Asanteni Wajumbe wa Kigamboni, Kamati yangu ya 'Wasiojulikana' ya Roho Mbaya CCM Dar es Salaam na Kamati Kuu ya CCM Dodoma 'Mtu' kachinjwa rasmi

Mkuu Gentamycine,

Mimi sitasema sana ila kwa kifupi kilichofanyika chaitwa "double knock effect" yaani mipango ilikwishasukwa kitambo.

Yaani zuia Kigamboni na ondoa ofisini..

Kibaya zaidi ni pale alipokamia kurudi kwa Tango Lima ndipo mazee yalipoomshauri mkulu awahishe utenguzi.

Lakini kweli kikulacho ki nguoni mwako.

Bwana Abuu Koinange ni mtu "smart" sana.

Mtu atumwa akukaimu halafu awe tyari kuchukua nafasi yako "in a friendly way".

Anyway kuna maisha baada ya uDC ila unavyomshauri aende kwa Yusufu si atalia sana akifika huko?
 
Tupo pamoja
Ef4urmdWoAA1GaZ.jpg
 
GENTAMYCINE,

Uwezi jua mwenzio unaweza sikia huyooooo dubai au Israel anawakilisha nchi. Teuzi zipo nyingi tu. Let's wait

Mwisho wake huyo 'Mpuuzi' wenu 'mnayemtetea' hapa ndiyo umeshafika na ninakuibia sasa za ndani kuna 'Ulaji' kafanya akiwa RC atashtakiwa tu.
 
Boss GENTAMYCINE Umesahau ... Rais ana nafasi 10 za upendeleo ??? !!!
Ila Bashite ... Kavuna alichopanda ... Na iwe fundisho kwake na Viongozi wengine wa aina yake


Yaani GENTAMYCINE na Jopo langu la Watu wenye Roho Mbaya za Ukweli na wanaojua 'Ndumba' na 'Fitina' za kila namna 'tusiojulikana' ndani ya CCM tukuamulie Wewe 'Mpuuzi' Mmoja halafu upite kwa Kutushinda? Kama ni Kamati yangu hii hii iliweza Kufanya 'Kafara' Kubwa Segerea Siku Moja kabla ya Mechi ya Simba na Yanga na Yanga 'Kula' Goli zile Nne (4) Wewe ungetuweza wapi Sisi Mafia hasa?

Kama kuna Mtu ambaye alikuwa akininyima Usingizi na aliyefanya nihangaike katika 'Kummaliza' kwa kila namna ili tu 'asigombee' na wala 'asipitishwe' Jimbo la Kigamboni ni Wewe 'Mpuuzi' fulani. Nashukuru sana Kelele zetu Kamati ya Roho Mbaya ( isiyojulikana ) ndani ya CCM 'imemaliza' Kazi yake na 'Mpuuzi' pamoja na 'Kumsumbua' sana Mama Namba Mbili 'Kikatiba' lakini bado ametoswa

Nilikuonya na hukutaka Kunisikia pale nilipokuambia mapema tu kuwa hutabaki kuwa hivyo ulivyokuwa Milele na kwamba ipo Siku tu 'Upepo' utakugeuka na utakuwa Mtu wa Kawaida tu nchi hii na 'Kupotezwa' mazima Kisiasa na Kiumaarufu ukadhani GENTAMYCINE nilikuwa natania na sasa yamekuwa. Na ulichokisahau tu ni kwamba hata huyo 'Babaako' nae alishakuchoka Kitambo

Kuna Watu (Members) wa hapa hapa nakumbuka nilipoanza tu 'Mashambulizi' yangu nawe kuwa hutofanikiwa na wala hutopitshwa na 'Babaako' huko Dodoma iwe isiwe 'Wakanitukana' na 'Kunidhihaki' sana tu wakiongozwa na huyu YEHODAYA na wengineo kadhaa. Hatimaye Rais wa Kamati ya Roho Mbaya 'isiyojulikana' ndani ya CCM GENTAMYCINE nimekuwa Mshindi.

Ushauri wangu Kwako tu ni kwamba Wewe 'Mpuuzi' kuanzia sasa anza Kujiandaa 'Kisaokolojia' kwani Maisha yako yataenda kuwa mabaya na magumu mno hapa Mjini kama si nchini pia. Nakuomba Watafute wale wote uliowakosea wakiongozwa na Jaji Mstaafu Mzee Warioba kisha uende kwa Yusuph Manji na Yule Mzee wa Ofisi ya Kinondoni ambaye ulimtukana na kumnyanyasa.

Kwa wale ambao mtapenda Kuungana nami katika Sherehe hii ya 'Mpuuzi Kutoshwa Rasmi' msikae mbali nawapeni Ratiba ya eneo la Sherehe yetu.
 
Mwisho wake huyo 'Mpuuzi' wenu 'mnayemtetea' hapa ndiyo umeshafika na ninakuibia sasa za ndani kuna 'Ulaji' kafanya akiwa RC atashtakiwa tu.
Mi sio namtete hapana nasema tu. Uwezekano huo bado upo. Na kuna nchi nyingi tu hatuna balozi huenda akapata hiyo fursa.
Binafsi nilikuwa namwelewa kipindi akiwa mkuu wa wilaya. nilianza kumwona hafai alipokuwa anawaweka wenye viti Wa mitaa kwenye mikutano wananza kusutana na wajumbe
 
Mkuu Genta,

Mimi sitasema sana ila kwa kifupi kilichofanyika chaitwa "double knock effect" yaani mipango ilikwishasukwa kitambo.

Yaani zuia Kigamboni na ondoa ofisini..

Kibaya zaidi ni pale alipokamia kurudi kwa Tango Lima ndipo mazee yalipoomshauri mkulu awahishe utenguzi.

Lakini kweli kikulacho ki nguoni mwako.

Bwana Abuu Koinange ni mtu "smart" sana.

Mtu atumwa akukaimu halafu awe tyari kuchukua nafasi yako "in a friendly way".

Anyway kuna maisha baada ya uDC ila unavyomshauri aende kwa Yusufu si atalia sana akifika huko?
Mkuu hilo jina #genta.
Huyu mkurya halitaki kabsa. Anapenda ukisema GENTAMYCINE
 
Kila lenye mwanzo pia lina mwisho.
Maisha ya siasa yana mwisho, lakini mwisho wa huyu jamaa siyo mzuri, maana aliendesha shughuli zake kibabe na ujivuni mwingi.

Wanasiasa wengine wenye kiburi kama yeye wajifunze
 
Kuna Watu ( Members ) hapa JF niliposema kuwa huyu 'Mpuuzi' muda wowote kuna 'Mashtaka' atayajibu na 'atafilisiwa' mazima tu hawakunielewa.
Kama alikuwa anajikusanyia kipato kwa njia isiyo halali na wakati huohuo Number moja hataki vipato vya dhuluma itakuwa ni Jambo jema kwa Makonda kushughulikiwa ipasavyo
 
Back
Top Bottom