingira yetu. Asbestos inapatikana katika majengo mengi ya zamani ya serikali kama vile ya shule na na hospitali na ya watu binafsi. Wananchi wameendelea kutumia mabaki ya bati za asbestos katika kuweka uzio na kujengea mabanda ya mifugo. Pia kuna mabomba yaliyotengenezwa kwa asbestos yamezikwa ardhini. Haya yalitumika katika mifumo ya maji safi na maji taka ambayo kwa sasa imekufa na haitumiki tena.
View attachment 1872905
Mabomba ya asbestos yaliyofukuliwa katika eneo la ujenzi wa barabara za mwendokasi awamu ya pili Dar es Salaam.

Asbestos imetumika sana katika kuezeka nyumba Tanzania. Katika report ya Makazi na Hali ya Jamii Kiuchumi Tanzania Bara (Basic Demographic and Socio-Economic Profile Report Tanzania Mainland) ya mwaka 2014 inaonesha kwamba asbestos ipo kwa asilimia 0.3% katika uezekaji wa majengo Tanzania bara ukilinganisha na mabati, zege na vigae6. Watu huvuna maji ya matumizi ya nyumbani katika maezeko haya ya asbestos. Hii ni kutokana kukosekana kwa elimu ya madhara ya asbestos katika jamii.
View attachment 1872909
Nyumba ambayo imeezekwa kwa asbestos
Chanzo: British lung cancer foundation

Kwa sasa haijalishi upo sehemu gani, kwa sababu katika mazingira yetu kuna vitu vingi au mabaki ya vitu ambavyo vimetengenezwa kwa asbestos. Hivyo mabaki ya asbestos yapo kwa kiasi kikubwa katika udongo. Pia watanzania wengi hawana uelewa kuhusu madhara ya asbestos hivyo wamekuwa wakikaa nazo katika mazingira yao bila kujua madhara yake. Watu wengi wamekuwa wakitumia vitu vyenye asbestos bila kujua hivyo kutochukua tahadhari yoyote.
View attachment 1872912
Bati za asbestos zilizoaribika zikiwa zimetupwa hovyo eneo la Mbagala

KWA NAMNA GANI ASBESTOS INAWEZA KUONDOLEWA KATIKA MAZINGIRA?
Katika nchi nyingi zilizoendelea kuna makampuni kadhaa yanayofanya kazi ya kuondoa asbestos katika mazingira. Kampuni hizo huwa na wataalamu na vifaa vya kugundua asbestos katika mazingira. Taasisi mbalimbali za kiserikali na binafsi huajiri kampuni hizi kuondoa asbestos katika mazingira yao.

JUHUDI ZA MATAIFA DUNIANI KUONDOA ASBESTOS KATIKA MAZINGIRA
Shirika la kazi duniani lilifanya mkutano wa makubaliano ya kimataifa mwaka 1986 ya kuthibiti uwepo wa asbestos katika mazingira. Nchi kadhaa kama vile Uganda na Zimbabwe ziliridhia makubaliano hayo lakini Tanzania ni mojawapo ya nchi ambazo hazijaridhia katika utekelezaji wa makubaliano hayo.
Kwa nchi nyingi kwa miaka kadhaa wamekuwa na kampuni mbalimbali ambazo hufanya kazi ya kuondoa asbestos katika mazingira lakini kwa Tanzania bado hatujaweza kufanya hivyo.

HITIMISHO
Katika nchi zinazoendelea kama Tanzania kumekuwa na maradhi mengi yatokanayo na taka hatarishi ambayo yanapunguza umri wa watu kuishi. Ni vyema serikali hasa kupitia vyombo vyake kama vile NEMC ikaongeza mikakati ya kuthibiti taka hatarishi hasa zilizosahaulika kama asbestos ili kulinda afya za watanzania. Wananchi wanatakiwa wapate elimu ya uelewa wa taka zote hatarishi ambazo zinapatikana katika mazingira yao na namna ya kujikinga nazo. Pia kuwe na mkakati wa kuondoa asbestos katika mazingira yetu. Juhudi hizi zikifanyika zitasaidia kulinda kizazi hiki na vijavyo.

