Asanteni kina dada wa mikoani

Mhdiwani

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
650
707
Ni maajabu kwangu lkn pia sjaamini sana hili tukio
Lkn mpk nimeamini
Kilichofanya nisiamini ni kutokana na kuzoeshwa vibaya na dada zetu wa dar,,,,,

Nahitaji ushauri wenu wadau kuhusu hili tukio ,,,

Mimi nilikua dar sasa katikati ya mwaka huu nikaletwa mbeya kuna kazi naendelea nayo
Ktk harakati zangu za kutimiza majukumu yangu
Nilikutana na dada mmoja maeneo ya kiwira sasa kama mnavyojua sshv mvua zinanyesha kwa wingi
Nilikua na mwamvuli ikabidi nijifunike nae kwa bahati mbaya yeye alikua anaenda mbali kidogo ikabidi nimuachie mwavuli wangu
Lkn nikampa namba ili Siku akipita mtaani kwetu anipitishie

Hakuwahi kunipigia na nilimpa namba yangu yake sjachukua ,
Sasa Jana kanipigia asubuhi akajitambulisha hlf akaniomba tuonane jioni ya Jana jmosi
Akasisitiza kua amenialika nkamwambia poa

Ilipofika jioni akanipigia cm tena nikamuuliza nije maeneo gani
Akanielekeza ni maeneo ya tukuyu

Nikajikoki nikaenda kufika hio sehem akawa hajafika ila akaniambia we agiza unachitumia nakuja sshv,,
Basi nkaagiza bia moja kabla sjamaliza akatokea akiwa na rafiki yake ,, tukasalimiana pale na kutambulishana then tukaendelea na story za kawaida

Akaagiza nyama na ndizi za kutosha kwakweli nilikunywa na kula mpaka nikawa natambaa ikabidi nikodiwe usafiri nikarudishwa home
Sasa tangu asbh nawaza hv yule Dada ni MTU kweli au anataka roho yangu? Tangu asbh ananipigia na kunitext ikabidi nizime simu
Mi siamini kama huku mkoani kuna watu wa namna hii kwasababu kule dar tunanyongwa sana,,

Naombeni ushauri wadau huyu dada nimpotezee au kwasababu ananiambia anapenda kua karibu na mimi sasa kwa staili hii ntarudi dar kweli
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom