Asanteni Madaktari; mmetuonesha hatupaswi kutaliwa kwa ubabe tena! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Asanteni Madaktari; mmetuonesha hatupaswi kutaliwa kwa ubabe tena!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Japhari Shabani (RIP), Mar 10, 2012.

 1. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #1
  Mar 10, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ukilitazama swala la sakata la mgomo wa madaktari juu juu unaweza kuwalaumu na kuwaita watu wasio na huruma na hawawatendei haki wagonjwa,wauaji,wasaliti,wamekiuka kiapo cha udaktari n.k. Kitu ambacho serikali JK na utawala kwa ujumla katika propaganda na porojo zao wanataka tuamini hivyo.

  Ukilitazama kwa ndani,wakualaumiwa na kubeba lawama zote ni Mh.Rais JK,serikali na chama Tawala CCM kwa sababu zifuatazo JK katika uteuzi wa mawaziri na nafasi mbalimbali katika serikali na taasisi mbali mbali hazingatii uwezo,uzoefu na sifa za mchaguliwa bali uswaiba na masilahi katika makundi ndani ya chama tawala.

  Hali ambayo inampa hali ngumu ya kutoa uamuzi wa kuwawajibisha wanapofanya ndivyo sivyo.Tatizo lingine kwa vile serikali na utawala hauna dhana ya kuwatumikia wananchi hivyo kauli nyini na ahadi wanazozitoa zinatoka katika ulimi na kubaki katika makaratasi bila kufanyiwa utekelezaji kwa maana ya kua za kisanii na porojo ili muda upite. Hakuna anaewajibika kwa kauli au ahadi serikali au JK inazozitoa kwa hali hii kutegemea ufanisi ni ndoto ya mwendawazimu.

  Mambo mengi yametokea(ufisadi,rushwa,uzembe n.k) katika serikali na viongozi katika serikali na taasisi za serikali hakuna anaejiuzulu au kuwajibishwa tume baada ya tume imekwisha.Hata huko katika CCM viongozi wanaopatikana huko ni kwa njia ya rushwa na ufisadi ambapo hao ndio viongozi baadae katika serikali.

  NENO KUJIUZULU KUWAJIBIKA KATIKA UTAWALA HUU HALIMO KATIKA MSAMIATI WAO.NJIA PEKEE YA KUWALAZIMISHA WAWAJIBIKE NI MIGOMO NA MANDAMANO HIVYO MGOMO WA MADAKTARI UMEONYESHA NJIA JINSI YA KUIBANA SERIKALI ITIMIZE AHADI ZAKE NA SIO POROJO.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 2. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,526
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  very very well said mkuu....salute you!!!there is no any better way to speak about the doctors saga than the way you have put it......Its very very unfortunate though kuwa watu hii thread wala hawaisomi sana......inasikitisha yaani....kuna watu humu wamekuwa vibaraka wa kutetea mabovu ya serikali tu......kila kitu cha msingi kikipigiwa kelele kinahusishwa na siasa...unajiuliza wanafaidikaje unakosa jibu yaani....this tells you one thing.....kwamba mabadiliko kwenye fikra za watanzania wengi bado yapo mbaali sana....maana kama unaona hata wasomi wanatetea ushenzi unaofanywa na serikali sasa inakuwaje kwa wale majority kule choka mbaya ground zero????....long way to go yaani...God bless TZ!!!
   
 3. TASLIMU

  TASLIMU Senior Member

  #3
  Mar 10, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umenena mkuu!!!
   
 4. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #4
  Mar 10, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kweli mkuu ni tatizo kwa nchi yetu kwa wasomi wengi ata marafiki zangu ambao nimesoma nao baada ya kurejea nyumbani ambao huku walikua na mtazamo tofauti na utawala huu wa CCM wakifika nyumbani wanabadilika utafikiri wame wamerogwa,ukiwauliza watakuambia wacha bwana hapa ili ufanye kazi kunanjia mbili kaa kimya au uinge mkono CCM.CCM inakua sharti namba moja kama ilivyokua wakati wa chama kimoja kwa kila mchakato wowote swali la kwanza kadi ya CCM.Hali imebadilika watu hawajabadilika.Matokeo yake CCM imekua mwamvuli na ngao ya kuficha uozo,uzembe,ufisadi n.k.Matokeo yake wataalam na wasomi wengi wenyesifa wananyimwa kazi kutokana na itikadi zao za kichama na kulinda masilahi ya wananchi,mawazo yao hayasikilizwi hata kama yanaukweli na manufaa kwa taifa.Utaratibu huu ndio unafanya viongozi wengi na wafanyakazi wengi wasio na vigezo vinavyofaa wanapata nafasi kwakua ni wanaCCM.Ikiwa fisadi,mkopa kodi,mzembe jiunge na CCM ni mwamvuli na ngao ya kukulinda,ndio maana CCM ni kimbilio la wafanyabiashara na mafisadi huo ndio ukweli .
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Mar 10, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kila mtu ana mtazamo wake na sii vibaya kupingana japokuwa inategemea na picha uloiweka kichwani. Binafsi yangu nachukia sana Magaidi na Ugaidi upo wa aina nyingi mojawapo ikiwa ni hii ya kuchukua watu MATEKA na kuwafanya hostage ili madai yako yafanikiwe.