REJEA
1. Jordan, P 1990. Mineral Industry Tanzania. Institute of Mineral Research of Zimbabwe. Report Number 119
2. United Republic of Tanzania, 2017, National Environment Statistics Report, Tanzania Mainland
3. United Republic of Tanzania, 2018, The National Solid Waste Management Strategy
4. Minnesota Department of Health. Environmental Health Division. Asbestos
https://www.health.state.mn.us/communities/environment/asbestos/homeowner/heffects.html
5. Boffetta P. 1998. Health effects of asbestos exposure in humans: a quantitative assessment. Med Lav.
6. United Republic of Tanzania, 2014, Basic Demographic and Socio-Economic Profile Report Tanzania Mainland.
Nakumbuka chuo tulisoma kuhusu hizi asbestos na namna inavyosababisha ugonjwa mbaya wa Asbestosis ambao hauna tiba.. kwa Afrika nchi ya Afrika ya kusini ilikuwa miongoni mwa nchi za awali kusitisha matumizi yake.. na ndio walikuwa watumizi wakubwa wa bati za material ya asbestos hasa kwa wakazi wa kipato cha kati na chini.... SLOW SILENT KILLER..
Tanzania naona mabati ya asbestos yametumika sana kwenye majengo ya shule za zamani hasa za bweni na nyumba za watumishi pia quarters hasa za walinda raia na mali zao, mbaya zaidi zile zinazoezuliwa ili kuweka bati mpya zinatumika kutengenezauzio ...

Uzi muhimu sana huu..
 
Shida kubwa ya Wazungu wakishaona kitu hakina Maslahi kwao ya Kiuchumi lazima waanze kukupigia vita na kueleza madhara Mengi. Tunaenda tena huko wanakataa gari za mafuta utasikia madhara ambayo hukuwahi kuyajua ya fuel
Una faida sana kwa mzungu ukiwa hai kwa vile wewe ni masoko ya bidhaa zake.... akuache uchapike na asbestosis ili apunguze consumers wa bidhaa zake nyingine!! Usitishwaji wa material yenye hizyo content ni toka miaka ya "1980's" huko. Hiyo vita ya kiuchumi unashindana naye nini (bajaj inakimbizana na subaru)
 
kweli kabisa mkuu
 
Asante
Wazo lako ni zuri sana
Ila sasa changamoto ipo ivi
Tatizo linaanzia mbali kumbuka haya ni madini yanayochimbwa hivyo tatizo litaanzia mgodini kwa wale wachimbaji lazima wataathirika na vumbi litokanalo na uchimbaji na hata wakijikinga sana kumbuka vumbi linaweza kuchukuliwa na upepo na kwenda kuwaathiri watu wengine. Pili madini haya yakishachimbwa yatapelekwa kiwandani ambapo pia wakati wa kuchakata vumbi linaweza kuwaathiri wafanyakazi. Wafanyakazi wa viwandani ndio walikuwa waathirika wakubwa kwa vumbi la asbestos kuliko hata waliotumia bidhaa za asbestos. Nadhani kutokana na haya ndio maana wazungu wakakosa mbinu mbadala na kuamua kuachana na asbestos kabisa
asante sana mchangiaji
Well emphasise !
 
Hili bandiko ni zuri sana. Sijui ni kwanini hata sikuliona mapema.

Mafundi wa magari mnaofanya Brake service, Lile vumbi linalotokana na Brake linings za shoes au Pads limecontain asbestos.

Kwa mazingira yalivyo maeneo mengi huenda watu wanalivuta au kulishika. Hii inaweza kuwaletea madhara.
Hivi brake shoe za pikipiki zimeundwa kwa bidhaa hii pia?
 
Ndio maana mabati yaliotengezwa enzi hizo mpaka sasa bado lipo vile bile ma haliozi hata uliloweke kwenye dimbwi
 
ASBESTOS NI NINI?
Asbestos ni madini yanayochimbwa ardhini kama madini mengine. Kwa miaka iyoyopita asbsestos ilikuwa na bei nzuri katika soko la dunia kwa sababu ilikuwa na matumizi mengi katika viwanda. Tanzania asbestos inapatikana Ikorongo (Musoma), mbembe (Morogoro), Rubeho(Mpwapwa) na Haneti (Dodoma) lakini madini haya hayakuchimbwa kutokuwa na soko na hii ilitokana na kuzuiliwa kwa matumizi yake katika nchi mbalimbali duniani.(1)

KWA NINI ASBESTOS NI HATARI?
Asbestos ni mojawapo ya chemikali au taka hatarishi kama ilivyoelezwa katika repoti ya Sensa ya Mazingira Tanzania bara ya 2017,

(2) na katika report ya Mpango wa Taifa wa uthibiti wa taka ngumu Tanzania ya mwaka 2018.
(3) Asbestos ni hatari kwa sababu huwa ina uwezo wa kuvunjika kwenye vinyuzi vidogo sana ambavyo hunasa kwenye njia ya hewa kwa muda mrefu. Vinyuzinyuzi hivi vidogo huendelea kuingia kwenye njia ya hewa kadiri mtu anavyozidi kupumua na baadae hufika kwenye njia ya mapafu. vinyuzivinyuzi vikitua kwenye mapafu huweza kusababisha madhara kama vile kansa ya mapafu, asbestosis (seli za mapafu kudhurika) na “mesothelioma” kansa ya mfuko wa mapafu
(4). Kansa ya mapafu huweza kutokea ndani ya mwaka mmoja kwa mtu aliyepo katika mazingira yenye asbestos lakini pia yaweza kuchukua miaka 10 na zaidi kwa mtu kupata madhara.
(5)Kiasi kidogo sana cha asbestos huweza usababisha ugonjwa wa mesothelioma. Wanafamilia wa wafanyakazi wanaofanya kazi sehemu zenye asbestos waliweza kupata ugonjwa huu kutokana na mabaki ya asbestos katika nguo zao(5).Sio kila mtu aliye katika mazingira yenye asbestos anaweza kupata magonjwa yatokanayo na asbestos. Ingawa mtu yeyote aliye katika mazingira yenye asbestos ana uwezeano mkubwa wa kupata magonywa yanayosababishwa na asbestos. Magonjwa yatokanayo na asbestos ni vigumu kuyatibu na ni vigumu kupona.

Hivyo ni muhimu zaidi kujizuia kuwa katika mazingira yenye asbestos.

KWA NAMNA GANI VINYUZINYUZI VYA ASBESTOS HUINGIA HEWANI?
Vinyuzinyuzi vya asbestos huingia hewani wakati vifaa au vitu vilivyotengenezwa kwa asbestos vinapoharibika, kusuguana kwa kusogezwasogezwa au kuondolewa sehemu bila uangalifu. Asbestos inaposagika haitoi vumbi la kawaida, hutoa vinyuzinyuzi vidogo sana ambavyo siyo rahisi kuviona, kuhisi au kupata ladha/harufu yake. Kuna vifaa maalum ambavyo huweza utumika kugundua uwepo wa vinyuzinyuzi vya asbestos kwenye hewa.

Mtu yeyote ambaye yupo katika mazingira yenye vinyuzinyuzi hivi huweza kuvipumua na kuingia katika mfumo wake wa hewa. Madhara ambayo humtokea mtu hutegemea kiasi cha vinyuzinyuzi kilichopo hewani, muda ambao huyo mtu amekaa katika hayo mazingira na uwepo wa chemikali nyinginezo. Pia madhara hutofautiana kutokana na umri, jinsia, lishe, kinga ya mwili, mtindo ya maisha na afya ya mtu kwa ujumla.4)

UNAWEZA KUJUA KAMA UMEPUMUA VINYUZINYUZI VYA ASBESTOS?
Wataalam wanasema ni vigumu sana kujua kama umeathirika na vinyuzinyuzi vya asbestos kwa sababu havisababishi kupiga chafya au kukohoa mara na havina madhara kwenye ngozi.

KWA NAMNA GANI UNAWEZA KUJUA UMEATHIRIKA NA ASBESTOS?
Njia inayotumika kujua kama umeathirika na asbestos ni x-ray ya kifua au CAT scan. X-ray hutumika kugundua dalili za mwanzo za magonjwa yanayosababishwa na asbestos.

ASBESTOS INAPATIKANA WAPI KATIKA MAZINGIRA YETU?
Asbestos ipo kwa kiasi kikubwa Tanzania kwani vitu vyenye asbestos vinapatikana sehemu mbalimbali Tanzania nzima. Asbestos ilitumika katika kuezeka nyumba, kutengenezea mabomba, nguzo, vifaa vya umeme na vitu vingine vingi. Asbestos ilipendwa sana kutumika kwa sababu ni ngumu, haiozi au kupata kutu ikilowa pia haishiki moto. Hadi sasa asbestos iliyotumika miaka mingi iliyipita bado ipo katika mazingira yetu. Asbestos inapatikana katika majengo mengi ya zamani ya serikali kama vile ya shule na na hospitali na ya watu binafsi. Wananchi wameendelea kutumia mabaki ya bati za asbestos katika kuweka uzio na kujengea mabanda ya mifugo. Pia kuna mabomba yaliyotengenezwa kwa asbestos yamezikwa ardhini. Haya yalitumika katika mifumo ya maji safi na maji taka ambayo kwa sasa imekufa na haitumiki tena.

View attachment 1872905
Mabomba ya asbestos yaliyofukuliwa katika eneo la ujenzi wa barabara za mwendokasi awamu ya pili Dar es Salaam.

Asbestos imetumika sana katika kuezeka nyumba Tanzania. Katika report ya Makazi na Hali ya Jamii Kiuchumi Tanzania Bara (Basic Demographic and Socio-Economic Profile Report Tanzania Mainland) ya mwaka 2014 inaonesha kwamba asbestos ipo kwa asilimia 0.3% katika uezekaji wa majengo Tanzania bara ukilinganisha na mabati, zege na vigae6. Watu huvuna maji ya matumizi ya nyumbani katika maezeko haya ya asbestos. Hii ni kutokana kukosekana kwa elimu ya madhara ya asbestos katika jamii.

View attachment 1872909
Nyumba ambayo imeezekwa kwa asbestos
Chanzo: British lung cancer foundation

Kwa sasa haijalishi upo sehemu gani, kwa sababu katika mazingira yetu kuna vitu vingi au mabaki ya vitu ambavyo vimetengenezwa kwa asbestos. Hivyo mabaki ya asbestos yapo kwa kiasi kikubwa katika udongo. Pia watanzania wengi hawana uelewa kuhusu madhara ya asbestos hivyo wamekuwa wakikaa nazo katika mazingira yao bila kujua madhara yake. Watu wengi wamekuwa wakitumia vitu vyenye asbestos bila kujua hivyo kutochukua tahadhari yoyote.

View attachment 1872912
Bati za asbestos zilizoaribika zikiwa zimetupwa hovyo eneo la Mbagala

KWA NAMNA GANI ASBESTOS INAWEZA KUONDOLEWA KATIKA MAZINGIRA?
Katika nchi nyingi zilizoendelea kuna makampuni kadhaa yanayofanya kazi ya kuondoa asbestos katika mazingira. Kampuni hizo huwa na wataalamu na vifaa vya kugundua asbestos katika mazingira. Taasisi mbalimbali za kiserikali na binafsi huajiri kampuni hizi kuondoa asbestos katika mazingira yao.

JUHUDI ZA MATAIFA DUNIANI KUONDOA ASBESTOS KATIKA MAZINGIRA
Shirika la kazi duniani lilifanya mkutano wa makubaliano ya kimataifa mwaka 1986 ya kuthibiti uwepo wa asbestos katika mazingira. Nchi kadhaa kama vile Uganda na Zimbabwe ziliridhia makubaliano hayo lakini Tanzania ni mojawapo ya nchi ambazo hazijaridhia katika utekelezaji wa makubaliano hayo.
Kwa nchi nyingi kwa miaka kadhaa wamekuwa na kampuni mbalimbali ambazo hufanya kazi ya kuondoa asbestos katika mazingira lakini kwa Tanzania bado hatujaweza kufanya hivyo.

HITIMISHO
Katika nchi zinazoendelea kama Tanzania kumekuwa na maradhi mengi yatokanayo na taka hatarishi ambayo yanapunguza umri wa watu kuishi. Ni vyema serikali hasa kupitia vyombo vyake kama vile NEMC ikaongeza mikakati ya kuthibiti taka hatarishi hasa zilizosahaulika kama asbestos ili kulinda afya za watanzania. Wananchi wanatakiwa wapate elimu ya uelewa wa taka zote hatarishi ambazo zinapatikana katika mazingira yao na namna ya kujikinga nazo. Pia kuwe na mkakati wa kuondoa asbestos katika mazingira yetu. Juhudi hizi zikifanyika zitasaidia kulinda kizazi hiki na vijavyo.

REJEA
1. Jordan, P 1990. Mineral Industry Tanzania. Institute of Mineral Research of Zimbabwe. Report Number 119
2. United Republic of Tanzania, 2017, National Environment Statistics Report, Tanzania Mainland
3. United Republic of Tanzania, 2018, The National Solid Waste Management Strategy
4. Minnesota Department of Health. Environmental Health Division. Asbestos
https://www.health.state.mn.us/communities/environment/asbestos/homeowner/heffects.html
5. Boffetta P. 1998. Health effects of asbestos exposure in humans: a quantitative assessment. Med Lav.
6. United Republic of Tanzania, 2014, Basic Demographic and Socio-Economic Profile Report Tanzania Mainland.
Kuna mtu amekulipa kuandika yote haya? Au una maslahi gani na kukataza asbestos? Nahisi kama kuna mkono wa viwanda vya mabati hivi..sijui lakn
 
Kwani Kuna mabati ya asbestos yanauzwa siku izi?
Hii kwa ajili ya elimu tu
 
Back
Top Bottom