Asanteni wanahabari kutuzimia maigizo ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,863
Hatua zilizochukuliwa na jukwaa la wahariri kumfungia mkuu wa mkoa wa Dar, yani kuamua kutoshirikiana naye. Kutoandika habari zake, kumetuliza nchi kiukweli.

Ni kitendo cha kizalendo, cha kuungwa mkono na kila mtanzania anayelipenda taifa lake na anayeitakia nchi yake mema. Tulikuwa na wasi wasi tusijue hatima ya jiji letu.

Tulikuwa hatujui baada ya operesheni zilizofail za shisha, omba omba, dada poa, kulala guest mchana, madawa ya kulevya angekuja na lipi jipya.

Kumbe nguvu ya mamba iko kumayi? Kumbe nguvu yenu ni vyombo vya habari? tumewajua!

SASA HIVI JIJI LIMETULIA!
 
Hatua zilizochukuliwa na jukwaa la wahariri kumfungia mkuu wa mkoa wa Dar, yani kuamua kutoshirikiana naye. Kutoandika habari zake, kumetuliza nchi kiukweli.

Ni kitendo cha kizalendo, cha kuungwa mkono na kila mtanzania anayelipenda taifa lake na anayeitakia nchi yake mema. Tulikuwa na wasi wasi tusijue hatima ya jiji letu.

Tulikuwa hatujui baada ya operesheni zilizofail za shisha, omba omba, dada poa, kulala guest mchana, madawa ya kulevya angekuja na lipi jipya.

Kumbe nguvu ya mamba iko kumayi? Kumbe nguvu yenu ni vyombo vya habari? tumewa!

SASA HIVI JIJI LIMETULIA!
Sasa hivi anadandia jukwaa la Rais ndio pa kusemea.
 
Gwajima alisema akipiga mtu... Mtu huyo hupotea kabisa ktk ramani alizokuwepo. Naanza kuamini amini kwa askofu langu la ukweli...nae makamba alipotea jumla, hahaha
 
Imewapa fundisho Ma-RC wengi sana...Maana hata Gambo ametulia ghafla kama kapigwa nusu kaputi...
Mikoani ma RC si sana kutumia vyombo vya habari kama ilivyokuwa kwa huyu. Usingejua ni yeye ni zaidi ya PM, makamu wa rais au alijiona rais pacha!
 
Back
Top Bottom