Asasi nne za kiraia zaishitaki Tanzania mahakama ya Afrika Mashariki kwa 'Ukiukwaji mkubwa' kutoka kwa polisi wake

cheap politics...
Wakimaliza makesi yao huku bongo hakuna hata atakayewasikiliza, bahati nzuri itakuwa 2022 huko Kenya watakuwa wameuana kwa mamia, unafiki wa vibaraka wa mabeberu utafunikwa na hilo.
 
Utemi Utemi tu - Kosoa Serikali kishabiki unakipata - kwanza hakuna kuogopa hivi vi mahakama uchwara - kwanza maamuzi ama hukumu yake yake ni kama mapendekezo tu kwa Serikali yetu sikuvu ya CCM

CCM oyeee - ushindi wa kishindo ndiyo nguzo yetu - Tunakubalika na watanzania - wengine wote mnajisumbua bure

Kutoka Lumumba ni mimi Mwamachama mkelelekwa aka mfia chama nisiye na cheo chochote
 
Uganda wakamshitaki Museveni na Kenya wamshitaki Kenyatta kwanza, kuanzia uchaguzi wa Kenya na sasa Uganda kisha wakiwashinda ndo waje huku kwetu.
Waganda na Wakenya wenyewe wataamua kuwashitaki Viongozi wao ikibidi siyo kwa ushauri wa vilaza wa CCM ambao hata lughà iliyotumika hawaelewi ingawa wanaweza kuwashitaki Viongozi wa hizo nchi wanachama ikibidi kwa kutumia Sheria huyohuyo. Vilaza ni vilaza tu hawawezi kufanya lolote kwa faida yao wala hawataki wengine wafanye!
 
Je, hizo Taasisi kutoka Jirani Kenya na Uganda zimeshamaliza Kwanza kutatua Matatizo makubwa ya Kiutawala ya huko nchini Kenya na Uganda?
Upo kwenye nyumba inayoungua unapiga yowe husikiki, inabidi jirani aingilie!!
IMG_20210104_164636_540.jpg
 
Asasi nne za kiraia zimeifikisha mahakamani Serikali ya Tanzania kwa ukiukwaji mkubwa kwenye uchaguzi mkuu wa karibuni ambao ulimrudisha madarakani Rais John Pombe Magufuli.

Taasisi kutoka Kenya na Uganda zinaishtaki Tanzania kwenye Mahakama ya Afrika Mashariki, zikituhumu vyombo vya usalama kutumia nguvu kupita kiasi, kupotea, kushikiliwa na hata kuuawa kwa wakereketwa wa upinzani wakati wa kampeni za uchaguzi na baada ya matokeo kutangazwa Oktoba.

"Serikali kupitia vyombo vya ulinzi na taasisi nyingine za serikali, vilijihusisha na kampeni ya ukiukwaji mkubwa wa sheria na kanuni muhimu za mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki" Taasisi hizo zilisema

Kesi katika mahakama ya EACJ zinaweza kuijaribu Tanzania kwenye uhusiano wake kikanda kwa mara nyingine ikizingatiwa sheria zake haziruhusu changamoto yoyote ya kisheria kuhoji matokeo ya Urais baada ya kutangazwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi.

Hoja ya taasisi hio zinatokana na Ibara ya 30(1) kutoa haki kushtaki kama 'watu' wanaoishi ndani nchi mwanachama wa EAC. Pia wanahoji, Tanzania kama nchi mwanachama analazimika kufuata mkataba kwenye utawala bora, haki, uwazi na kulinda haki za binadamu

==========

Four civil rights organisations are suing the Tanzanian government for “massive violations” in the recent general election in which President John Pombe Magufuli was voted back in office.

The organisations from Kenya and Uganda are suing Tanzania at the East African Court of Justice, alleging that security agents clobbered, disappeared, detained and even killed opposition supporters during the election campaigns as well as after the results were announced in October.

“The government, through its security services and other institutions of the state, engaged in a campaign of serious and massive violations of the rule of law and fundamental and operational principles of the East African Community Treaty,” the organisations said in suit papers.

The case at the EACJ could test Tanzania’s regional integration credentials once more, given its own domestic laws forbid any legal challenge on presidential elections, once the results have been declared by the National Electoral Commission.

The Kenya Human Rights Commission, the Kenya Section of the International Commission of Jurists (ICJ-K), and Uganda’s Chapter Four and the Centre for Constitutional Governance are suing Dar es Salaam for what they say is violations committed by a partner state of the East African Community (EAC).

They argue that the EAC Treaty’s Article 30(1) grants them rights to sue as “persons’ resident within a partner state of the EAC.” They also argue that as a member of the EAC, Tanzania was bound by the treaty’s provisions on good governance, social justice, transparency and protection of human rights.
Related

During elections last October, the four organisations say the state engaged targeted violence on ordinary citizens, journalists, activists, opposition supporters and politicians “and other individuals who held or were perceived to hold alternative political views.”

