Asanteni wanaJF: Nimefanikiwa ku-move on na kujitoa kwenye mahusiano pasua moyo

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,200
3,609
Ilikuwa ni kazi ngumu ilinichukua takribani Miezi mitatu moyo wangu kukubaliana na matokeo sasa mpenzi wangu kanichoka haitaji kuendelea na mimi na ananifanyia kila aina visa vitavyonifanya niumie mwisho wa siku nione mahusiano magumu nikae pembeni mwenyewe.

Ila nawashukuru wanaJF walionipatia mbinu ya kukabiliana mambo yakifikia hatua hii mpka sasa yule manzi haamini kilichotokea hadi leo hakuamini kama nimekubaliana na matokeo na ninaendelea na maisha yangu
 
Jiweke bize, usikae peke yako maana utaruhusu mawazo na itafanya umkumbuke.

Mfano leo kama hauna kazi twaweza kwenda Taifa kumsupport Lissu akiaga mwili wa mkapa.
 
Asante Sana ila nilichojifunza uki break up na mpenzi wako ndo utajua sababu iliyomfanya mpenzi wako akupende na sababu hiyoo ikiondoka basi ndo mwisho wa safari


Hata ufanyeje
Kweli kabisa...mapenzi yakiisha yameshaisha.

Usikute na wewe kuna mtu ulimuumizaga makusudi enzi hiiiizoooo sasa leo ndo zamu yako😃😃ila sio mbaya ndo maisha.endeleakupiga kazi za ujenzi wa taifa
 
Yeah, sio kila mahusiano lazima yafikie ndoa. Mengine huwa ni kama tuisheni...
Unachosema ni sahihi kitu nilichojifunza mpenzi wako akikuchoka nothing you can do kuyarudisha mapenzi Kama ilivyokuwa mwanzo

Kuna wakati unaweza kumpa chochote akipendacho ili kumfurahisha lakini wapi ndo unazidi kuumia kwani matarajio yako afurahie uwepo wako lakini wapi

Bora ukae pembenu. Yaishe
 
Back
Top Bottom