Asasi zaamka kulinda Maadili ya Viongozi wa Umma

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,130
44
Asasi zapinga kanuni batili katika Sheria ya Maadili
Mwandishi Wetu
Daily News; Friday,April 25, 2008 @17:03

Habari nyingine
Tabata Dampo waendesha zoezi kutambua wamiliki
Mkakati wa udhibiti wa mafua ya ndege keshokutwa
Watano kesi ya kuua Polisi waachiwa huru
Asasi zapinga kanuni batili katika Sheria ya Maadili
Ndege iliyokodishwa na ATC siyo mbovu – Waziri
Wizara yaeleza faida za ziara ya Bush
Mbunge ataka elimu ya wanawake wa miaka 40
Nafasi ya wabunge wilayani yafafanuliwa
Mbunge ataka barabara Mnazi Bay iwekwe lami
Shekifu: Uopoaji maiti Mererani utaendelea

ASASI tano zisizokuwa za kiserikali jana zilifungua kesi ya msingi kupinga kanuni batili katika sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002.

Kesi hiyo imefunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kupinga kanuni ya 6 (1) na (2) na kanuni ya 7 (2) (c) ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995.

Mashirika yaliyofungua kesi hiyo ni Mtandao wa Asasi zilizo Kusini mwa Afrika zinazojishughulisha na Masuala ya Haki za Binaadamu (SAHRINGON), Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Asasi inayojishughulisha na Haki za Wanawake (KIVULINI) na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria (Nola) na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA).

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Ananilea Nkya, mashirika hayo yanadai kuwa kanuni hizo Kanuni ya 6 (1) na (2) zenye vipengele vinavyoweka vipingamizi visivyo vya lazima vya kumzuia mwananchi kuwa na haki ya kupata taarifa zinazotolewa na viongozi wa umma kuhusiana na rasilimali, mapato au madeni yao.

Taarifa za mali za viongozi zinapaswa kupokelewa na Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma kama inavyoagizwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Ibara ya 132 kifungu kidogo cha 4 na cha (5) (b).

Vifungu hivyo vya Katiba pamoja na mambo mengine vinampa mwananchi haki ya kupata taarifa za mapato, rasilimali na madeni ya kiongozi, ilisema taarifa ya Nkya. Nkya alidai kuwa lakini cha kushangaza kanuni ya 7(2) (c) inazuia mtu aliyepata fursa ya kuona mali za kiongozi wa umma kuzitangaza hadharani hivyo zinapingana na Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye vipengele (a), (b), (c) na (d) ambavyo vinampa uhuru raia wa Tanzania haki kuhusu habari.

Vifungu hivyo vinavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 132 kifungu kidogo cha 4 na cha (5) (b) na pia kwenye Sheria hiyo ya Maadili Ibara ya 9, ibara ndogo ya (1) na Ibara ya 14, ambavyo vinatoa mwanya wa kufunguliwa kesi ya jinai kwa mtu au chombo chochote kitakachotoa taarifa kuhusiana na mapato, rasilimali na madeni ya viongozi wa umma.

Hivyo alisema mashirika hayo yamefungua kesi hiyo kuomba tafsiri ya Mahakama, kutamka kuwa kanuni 6 (1) (2) na kanuni 7 (2) (c) za Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 kuwa ni batili kwa kuwa inapingana na Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo ni sheria mama ya nchi.

“Kadhalika mashirika hayo yanaitaka Mahakama Kuu kutamka kuwa raia ye yote wa Jamhuri ya Muungano ana haki ya kupewa na kuchapisha taarifa kuhusiana na mapato, rasilimali na madeni ya viongozi wa umma bila vipingamizi mradi atatunza maadili na usalama wa Taifa,” ilisema taarifa hiyo.

Mashirika hayo pia yanaomba nguvu ya Mahakama kutoa nafuu zozote zinazowezekana kuhakikisha kuwa masilahi ya umma wa Tanzania yanazingatiwa kutokana na sheria hiyo.
 
Mkapa dawa yake ni kumuangua apate BUSHA, Kisha tumuamuru arudishe alichochukua
 
Asasi zapinga kanuni batili katika Sheria ya Maadili

ASASI tano zisizokuwa za kiserikali jana zilifungua kesi ya msingi kupinga kanuni batili katika sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002.

Viogozi wetu wanasatihili kufikishwa mahakamani na kupata adhabu stahili.

Viongozi wetu wanajua fika na wanauwezo wa kutofautisha kati ya Mwanadamu mwenye Utu na yule asiye na utu!

Viongozi wetu wanajua kinachomfanya mwanadamu mmoja kuwa na utu na kukosesha mmoja tuzo hilo kuwa ni maadili ya utu!

Hakuna mwanadamu aliyejiumba!

wote wameumbwa na kukabidhiwa UTU!

Kuusalitu utu na maadili yake ni kumsaliti aliye Kuumba!

Na wauliza viongozi wetu wanaofanya mchezo na Maadili ya Utu na Ubinaadamu wa Mtanzania, wana Pumzi ya Kutosha Kupambana na Muumba wao?

Kama wanaujuzi mkuu wajibadili wajirudishe kwa aliowaumba ili awategenezee maumbo mapya..wawe vijitumbili ambavyo ni vijinyama,kama kweli kabisa hawautaki utu na maadili yake na hasa inapofikia kwenye UONGOZI!

Kama wameukana utu na maadili yake Basi wakawe viongozi wa tumbili huko vichakani! sio sisi watu na utu wetu!

Kama unataka kuongoza na hasa watanzania! Basi anza kutukuza utu, hasa utu na maadili yake ya uongozi!

Narudia, Kuukana utu na maadili yake ya uongozi ni kumkana MUNGU! Aibu hiyo haitaepukika! Pigo kali la Mungu litawafuata popote!

Ushahidi?

Muulize Mkapa, ilikuwaje akaukana utu wake na wa familia yake na wa Taifa? Nini kinamfuata na nini kitamfika??

Muulize Chenge! Kuupuuzia utu wa watu wengine kwa viporojo vya vijisenti huku akijua fika kima cha chini cha mshahara na waalimu walikopwa mishara yao karibu miaka sasa?

Waulize wakuu wa Richmond kuwa mwaka ulipoanza walifikiria wangetema vyeo vyao kabla hata mwaka haujafikia kati?

Nisemehivi ...Mjanja kidogo na anyejikuta anahusika...Afanye kila kinachwezekana kabla hajaiishia pabaya..tena afanye hivyo maramoja bila kuchelewa! alifanyehilo leo..na ikiwezekana kabla ya kulala usiku huu!

Ahakikishe maadili ya uongozi yanatekelezwa katika kiwango sahihi bila kuchelewa!
 
Back
Top Bottom