  Na Dunia nzima tunachukia Ugaidi huu sii kwa sababu hawana madai ya hakim bali kutumia watu wasiokuwa na hatia kama ngao ya kufikisha ujumbe wako, iwe wale magaidi wa Kipalestina waliochukua wachezaji wa Israel ktk uwanja wa Olimpiki Ujarumani au Magaidi wapigania Uhuru wa Sandinista huko Nicaragua, hoja nyuma ya pazia hili ni kwa nini wanachukua wananchi wasiokuwa na hatia kabisa kuwa hostage kuhatarisha maisha na uhai wao kwa mgogoro usiowahusu ila baina ya serikali na wapambanaji..

  Binafsi yangu sina matatizo kabisa na madai ya madaktari maana ni haki yao na watanzania wote kwa ujumla. Utawala huu umekuwa dhalimu sana kiasi kwamba hawajali lolote kuhusiana na utawala bora, lakini majawabu hayawezi kupatikana kwa kuwachukua wananchi mateka na hata kuhatarisha maisha yao tukihesabu vifo baada ya vifo ili machungu haya yawaumize serikali na ikubali kushindwa.

  Ikumbukwe tu zipo serikali zinazosema hawawezi kusalimu amri kwa magaidi na kama haya yatakuwa maamuzi ya serikali ya JK pamoja na kwamba hatupendezewi sote, basi vifo vya raia waliokufa na wanaokufa bure na sii kwa kujitoa mhanga na vita hii vitawa hunt maisha yao yote...
   
 6. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu naona uanchanganya kuchukua mateka na kugoma! Hivi waalimu wanapogoma kufundisha wanamchukua nani mateka? Na je polisi wakigoma kuripoti wanakuwa wamemchukua nani mateka? Sasa daktari yeye akitaka kugoma ili asikilizwa afanyeje? akalale na maiti? Nadhani ungetafuta neno zuri kutetea hoja yako kuliko kudai kwamba mtu anachukuliwa mateka katika swala hili!
   
 7. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  madaktari ni watu wapole na wanaopenda kujitolea.tusiwafanye wajinga
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Mar 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  Naam!

  Nimesoma na kurudia mara kadhaa taarifa ya chama cha madaktari kuhusu kusitisha mgomo na niseme kwamba nimeipenda upeo na heshima yangu kwa madaktari wetu imezidi mara elfu zaidi. Yeyote aliyesoma taarifa hiyo anaweza kuiona kuwa ni taarifa ya kutokusalimu amri (non-surrender) bali ni kauli ya kamikaze kukataa kuchukuliwa mateka. Uamuzi wa madaktari kusitisha mgomo kufuatia agizo la mahakama kuu kuwataka warudi kazini ni uamuzi ambao unahitaji kukubaliwa na kupongezwa na wale wote ambao walisimama na madaktari toka mwanzo wa mgomo huu. Binafsi na kutoka moyoni kabisa nasema madaktari wetu asanteni na heshima yangu kwenu imeinuliwa juu zaidi sasa kuliko wakati wowote ule mwingine!

  Kukataa kutawaliwa kibabe
  Mgogoro huu ulianza kwa sababu kuna watu waliamini kuwa wanaweza kutawala wenzao kibabe bila kujali matokeo ya kutawala huko kwao. Mmetuonesha kuwa mtu kuwa Waziri au Katibu Mkuu kiongozi siyo kibali cha kufanya lolote, kwa yeyote na popote bila kuulizwa. Mmetuonesha kuwa ni jukumu la wananchi kuwahoji viongozi wao na wasiporidhishwa nao kuwapinga. Mmefanya kitu kipya katika Tanzania kufanywa na watu wasio wanasiasa - kukataa kuburuzwa na viongozi wa kisiasa! Mmeonesha kukataa ubabe wa utawala uliolewa madaraka. Kwa hili, mtakuwa mmewapa moyo watu wengine vile vile kutokubali kunyanyaswa, kupuuzwa, kudhehekiwa na kuburuzwa na wanasiasa! Salute!

