Asanteni Madaktari; mmetuonesha hatupaswi kutaliwa kwa ubabe tena!

Hapana siyo kuheshimu madaraka ya mkuu wa nchi kwani hakuna mahali popote ambapo Ikulu iliwataka madaktari kurudi kazini mara moja bali mahakama ndiyo imefanya hivyo?
Mkuu mbona unapindisha ukweli?
Hivi kuna ugumu gani kuelewa Drs wamekubali baada ya kukutana na JK, au unataka kutuaminisha kwamba hata wasingeonana na JK wangesitisha mgomo kwasababu ya mahakama ya kazi
 
Naam!

Nimesoma na kurudia mara kadhaa taarifa ya chama cha madaktari kuhusu kusitisha mgomo na niseme kwamba nimeipenda upeo na heshima yangu kwa madaktari wetu imezidi mara elfu zaidi. Yeyote aliyesoma taarifa hiyo anaweza kuiona kuwa ni taarifa ya kutokusalimu amri (non-surrender) bali ni kauli ya kamikaze kukataa kuchukuliwa mateka. Uamuzi wa madaktari kusitisha mgomo kufuatia agizo la mahakama kuu kuwataka warudi kazini ni uamuzi ambao unahitaji kukubaliwa na kupongezwa na wale wote ambao walisimama na madaktari toka mwanzo wa mgomo huu. Binafsi na kutoka moyoni kabisa nasema madaktari wetu asanteni na heshima yangu kwenu imeinuliwa juu zaidi sasa kuliko wakati wowote ule mwingine!

Kukataa kutawaliwa kibabe
Mgogoro huu ulianza kwa sababu kuna watu waliamini kuwa wanaweza kutawala wenzao kibabe bila kujali matokeo ya kutawala huko kwao. Mmetuonesha kuwa mtu kuwa Waziri au Katibu Mkuu kiongozi siyo kibali cha kufanya lolote, kwa yeyote na popote bila kuulizwa. Mmetuonesha kuwa ni jukumu la wananchi kuwahoji viongozi wao na wasiporidhishwa nao kuwapinga. Mmefanya kitu kipya katika Tanzania kufanywa na watu wasio wanasiasa - kukataa kuburuzwa na viongozi wa kisiasa! Mmeonesha kukataa ubabe wa utawala uliolewa madaraka. Kwa hili, mtakuwa mmewapa moyo watu wengine vile vile kutokubali kunyanyaswa, kupuuzwa, kudhehekiwa na kuburuzwa na wanasiasa! Salute!

Mmeonesha mabadiliko yana gharama - wakati mwingine kubwa sana
Mojawapo ya matokeo ya huu mgomo ni gharama yake. Kwa kweli hakuna mtu yeyote aliyejua kuwa mgomo wa madaktari unayekuja ambaye hakujua au kukadiria uwezekano wa matokeo yake hasa katika maisha ya wagonjwa na hisia za wananchi. Madaktari wanapoachwa kugoma - iwe kwa saa moja, siku moja, wiki moja au kwa mwezi mmoja kuna gharama. Na wanapofikia madaktari kugoma kwa zaidi ya siku moja ni ishara tu kuwa wanasiasa wameshindwa kutatua matatizo yao; wanapogomwa kwa zaidi ya wiki moja manake ni kushindwa kabisa na kuporomoka kwa uongozi wa kisiasa!

Madaktari hawatakiwa kuachwa kugoma; Pale tu tishio la mgomo lilipotolewa ilitakiwa uongozi wote wa taifa letu kulipa jambo hili uzito mkubwa sana kuliko ilivyofanywa mwanzoni. Wengi tunakumbuka kuwa mgomo huu ulipoanza kikao cha Bunge kilikuwa nacho kinaanza Dodoma na tunakumbuka jinsi bunge lilivyosuasua hata kujadili hili huku wakililia posho zao! Rais alitolea kauli suala la posho lakini hakutolewa kauli suala la mgomo wa madaktari! Rais alitoa pouwa kwa wafiwa mbalimbali lakini siyo wale walioathirika na mgomo! Mwezi mmoja baadaye ndiyo Rais ametolea taarifa tena vuguvugu.

Matatizo yote yaliyowakuta wananchi na hasa wagonjwa - ikiwemo vifo - yametokana na jambo moja tu! Siyo madaktari kugoma - bali madaktari kuachwa wagome kwa masaa, siku na wiki! Hivi kweli tumeacha madaktari wagome na tulitarajia wagonjwa wapone?

