Kikwete ampa John Cheyo milioni 120/-
Hivi kuna ndoa gani kati ya John Cheyo na serikali ya CCM?
Na Gladness Mboma
SERIKALI imetoa sh. milioni 126 kama mchango wake kwa ajili ya kuimarisha shughuli za Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD).
Mwenyekiti wa UDP, Bw. John Cheyo alisema hayo jana Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge, alipozungumzia mgogoro wa Kenya.
Bw. Cheyo alisema fedha hizo walikabidhiwa jana Ikulu, Dar es Salaam na Rais Jakaya Kikwete, ambazo zitasaidia kuimarisha kituo hicho kinachopigania demokrasia nchini.
Alisema kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakiiambia Serikali kuwekeza katika amani kwa kukutana na vyama vya Upinzani kuzungumzia amani na kuwekeza TCD.
Akizungumzia mgogoro wa Kenya, Bw. Cheyo alisema Watanzania wanapenda kuona watu hao wakikaa pamoja katika meza moja, ili kutatua migogoro yao.
"Nimewapongeza Wakenya kwa kuwaona wamekaa meza moja juzi na kuchagua Spika kwa utulivu na amani bila kuleta fujo na ninaamini mwendelezo huo utasaidia amani iliyokuwapo mwanzo kurejea upya," alisema Bw. Cheyo.
Aliwataka Wakenya wajaribu kutumia Bunge kutatua migogoro waliyonayo ili waweze kukaa pamoja kama ilivyokuwa mwanzo.
Source: Majira 17-01-2007