  Mmeonesha mabadiliko yana gharama - wakati mwingine kubwa sana
  Mojawapo ya matokeo ya huu mgomo ni gharama yake. Kwa kweli hakuna mtu yeyote aliyejua kuwa mgomo wa madaktari unayekuja ambaye hakujua au kukadiria uwezekano wa matokeo yake hasa katika maisha ya wagonjwa na hisia za wananchi. Madaktari wanapoachwa kugoma - iwe kwa saa moja, siku moja, wiki moja au kwa mwezi mmoja kuna gharama. Na wanapofikia madaktari kugoma kwa zaidi ya siku moja ni ishara tu kuwa wanasiasa wameshindwa kutatua matatizo yao; wanapogomwa kwa zaidi ya wiki moja manake ni kushindwa kabisa na kuporomoka kwa uongozi wa kisiasa!

  Madaktari hawatakiwa kuachwa kugoma; Pale tu tishio la mgomo lilipotolewa ilitakiwa uongozi wote wa taifa letu kulipa jambo hili uzito mkubwa sana kuliko ilivyofanywa mwanzoni. Wengi tunakumbuka kuwa mgomo huu ulipoanza kikao cha Bunge kilikuwa nacho kinaanza Dodoma na tunakumbuka jinsi bunge lilivyosuasua hata kujadili hili huku wakililia posho zao! Rais alitolea kauli suala la posho lakini hakutolewa kauli suala la mgomo wa madaktari! Rais alitoa pouwa kwa wafiwa mbalimbali lakini siyo wale walioathirika na mgomo! Mwezi mmoja baadaye ndiyo Rais ametolea taarifa tena vuguvugu.

  Matatizo yote yaliyowakuta wananchi na hasa wagonjwa - ikiwemo vifo - yametokana na jambo moja tu! Siyo madaktari kugoma - bali madaktari kuachwa wagome kwa masaa, siku na wiki! Hivi kweli tumeacha madaktari wagome na tulitarajia wagonjwa wapone?

  Kuogopa kushinikizwa na wananchi kumeligharimu taifa
  Tatizo kubwa ambalo nimelionesha huko nyuma ni hofu ya kijinga kuwa viongozi wakiondolewa kwa mashinikizo basi wengine nao wataondolewa kwa mashinikizo. Tujiulize kama wananchi hawawezi na hawapaswi kuishinikiza serikali yao nani anapaswa kufanya hivyo? Kama wananchi hawawezi kuwakataa viongozi wabovu nani awakatae? Kama wananchi hawawezi kushinikiza mamlaka zilizo juu yao kuwasikiliza nani aje kufanya hivyo? Wawekezaji? Mabalozi? Nchi za Kimagharibi?

  Wananchi wanayo haki ya msingi (inherent right) ya kuishinikiza serikali yao na viongozi wao; viongozi hili waliogope lakini wasiinyang'anye haki hii. Madaktari walitumia mbinu mbalimbali za kutatua tatizo hili wakapuuzwa na wakaamua kuweka shinikizo la mgomo; serikali ilitakiwa iitikie mara moja badala ya Rais kuondoka na kuonekana kutokujali kabisa kinachotokea nchini.

  Waziri Mkuu amebebeshwa mzigo asiouweza
  Kati ya vitu vya ajabu sana ni kuwa watu walitarajia PInda atatue tatizo la mawaziri. Wengi inaonekana hawajui kuwa mawaziri hawateulizi na Waziri Mkuu na Waziri Mkuu wa Tanzania hawawezi kumfukuza Waziri yeyote kwani siyo anayeunda baraza la mawaziri. Waziri Mkuu hana uwezo wa kumuwajibisha Mponda au Nkya! Kikatiba Waziri Mkuu wetu ni dhaifu sana mbele ya Rais kwani yeye naye anafanya kazi kwa ridhaa ya Rais. Japo anapitishwa na Bunge, Bunge haliwezi kumzuia rais kumuondoa!

  Kwa vile mgogoro ulihusu mawaziri ni Rais peke yake - aliyewateua na ambaye wanatumika kwa ridhaa yake - alipaswa kuingilia kati siyo Waziri Mkuu. Waziri Mkuu alikuwa na uwezo tu wa kufikisha ujumbe wa Rais lakini hakuwa na bado hana uwezo wa kufanya lolote kwa waziri yeyote nchini. Inaonekana watu wengi wamesahau sakata la Richmond. Waziri wa NIshati na Madini wa wakati ule walilalamikiwa kuhusiana na mkataba wa Richmond; Waziri Mkuu aliingilia kati lakini hakuwa na uwezo wa kumzuia Waziri yeyote kufanya lolote kwa sababu hana uwezo huo. Waziri Mkuu alifanya yale yaliyondani ya uwezo wake lakini kuwawajibisha mawaziri si mojawapo hili alimuachia Rais.

  Ndio maana naamini kuwa Pinda inampasa kujiuzulu kumsaidia Rais kuunda baraza jingine. Kama Waziri Mkuu wakati wa kashfaa ya Richmond alivyojiuzulu na kumpa nafasi rais kuunda baraza jingine ninaamini PInda baada ya kuoneshwa kuwa ni dhaifu mara tatu kwenye sakata hili amepoteza credibility ya kuonesha uongozi. Njia pekee - akitaka kuwa na heshima - ni kujiuzulu ili kumpa Rais nafasi ya kujipanga upya. Kwa vile Rais anasuasua katika kufanyia mabadiliko baraza Waziri Mkuu akijiuzulu baraza nalo linavunjika - japo hakuliunda yeye!

  Madaktari wamerudi nyuma bila kusalimu amri (retreat withour surrendering)
  Walichosema madaktari ni muhimu sana kwa Rais na viongozi wetu wa kisiasa kukifikiria. Je wanaweza kumlazimisha Daktari kurudi kazini bila kuhatarisha maisha ya wagonjwa? Je daktari kurudi kazini katika mazingira yale yale yaliyosababisha mgomo inamsaidia nani hasa? Je daktari kuonekana hospitalini anapima pima na kutembea temba au kuzungumza na wagonjwa hata kama hana dawa, vifaa n.k inasaidia nini? Kama kweli leo kuna hospitali ambazo X rays hazifanyi kazi na zipo zisizo na CT Scans kweli daktari anaporudi hapo tunaweza kusema amerudi kufanya kazi au kuonekana kazini?

  Msimamo wao juu ya Nkya na Mponda unatuma ujumbe mzito

  Hata hivyo madaktari wametuma ujumbe mzito sana kwa wote wale ambao wanafikiria kuwa wameumaliza mgomo - kwamba mawaziri hao ni tatizo kwa sekta ya afya. Madaktari wanasema hivyo kwani wamewaona wakifanya nao kazi kwa mwaka uliopita, wamezungumza nao mara nyingi na wanawajua uwezo wao. Madaktari wanasema hawa ni tatizo - ni jukumu la rais kuendelea nao au kutokujali maneno ya wataalamu hawa. Kuendelea kuwa nao kwa sababu ya kuogopa shinikizo ni kuhatarisha zaidi sekta ya afya kuliko kuwaondoa.

  "Wakati madai yetu yakishughulikiwa (na Rais) tunapenda kusema kuwa hatuna imani na Waziri wa Afya Mhe. Dr. Haji Mponda na (naibu) Mhe. Lucy Nkya na kuwa tunamsimamisha rasmi uanachama wa MAT Mhe. Dr. Lucy Nkya" wamesema madaktari katika tamko lao na kuongeza "madaktari tunatamka kuwa Waziri wa Afya Dr. Haji Mponda na Naibu wake Dr. Lucy Nkya ni maadui wa madaktari na wa sekta ya afya kwa ujumla hapa nchini na tunaahidi kutowapa ushirikiano wowote wa kibinafsi au wakiutendaji". Kama ujumbe huu wa mwisho haujafungua masikio ya watawala wetu basi hakuna ujumbe mwingine unaoweza kufunguliwa.

  Asanteni madaktari
  Madaktari asanteni kwa kuliamsha taifa na kutukumbusha kuwa kuna gharama katika kuleta mabadiliko. Gharama ya majina, hadhi, na sifa zetu; kuna gharama ya nafsi zetu na kwa kweli kabisa kuna gharama kwa watu wengine vile vile. Mmetuonesha kile tulichokiona sehemu nyingine duniani - mabadiliko yana gharama kubwa - kuna watu watapoteza kazi, wapo watakaochukizwa na wapo wengine watapoteza hata maisha yao. Niliandika wiki iliyopita kuhusu Steve Biko na kuonesha kuwa alilipia gharama kubwa ya uhai wake kwa kuwaamsha vijana wa Afrika ya Kusini! Mmefanikiwa katika kilichoshindikana - kuiambia serikali haiwezi kutawala kwa mabavu na dharau!

  Ni matumaini yangu watawala wetu wamejifunza jambo kidogo katika hili - wawe na haraka ya kutatua matatizo badala ya kutafuta namna ya kulindana na kubebana na kutetea vitumbua vyao. Kwa sababi, kama madaktari wameitikisa kidogo serikali hivi, itakuwaje endapo mgomo mkubwa zaidi utakuja kufanyika? Kuna mistari imechorwa na sasa imeanza kuvukwa. Wasiwalazimishe na wengine kuvuka kwani wasipoangalia nchi kweli kabisa itaishi kutoka mgomo na kashfa hadi mgomo na kashfa nyingine na hivyo kuzidi kujidhoofisha.

  Walioathirika wapewe pole kweli
  Wapo walioathirika sana na mgomo huu na kwa kweli kila Mtanzania kwa namna moja au nyingine ameathirika. Wapo ambao tumesupport mgomo huu tukijua kabisa kuwa ndugu zetu wanatakiwa kwenda hospitali huko huko na wengine wamepoteza jamaa zao wakati wa mgomo huu. Kama nilivyosema mwanzoni madaktari hawakutakiwa waachwe wagome, na kwa vile ni wanasiasa ndio waliowaacha madaktari wagome ni wao wanasiasa wanabeba lawama zote za madhara ya mgomo huu kwani kama wameweza kuuzimisha kwa kikao cha masaa machache Ikulu wangeweza kufanya hivyo Januari! Hawakufanya na matokeo yake ni haya yaliyotokea.

  Kikwete akubali kuwajibika kwa yote yaliyotokea
  Kama nilivyosema juzi, namna pekee ya kuanza kwa usahihini kwa Rais kukubali kubeba lawama za mgomo huu wote kuanzia mwanzo hadi hivi sasa. Kama Rais alipaswa kuingilia kati mara moja na ugoigoi wa kufanya hivyo ndio umefikisha hapa tulipofika. Hawezi kukwepa lawama na hana mwingine anaweza kushare naye lawama hizo. Na tunarajia kuwa atawawajibisha hawa viongozi na wakati huo huo kupanga mkakati wa nguvu wa kuboresha sekta ya afya.

  Kwa kukubali kusitisha mgomo baadaya kukutana na Rais madaktari wametuonesha nani anastahili kuwajibika. Natumaini naye amejitambua hivyo.

  MMM-BGM
   
 9. W

  We know next JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  MM Tumekusoma na imetulia na kututuliza roho. Nilisema ktk post yangu moja kuwa hawa madaktari wamekuwa "Agent of Change" kwa niaba ya watanzania wote bila kujali itikadi zetu wala professions zetu. Kwa kweli, wametuwakilisha vyema.
   
 10. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Madaktari wamefanya kitu kikubwa sana kwa kuwaamsha watanzania na pia wametuma ujumbe mzito na wa ukweli kwa raisi kikwete. Wasiwasi wangu ni kama kikwete atazingatia tamko la madaktari juu ya wateule wake.
   
 11. S

  SirBonge JF-Expert Member

  #11
  Mar 10, 2012
  Joined: Jul 18, 2010
  Messages: 349
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 60

  Marekebisho kidogo mkuu!
  Mzee Mwanakijiji, tamko la kusitisha mgomo sio kufuatia Amri ya Mahakama Bali ni kuheshimu Madaraka ya Mkuu ya Nchi
   
 12. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #12
  Mar 10, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Nimewapenda madaktari. Lazima tujue tunataka nini na kukisimamia no matter what!
   
 13. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #13
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Sijui ni kwa nini kulikuwa na kusudio la kukutana na wazee (wa ccm).

  Tunajua rais ni mtu wa maneno matamu na mjuzi wa kutoa ahadi, kwenye hili la madaktari ujanja huo hautamsaidia. Madaktari wameonyesha msimamo thabiti na hawakujiingiza kwenye jazba hata pale waziri mkuu alipokuja na hoja za kushambulia watu binafsi.

  Ni wakati wa rais kutenda na ionekane hivyo kwa wasaidizi wake
   
 14. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #14
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  The Following User Says Thank You Mzee Mwanakijiji For This Useful Post.
  Sigma
  (Today)
   
 15. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #15
  Mar 10, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Mimi sikuunga mkono mgomo wa kwanza wa madaktari na de facto na huu wa pili sikuunga mkono. Ila kuna kitu kimenishangaza zaidi kwenye huu mgomo wa pili: hivi nani aliwashauri madaktari wampe ultimatum mtu ambaye hawajawahi kukaa naye mezani kwenye majidiliano? Mimi nilitegemea madaktari kwanza wangeomba kukutana na Rais wamweleza kumkataa kwao waziri na naibu wake face to face, then kutokana na responce yake ndio wangekuja na reaction. Sasa wao wamereact mahali ambapo hakukuwa na action! Utampaje Rais taarifa ya kutaka atengue uteuzi wake kwa kupitia vyommbo vya habari? Je, viongozi wa mgomo walimuandikia Rais barua ya kumtaka afukuze kazi mawaziri? Rais hafanyi kazi kwa kutumiaa vyombo vya habari. Mimi nadhani madaktari wakubali tu kuwa hawakupata ushauri unaotosheleza kujenga hoja madhubuti na kwamba utatuzi wa kweli utapatikana iwapo watajikaza "kiume" na kufuatilia madai yao hatua kwa hatua, haya mambo ya ultimatum no no no...
   
 16. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #16
  Mar 10, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni kwamba kuna Watanzania wengi ambao hawajawahi kuwa katika mazingira ya mgomo au kusigana na dola. Hawa hawaelewi uzito wa jambo hilo na wanajiongelea tu, utadhani ni jambo rahisi kama kukariri wimbo wa mwanamuziki maarufu.

  Naomba watu watambue kwamba kitendo cha kusimama hadharani na kupingana na dola kwa hoja (hata gama madai yanayopiganiwa ni genuine), ni kinyume na mafunzo na malezi yetu ya toka enzi za ujamaa. Ni jambo zito sana. Linahitaji ujasiri na wote wanaojitolea kuongoza jitihada kama hizi wanatakiwa kupewa standing ovation, pamona na kwamba matokeo yanaweza yasionekane kama wengi walivyotegemea.

  Pia kuna lugha maalumu za kuweka hitimisho la matatizo bila kusababisha trauma kwa upande wowote. Hili ni muhimu ili kuweka mazingira ya kuonesha kwamba walau kwa muda huu tatizo limefikia hatua ya kumaliza mgomo.

  Tamko la Madaktari ni zito na kuna watu wengi (hata baadhi ya madaktari) ambao hawatalielewa!! Hawa wajipe muda ili waweza kuelewa badala ya kulichukulia kwa jaziba!

  Babu DC!!
   
 17. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #17
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hilo la mahakama kuu, lilikuja kwenye majadiliano kati ya Kikwete na madaktari.
  Madokta walimuambia Kikwete categorically kuwa hawaiogopi mahakama kuu kwani wanajua mgomo si halali na bado wamegoma.
  Kikwete mwenyewe aliwaambia kwamba waachane na mahakama kuu "hii ni kati yangu mimi na nyinyi" nukuu ya JK
   
 18. P

  Paul S.S Verified User

  #18
  Mar 10, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu Gad ONEYA
  Mkandara ametumia falsafa kubwa sana hapa kuzingatia na unyeti wa taaluma husika na impact ya mgomo kwa wananchi
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Mar 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  Hapana siyo kuheshimu madaraka ya mkuu wa nchi kwani hakuna mahali popote ambapo Ikulu iliwataka madaktari kurudi kazini mara moja bali mahakama ndiyo imefanya hivyo?
   
 20. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #20
  Mar 10, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Nani angewapa madaktari access ya haraka kiasi hicho ya kumuona Rais? Kwa bahati mbaya wafanyakazi wengi wa umma hasa wa maeneo nyeti, wamejaa viburi na dharau na mara nyingi wanaamini wana majawabu ya mambo yote yanayoihusu Tanzania. Madaktari vichwa vyao viko safi. Waligundua kulikoni kuwapigia magoti watu wasiostahili, kama noma na iwe noma. Tusidanganyane hapa, viongozi wengi wa umma hawana huruma kabisa na Taifa hili pamoja na watu wake. Ndo maana wanafanya mengi yanayowadhulumu na kuwahujumu watu maskini. Sikubaliani kabisa na hoja kwamba makosa wanayo madaktari tu. System nzima imeoza inahitaji marekebisho
   
Loading...