Kuogopa kushinikizwa na wananchi kumeligharimu taifa
Tatizo kubwa ambalo nimelionesha huko nyuma ni hofu ya kijinga kuwa viongozi wakiondolewa kwa mashinikizo basi wengine nao wataondolewa kwa mashinikizo. Tujiulize kama wananchi hawawezi na hawapaswi kuishinikiza serikali yao nani anapaswa kufanya hivyo? Kama wananchi hawawezi kuwakataa viongozi wabovu nani awakatae? Kama wananchi hawawezi kushinikiza mamlaka zilizo juu yao kuwasikiliza nani aje kufanya hivyo? Wawekezaji? Mabalozi? Nchi za Kimagharibi?

Wananchi wanayo haki ya msingi (inherent right) ya kuishinikiza serikali yao na viongozi wao; viongozi hili waliogope lakini wasiinyang'anye haki hii. Madaktari walitumia mbinu mbalimbali za kutatua tatizo hili wakapuuzwa na wakaamua kuweka shinikizo la mgomo; serikali ilitakiwa iitikie mara moja badala ya Rais kuondoka na kuonekana kutokujali kabisa kinachotokea nchini.

Waziri Mkuu amebebeshwa mzigo asiouweza
Kati ya vitu vya ajabu sana ni kuwa watu walitarajia PInda atatue tatizo la mawaziri. Wengi inaonekana hawajui kuwa mawaziri hawateulizi na Waziri Mkuu na Waziri Mkuu wa Tanzania hawawezi kumfukuza Waziri yeyote kwani siyo anayeunda baraza la mawaziri. Waziri Mkuu hana uwezo wa kumuwajibisha Mponda au Nkya! Kikatiba Waziri Mkuu wetu ni dhaifu sana mbele ya Rais kwani yeye naye anafanya kazi kwa ridhaa ya Rais. Japo anapitishwa na Bunge, Bunge haliwezi kumzuia rais kumuondoa!

Kwa vile mgogoro ulihusu mawaziri ni Rais peke yake - aliyewateua na ambaye wanatumika kwa ridhaa yake - alipaswa kuingilia kati siyo Waziri Mkuu. Waziri Mkuu alikuwa na uwezo tu wa kufikisha ujumbe wa Rais lakini hakuwa na bado hana uwezo wa kufanya lolote kwa waziri yeyote nchini. Inaonekana watu wengi wamesahau sakata la Richmond. Waziri wa NIshati na Madini wa wakati ule walilalamikiwa kuhusiana na mkataba wa Richmond; Waziri Mkuu aliingilia kati lakini hakuwa na uwezo wa kumzuia Waziri yeyote kufanya lolote kwa sababu hana uwezo huo. Waziri Mkuu alifanya yale yaliyondani ya uwezo wake lakini kuwawajibisha mawaziri si mojawapo hili alimuachia Rais.

Ndio maana naamini kuwa Pinda inampasa kujiuzulu kumsaidia Rais kuunda baraza jingine. Kama Waziri Mkuu wakati wa kashfaa ya Richmond alivyojiuzulu na kumpa nafasi rais kuunda baraza jingine ninaamini PInda baada ya kuoneshwa kuwa ni dhaifu mara tatu kwenye sakata hili amepoteza credibility ya kuonesha uongozi. Njia pekee - akitaka kuwa na heshima - ni kujiuzulu ili kumpa Rais nafasi ya kujipanga upya. Kwa vile Rais anasuasua katika kufanyia mabadiliko baraza Waziri Mkuu akijiuzulu baraza nalo linavunjika - japo hakuliunda yeye!

Madaktari wamerudi nyuma bila kusalimu amri (retreat withour surrendering)
Walichosema madaktari ni muhimu sana kwa Rais na viongozi wetu wa kisiasa kukifikiria. Je wanaweza kumlazimisha Daktari kurudi kazini bila kuhatarisha maisha ya wagonjwa? Je daktari kurudi kazini katika mazingira yale yale yaliyosababisha mgomo inamsaidia nani hasa? Je daktari kuonekana hospitalini anapima pima na kutembea temba au kuzungumza na wagonjwa hata kama hana dawa, vifaa n.k inasaidia nini? Kama kweli leo kuna hospitali ambazo X rays hazifanyi kazi na zipo zisizo na CT Scans kweli daktari anaporudi hapo tunaweza kusema amerudi kufanya kazi au kuonekana kazini?

Msimamo wao juu ya Nkya na Mponda unatuma ujumbe mzito

Hata hivyo madaktari wametuma ujumbe mzito sana kwa wote wale ambao wanafikiria kuwa wameumaliza mgomo - kwamba mawaziri hao ni tatizo kwa sekta ya afya. Madaktari wanasema hivyo kwani wamewaona wakifanya nao kazi kwa mwaka uliopita, wamezungumza nao mara nyingi na wanawajua uwezo wao. Madaktari wanasema hawa ni tatizo - ni jukumu la rais kuendelea nao au kutokujali maneno ya wataalamu hawa. Kuendelea kuwa nao kwa sababu ya kuogopa shinikizo ni kuhatarisha zaidi sekta ya afya kuliko kuwaondoa.

"Wakati madai yetu yakishughulikiwa (na Rais) tunapenda kusema kuwa hatuna imani na Waziri wa Afya Mhe. Dr. Haji Mponda na (naibu) Mhe. Lucy Nkya na kuwa tunamsimamisha rasmi uanachama wa MAT Mhe. Dr. Lucy Nkya" wamesema madaktari katika tamko lao na kuongeza "madaktari tunatamka kuwa Waziri wa Afya Dr. Haji Mponda na Naibu wake Dr. Lucy Nkya ni maadui wa madaktari na wa sekta ya afya kwa ujumla hapa nchini na tunaahidi kutowapa ushirikiano wowote wa kibinafsi au wakiutendaji". Kama ujumbe huu wa mwisho haujafungua masikio ya watawala wetu basi hakuna ujumbe mwingine unaoweza kufunguliwa.

Asanteni madaktari
Madaktari asanteni kwa kuliamsha taifa na kutukumbusha kuwa kuna gharama katika kuleta mabadiliko. Gharama ya majina, hadhi, na sifa zetu; kuna gharama ya nafsi zetu na kwa kweli kabisa kuna gharama kwa watu wengine vile vile. Mmetuonesha kile tulichokiona sehemu nyingine duniani - mabadiliko yana gharama kubwa - kuna watu watapoteza kazi, wapo watakaochukizwa na wapo wengine watapoteza hata maisha yao. Niliandika wiki iliyopita kuhusu Steve Biko na kuonesha kuwa alilipia gharama kubwa ya uhai wake kwa kuwaamsha vijana wa Afrika ya Kusini! Mmefanikiwa katika kilichoshindikana - kuiambia serikali haiwezi kutawala kwa mabavu na dharau!

Ni matumaini yangu watawala wetu wamejifunza jambo kidogo katika hili - wawe na haraka ya kutatua matatizo badala ya kutafuta namna ya kulindana na kubebana na kutetea vitumbua vyao. Kwa sababi, kama madaktari wameitikisa kidogo serikali hivi, itakuwaje endapo mgomo mkubwa zaidi utakuja kufanyika? Kuna mistari imechorwa na sasa imeanza kuvukwa. Wasiwalazimishe na wengine kuvuka kwani wasipoangalia nchi kweli kabisa itaishi kutoka mgomo na kashfa hadi mgomo na kashfa nyingine na hivyo kuzidi kujidhoofisha.

Walioathirika wapewe pole kweli
Wapo walioathirika sana na mgomo huu na kwa kweli kila Mtanzania kwa namna moja au nyingine ameathirika. Wapo ambao tumesupport mgomo huu tukijua kabisa kuwa ndugu zetu wanatakiwa kwenda hospitali huko huko na wengine wamepoteza jamaa zao wakati wa mgomo huu. Kama nilivyosema mwanzoni madaktari hawakutakiwa waachwe wagome, na kwa vile ni wanasiasa ndio waliowaacha madaktari wagome ni wao wanasiasa wanabeba lawama zote za madhara ya mgomo huu kwani kama wameweza kuuzimisha kwa kikao cha masaa machache Ikulu wangeweza kufanya hivyo Januari! Hawakufanya na matokeo yake ni haya yaliyotokea.

Kikwete akubali kuwajibika kwa yote yaliyotokea
Kama nilivyosema juzi, namna pekee ya kuanza kwa usahihini kwa Rais kukubali kubeba lawama za mgomo huu wote kuanzia mwanzo hadi hivi sasa. Kama Rais alipaswa kuingilia kati mara moja na ugoigoi wa kufanya hivyo ndio umefikisha hapa tulipofika. Hawezi kukwepa lawama na hana mwingine anaweza kushare naye lawama hizo. Na tunarajia kuwa atawawajibisha hawa viongozi na wakati huo huo kupanga mkakati wa nguvu wa kuboresha sekta ya afya.

Kwa kukubali kusitisha mgomo baadaya kukutana na Rais madaktari wametuonesha nani anastahili kuwajibika. Natumaini naye amejitambua hivyo.

MMM-BGM

Hongera mkuu kwa uchambuzi wako yakinifu
Wananchi wengi hawaelewi nini kilikuwa kikifanyika.....
na inasikitisha kuwa wananchi wengi bado wamelala sana sijui lini wataamka !!!!!1
Yaani this time nimeipata picha halisi ya watz wanasahau mapema sana....
And thats why CCM has managed to be on power for this long despite of their countless MADUDU .....
Leo Mwananchi wa Dodoma anaambiwa ataletewa meli akimchagua Mh. wakati Dodoma hakuna hata mto wa kupita Mtumbwi
Wa Dar wanaambiwa watajengewa barabara za angani .......hardly mwaka umepita lakini saivi
aahhh wananchi hawa wamesahau kabisa.....na watawala wako very comfortable......
 
Umesoma lakini hujaelewa umelewa ushabiki usio na maana..

Rudi tena kwenye drawing boards, unachotetea ni mauaji kwa vile tu padre mwenzako hajawa rais period..

Is like saying liwalo na liwe..pathetic..

At the end mdrs wamerudi kazini wananchi wanahudumiwa bravo JK

Endelea na hila zako utakonda bure ..kajipange 2015 padre wako atalia mara mbili..
 
Wewe ni muislam mjinga kabisa! Huo ni ukweli
 
Umesoma lakini hujaelewa umelewa ushabiki usio na maana..

Rudi tena kwenye drawing boards, unachotetea ni mauaji kwa vile tu padre mwenzako hajawa rais period..

Is like saying liwalo na liwe..pathetic..

At the end mdrs wamerudi kazini wananchi wanahudumiwa bravo JK

Endelea na hila zako utakonda bure ..kajipange 2015 padre wako atalia mara mbili..

Tumia akili kufikiri...kwaheri!!
 
Pole!Historia itakuhukumu..na dhamira yako itakusuta..unajifanya una huruma kumbe unafiki mkubwa....Eti hata Yesu....

Unajisemea mwenyewe..mimi natwanga ukweli tu..yesu hakuambiwa na wayahudi mjinga? uwongo uko wapi..

nshasema huna hoja utaishia kutukana tu..kwaheri
 
Nooooooooooooooo!!

Nimewapata vizuri tu; just making sure... manake hatuhukumu kwa vilivyosemwa sirini bali vilivyosemwa hadharani. Amri ya mahakama kuu kitengo cha kazi imetekelezwa. Hakuna mahali popote hadharani madaktari waliikataa amri ya mahakama kuwa si halali na hakuna mahali ambapo Ikulu iliwaagiza au kuwaomba madaktari kurudi kazini. SIKANUSHI kuwa haikuzungumzwa vilivyozungumzwa sirini.
 
Unajisemea mwenyewe..mimi natwanga ukweli tu..yesu hakuambiwa na wayahudi mjinga? uwongo uko wapi..

nshasema huna hoja utaishia kutukana tu..kwaheri

sasa na wewe unajifananisha na Yesu?kufuru gani hii?? wa kusema ukweli uwe wewe?au ubinafsi unakusumbua?may be upo kazini..hivo sio kosa lako ni tumbo...
 
Yes nasema ukweli kama Yesu..any problem with that?

Naamini na wewe uko kazini au siyo? huna hoja kwaheriiii.
 
Nimewapata vizuri tu; just making sure... manake hatuhukumu kwa vilivyosemwa sirini bali vilivyosemwa hadharani. Amri ya mahakama kuu kitengo cha kazi imetekelezwa. Hakuna mahali popote hadharani madaktari waliikataa amri ya mahakama kuwa si halali na hakuna mahali ambapo Ikulu iliwaagiza au kuwaomba madaktari kurudi kazini. SIKANUSHI kuwa haikuzungumzwa vilivyozungumzwa sirini.

Hii inaitwa spinning for the sake of spinning..lol

Wameongea na JK na wamerudi kazini hutaki kukubali uwezo wa JK ni uchoyo wako..

Just 2015 padre mwenzako apigwe chini tena
 
naona hata waliokuwa na msimamo hasi wamelegea. Kumbuka rais, pinda ndo aliyesema atamshauri aafu pia kuna kamati ya majadiliano ilikubali hilo na kusaini makubaliano hivyo walipaswa kumfikishia jk. Hii inanikumbusha ishu zetu nyingi za kikazi zinavyoishia kwenye dust bins za masecretary wa ofisi za wakuu wa kazi afu tunapigwa kalenda na kukaa kimya. Lazima uwe firm ndipo madai yako yatasikilizwa. Ukiendelea kumkubalia sekretary hutafanikiwa kwani taarifa hazifiki zinakotakiwa. Kwenye hili sakata kila mtu alikuwa anajitahidi kumdanganya bosi wake akitegemea umoja wa madaktari utasambaratika na mwisho ishu iyeyuke. Pia sio mahakama ndo iliyosimamisha mgomo,hebu jiulize maswali haya: mahakama kuu iko chini ya pm,maana tangazo lilitoka ofisi ya pm? Mahakama inafanya kazi kupitia vyombo vya habari,maana wahusika hawana barua ya amri hiyo? Siku hizi mahakama zetu zinafanya kazi usiku,maana tangazo lilitolewa saa 6 usiku na tbc? Wanaposema mgomo si halali,kuna mgomo halali kisheria? Ukipata jibu utajua ni kujiaibisha kwa wanasheria wetu wanaokubali kutumiwa wakisubiri kuteuliwa kwenye tume baada ya kustaafu. WELL DONE DOCTORS!
 
Naungana na wote ,wanaowashukuru madaktari.

Pamoja na mahakama kutumia sheria ambayo kwangu naona imejitusi na kumchukulia Mwanasheria mkuu kama mtu aliyechoka mawazo na si mshahuri mzuri kwa serikali,kwa kutumia mahakama badala ya kuishahuri serikali kuwatendea haki watanzania.

Swala hili lingetazamwa kwa upande mwingine,mwanasheria mkuu angeishitaki serikali kwa kutowatendea haki watanzania.

Ndiyo maana inabidi tufikie hatua sasa ya kuviwajibisha vyombo na uwongozi wa serikali,ili kurudisha nidhamu kati ya watawala na watawaliwa.

Vinginevyo nguvu na ubabe ukiendelea kutumika,gharama yake itakuwa kubwa.mf;

Madaktari watarudi kazini,ni wangapi watafanya kazi wakiwa na high moral,nini matokeo yake huduma zitakuwapo lakini ubora utapungua,kwani kama wananchi ndicho tunacho hitaji?
 
Nimewapata vizuri tu; just making sure... manake hatuhukumu kwa vilivyosemwa sirini bali vilivyosemwa hadharani. Amri ya mahakama kuu kitengo cha kazi imetekelezwa. Hakuna mahali popote hadharani madaktari waliikataa amri ya mahakama kuwa si halali na hakuna mahali ambapo Ikulu iliwaagiza au kuwaomba madaktari kurudi kazini. SIKANUSHI kuwa haikuzungumzwa vilivyozungumzwa sirini.

mwanakijiji pamoja na kuheshimu maoni yako, nakuomba ufikirie mara mbili unaposema unajadili kile kilichowekwa hadharani na sio sirini maana kama ndivyo hakuna haja ya watu kufanya investigations ili kuchimbua mambo yaliyojificha ama kufanya critical analysis ya issue ambazo haziko waziwazi kwa lengo la kubaini what has been hidden behind the scene.
 
Umesoma lakini hujaelewa umelewa ushabiki usio na maana..

Rudi tena kwenye drawing boards, unachotetea ni mauaji kwa vile tu padre mwenzako hajawa rais period..

Is like saying liwalo na liwe..pathetic..

At the end mdrs wamerudi kazini wananchi wanahudumiwa bravo JK

Endelea na hila zako utakonda bure ..kajipange 2015 padre wako atalia mara mbili..
Hii ndiyo nini sasa?
 
Back
Top Bottom