The elections saw Magufuli emerge the winner with 12.5 million votes, or 84.39 per cent of the vote, according to the National Electoral Commission of Tanzania. His closest opponent, Tundu Lissu, garnered 1.9 million votes. Thirteen others fell below 3 per cent. The ruling Chama Cha Mapinduzi also won 262 of the 264 seats in Parliament.

Yet the landslide victory was clouded with claims of irregularities. The Tanzanian Elections Watch a group of observers from the continent said the vote count “raised questions of credibility” and asked authorities to investigate. The NEC rejected claims of vote stuffing and the police denied any wrongdoing.

The four NGOs want the EACJ to affirm that the conduct of Tanzania security agents constitute violations against the treaty.

They also want the Court to order reparations, including damages, apology from the Tanzanian government, an independent investigation into the violations to prosecute the culprits and relevant reforms to prevent recurrence.

This will be the second major case the Tanzanian government will face under a Court created as part of the organs of the EAC. In 2014, conservationists led by the Africa Network for Animal Welfare won against Dar after the EACJ termed Tanzania’s plans to construct a major highway through the Serengeti National Park “unlawful.”

The NGO had argued that the Serengeti ecosystem, linked to Kenya’s Masai Mara, was crucial for the survival of animals and that a highway would disrupt what it called a transboundary resource.

SOURCE: The East African
This is material as long as the Tanzanian population and activists join the front.
 
Katiba yetu lazima ina shida kubwa, rais anaweza kushinda bila kupata majority ya zaidi ya 50% na hapo hapo ushindi wake hauwezi kupingwa mahakamani.

Ni bora mchakato wa mabadiliko ya katiba urudi au tuendelee na kudai haki kutokea kenya na uganda kama hii mada inavyoeleza.
Wote kwa pamoja tuamke kudai marekebesho ya katiba. Hii ndiyo dawa ya yote haya yanayotokea. Tusiwaachie watu wa nje kutupigania.
 
Civil societies hizo mara nyingi hizo ni njia za kujustify funds wanazopewa na mabeberu.

Hauwezi kufungua NGO halafu unapokea pesa Za watu usipeleke ripoti ya kazi zako.

Lazima utafute tu jambo la kukuonesha kuwa unafanya kazi na fedha za donors haziendi bure.
 
Tanzania ni nchi huru yenye kujiamria mambo yake pasipo kuingiliwa na nchi yoyote, pia sisi watanzania zaidi ya milioni 12 ndio tumemchagua atutumikie hivyo hao mawakala wa mabeberu watuache
 
Upo kwenye nyumba inayoungua unapiga yowe husikiki, inabidi jirani aingilie!!View attachment 1668773
Jirani wenye nani? Hawa akina Uhuru Kenyatta ambaye muda wowote ICC inaibua Kesi yake ya Mauwaji baada ya Ushahidi mpya Kupatikana pamoja na Yoweri Museveni ambaye sasa ameshavuka Kiwango cha mwisho cha Ukatili na Kuwanyanyasa Wapinzani wake huko Kwake nchini Uganda? Ukizifananisha Tanzania, Kenya na Uganda bado Tanzania ipo mahala pazuri kwa Amani, Ustawi na Maendeleo kuliko hawa wengine.
 
We ni janga sasa, hiko kichwa umebebea tu nywele.

Hamia kenya au uganda.

Wala hapa hakuihitaji mjadala.

Nakuhakikishia HAKUNA LOLOTE WANALOWEZA FANYA ZAIDI TU YA KUBWEKA.
Hata kama hamna kitakachotokea angalau wamepaza sauti kuliko kukaa kimya,
 
Uchaguzi umekwisha Bavicha chapeni kazi!
Uchaguzi huu hauwezi kwisha abadan kwa sababu watu wengi hawakuridhika nao. Usitegemee watu kamwe kunyamaza kuongelea uchaguzi huu. hili tayari limo kwenye historia forever na hakuna raba itakayoweza kulifuta. Hili mlijuwe na inabidi mlikubali kwa kuwa hakuna namna nyengine!
 
Mkuu Replica,

What are the four civil rights organizations as quoted from your thread?

Are the civil rights organizations challenging Tanzanian government representing the two states of Uganda and Kenya to meet the legal litigation as they termed it?

"....The organisations from Kenya and Uganda are suing Tanzania at the East African Court of Justice, alleging that security agents clobbered, disappeared, detained and even killed opposition supporters during the election campaigns as well as after the results were announced in October....."

Do you have substantial evidence with synthesis proof that the purported allegations were facilitated by Tanzanian government's law enforcement instruments?

Do the said civil rights organizations aware that Tanzania withdrew from being member of the EACJ on matters allegedly related to human rights abuses?

Were the Kenyan and Ugandan civil rights posing as human rights organizations directly affected by the purported allegations to test the EACJ capability to preside the case?

*Another losing game has been embarked on by the envious crooks vesting the human rights organization anticipating to expose their ahtred against the government of Tanzania is on the spring board reprisal that won't make it.
Umejipa jina kubwa kumbe hamnazo. Mahakama ya Africa na mahakama ya Africa mashariki wapi na wapi?
 
Back
Top Bottom