Asanteni sana Wabunge vijana; kwa misimamo hiyo Tanzania ya neema yaja

Syzygus

JF-Expert Member
Sep 20, 2014
267
0
Ndugu zangu, niko huku vijijini Morogoro Kusini, Wilaya za Kilombero na Ulanga.

Nimeshangazwa sana na mwamko wa vijijini leo ambapo watu wengi walikuwa wakifuatilia hoja na michango ya Wabunge waliokuwa wakijadili sakata la Escrow Account ya Tanesco/Iptl.

Wapo walikuwa wakifuatilia kupitia Tv kwenye mabaa, lakini wengi walikuwa wakifuatilia Redio Ulanga ya Halmashauri ya W-Ulanga; asanteni sana redio Ulanga.

Binafsi nimefuatilia kupitia redio ingawa nilikuwa safarini muda wote.

Nimefuatilia michango takriban yote; hata hivyo nimefurahishwa sana na michango na taarifa za Wabunge Vijana kutoka Vyama vyote-CCM, NCCR, CDM.

Wabunge vijana waliosuuza moyo wangu na kunifanya kuonea shauku sana Tanzania ijayo ni Deo Haule Vilikunjombe, Hamis Andrea Kigwangalah, Luhaga Mpina [wote CCM], Zitto Zuberi Kabwe, na David Kafulila. Michango yao, hoja zao, na Taarifa waluzokuwa wakitoa kwenye mjadala huo zimenifanya nianze kuona Tanzania yenye neema siku za usoni kama watapata nafasu ya kushika madaraka makubwa miaka ijayo.

Wameweka siasa za vyama vyao kando na kuzungumzia masuala tofauti na Wabunge wenzao ambao sina sababu ya kuwataja.

Asanteni sana Wabunge vijana; najua mtatukanwa sana, mtasimangwa sana na wahafidhina wa vyama vyenu, lakini kwa wananchi tuliowasikiliza mmeonyesha uzalendo, uchungu na moyo mkuu kwa ajili ya Taifa hili.

Namani kuishi ktk nyakati ambao mtakuwa kwenye madaraka makubwa ya kiutendaji ktk nchi yetu.

Watanzania, nawasihi tuwarudishe bungeni vijana hawa 2015.

Asanteni sana Wabunge vijana, natamani 2015 waongezeke vijana zaidi wa aina yenu. Mungu awatangulie ktk safari yenu ya kisiasa.
 

maswitule

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
1,392
1,500
Uko sahihi na amini wabunge wazee kama mbunge wangu wa kule usukumani hawaelewi nini maana ya pesa ya uma na nini kinaendelea, hakika ukweli vijana ndio huujua kabla ya wazee na unapotaka kujua kesho itakuweje waulize vijana na si mzee kama mbunge wangu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom