Asanteni JF kwa ushauri wenu = Hakimu 'wa Liyumba' atupwa mkoani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Asanteni JF kwa ushauri wenu = Hakimu 'wa Liyumba' atupwa mkoani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ng'wanza Madaso, Sep 21, 2009.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hakimu 'wa Liyumba' atupwa mkoaniNI ALIYEMPA DHAMANA YA SH882M KATI YA SH55BILIONI
  HAKIMU Hadija Msongo, aliyewahi kutoa dhamana katika mazingira ya utata kwa mtuhumiwa Amatus Liyumba, amehamishwa kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kupelekwa mkoani Pwani.

  Uamuzi huo wa Ofisi ya Jaji Kiongozi kumhamisha hakimu huyo, umetolewa katika kipindi ambacho mahakama ya Kisutu imekuwa ikiangaliwa kwa karibu na Watanzania wengi, kutokana na kuwa sehemu kuu ya usikilizaji wa kesi nyingi za ufisadi.

  Msongo alimpa dhamana Liyumba Februari 17 mwaka huu, kwa kutumia hati moja moja ya nyumba ya Liyumba yenye thamani ya Sh882 milioni huku hati nyingine zikiendelea kuhakikiwa baada ya ofisa huyo mwandamizi wa zamani wa Benki Kuu (BoT), kutakiwa kutoa dhamana yenye thamani ya Sh55 bilioni.

  Liyumba alipewa dhamana hiyo wakati akiwa ameshtakiwa kwa mara ya kwanza kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi, yaliyoisababishia serikali hasara ya Sh 221 bilioni, ambazo ni tofauti ya gharama halisi ya ujenzi wa majengo ya minara pacha kwenye makao makuu ya benki hiyo ,kulinganisha na gharama inayodaiwa kukuzwa kifisadi.

  Kwa mujibu wa habari za kuaminika, uhamisho wa hakimu huyo umekuwa kama adhabu kutokana na kufanya uamuzi wa dhamana hiyo, ambayo pia ilihusisha hati ya kusafiria iliyoisha muda.

  Hata hivyo, Jaji Kiongozi Fakhi Jundu aliliambia gazeti hili ofisini kwake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba, uhamisho huo ni sehemu ya utaratibu wa kawaida tu.

  Akitoa dhamana hiyo, Msongo ambaye baadaye alijitoa kwenye kesi hiyo, alisema hati nyingine 10 zilizokuwa zimewasilishwa na Liyumba kwa ajili ya dhamana, ziendelee kuhakikiwa na mahakama.

  Hata hivyo, hati hizo zilipingwa na upande wa mashtaka kutokana na baadhi kuwa mali zinazohamishika kama ng'ombe, kuku na matrekta.

  Baada ya kutolewa kwa dhamana hiyo, upande wa serikali ulidai kutoridhishwa na uamuzi huo. Jalada la kesi hiyo lilitakiwa Mahakama Kuu na siku iliyofuata wadhamini wa Liyumba walikamatwa na kushikiliwa mahakamani.

  Mahakama hiyo ilifuta dhamana hiyo Februari 24 na Hakimu Msongo alijitoa kusikiliza kesi hiyo Machi 20. Kesi hiyo sasa inasikilizwa na Hakimu Wariyalwande Lema.

  Lakini Jaji Kiongozi Jundu alisisitiza kwamba, uamuzi wa kumhamisha hautokani na adhabu ya kutoa dhamana hiyo kwa Liyumba.

  "Ni uhamisho ambao umefanyika chini ya utaratibu wa kawaida, kwa maana hata barua yake haisemi kwamba, amehamishwa kutokana na kutoa dhamana kwa Liyumba," alifafanua.

  Alisema ni kweli uamuzi huo ulifanyika baada ya dhamana hiyo, lakini haukuwa adhabu na kwamba, kazi ya kuadhibu hufanywa na jopo maalumu la nidhamu la mahakama.

  Jundu aliongeza kwamba, mahakama ina utaratibu wake wa kufanya uhamisho kila mara ili kuweza kuongeza tija na ufanisi katika mahakama zake mbalimbali nchini kote.

  Lakini habari ambazo Mwananchi imezipata zinasema kuwa, hakimu huyo alihamishwa kwa lengo la kumwondoa mahakamani Kisutu, ambako kesi nyingi za ufisadi zimekuwa zikipelekwa.

  Kwa mujibu wa habari hizo, upande wa serikali ulichukizwa na maamuzi hayo ya kumwachia Liyumba ambaye alishinda kesi ya awali kutokana na hoja za kiufundi, lakini akafunguliwa tena kesi baada ya serikali kurekebisha hati ya mashtaka.

  Hadi sasa Liyumba yuko ndani baada ya majaribio yake yote ya kutaka sheria imuokoe na kiwango kikubwa cha dhamana kugonga mwamba. Baada ya kushtakiwa upya akiwa peke yake, Liyumba sasa anatakiwa kuwasilisha dhamana yenye thamani ya zaidi ya Sh100 bilioni.

  Wanasheria wake walifanikiwa kuishawishi mahakama kuwa, kipengele kinachotaka mtuhumiwa atoe dhamana yenye thamani ya nusu ya fedha anazodaiwa kuiba, hakitakiwi kutumika kwenye kesi ya kigogo huyo wa zamani wa BoT kwa kuwa hashtakiwi kwa wizi.

  Mahakama ilipunguza kiwango hicho cha dhamana hadi Sh300 milioni. Lakini siku ambayo alitakiwa kuachiwa huru, upande wa mashtaka haukuwa tayari kuhakikisha hati za mali na hivyo kusababisha aendelee kukaa mahabusu.

  Baadaye upande wa mashtaka ulikata rufaa Mahakama Kuu, ambayo iliagiza tena kuwa mshtakiwa awasilishe dhamana ambayo ni nusu ya mali anayodaiwa kuisababishia serikali hasara.

  Hata hivyo, wanasheria wa Liyumba bado hawajanyoosha mikono juu kukubali kushindwa katika kuhakikisha mteja wao anakuwa nje kwa dhamana. Wiki moja iliyopita alishindwa kujitokeza mahakamani baada ya kuelezwa kwamba alikuwa mgonjwa huko mahabusu anakoshikiliwa hadi sasa.


  Source: Tanzania daima
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Angehamishiwa Tandahimba ama Kigonsera , hapo Pwani mbona bado yuko mjini?
   
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  Sep 21, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Ndugu wacha kuchonganisha jukwaa la jamii na huyo jaji ulichofanya ni kibaya sana kama mada umetoa kwenye gazeti weka kama mada ilivyo usibadili chochote , unavyosema jf kama vile jf ndio imehusika katika mchakato wa kuhamishwa huyo mtu kwa namna moja au nyingine huu ni uchanganishi hatutaki hivi kama ina husika tungeona tamko lake rasmi
   
 4. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Yaani Tandahimba ndiko wanakotupwa wala rushwa au?

  Unawashushia hadhi wakazi wa wilaya hii, kwani wao si watu?
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ila Pwani ndiko wanakofaa wala rushwa? Mazee una ID ngapi hapa JF hahahah!
   
 6. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Nani kasema Pwani wanafaa wala rushwa? Mimi sikusema hivyo.Mimi nina attack assertion yako kwamba kumpeleka mtu Tandahimba ni "adhabu" sawia kwa mtu mla rushwa, umeifanya wilaya ya Tandahimba kuwa kama gereza na mwenyewe umeridhika kabisa.Ndiyo maana nakuonyesha kwa kuhalalisha Tandahimba kuwa jaa la kutupa wala rushwa, unakuwa huwatendei haki wananchi wa wilaya hiyo.

  Granted inawezekana kabisa kwamba huko ni vijijini mbali na mjini, lakini hii ndiyo iwe sababu ya kuwatupa wala rushwa huko? Keshokutwa wakitaka huduma bora za jamaii mtakataa kwa sababu "kumejaa wala rushwa"?.Wakishindwa kuendelea hata kidogo kujinasua na hiyo vicious cycle of poverty mtakubali kwamba hizi tabia za kuzifanya hizi peripheries za nchi yetu ziwe ndiyo Siberia yetu zinachangia?

  C'mon man, kubali umechemsha.
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Soma tundiko zima kuanzia juu.....vinginevyo mwandishi wa habari yote hii amechemsha. Na si mimi if that will make you happy!
   
 8. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Any way you cut the below comment, it is disgraceful regardless of what is in the article. The entire idea that some parts of our country are better and more deserving than others reeks of black on black apartheid and Bantustanism.

   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Be happy with yourself! Hakuna ugomvi dogo....
   
 10. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  This level of contentedness with mediocrity and an allergic revulsion to any thought provoking analysis, coupled with an unhealthy degree of egoism is exactly what got us as a country where we are.

  If I were you, to save face and maintain a credible level of civility I would apologize to the good people of Tandahimba and gracefully bow out.

  How can I be "happy with myself" while the seeds of division are planted to divide citizens of my country into ridiculous classes right in from of my eyes?

  Funny that you can tell somebody is "dogo" over the net, especially if the "dogo" in question is demonstrating intellectual maturity pegged light years ahead of your nonchalant mental debauchery.

  Mi ndo maana nakataa hiki kilemba cha ukoka cha "Great Thinkers", not unless we at least adopt the humility to accept when we are wrong.
   
 11. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Sioni sababu ya kukwaruzana katika hili nadhani suala hapa liwe mtu akinyimwa dhamana ndio iwe ajabu lakini akipewa dhamana hakuna kitu cha ajabu kwani katiba yetu inaruhusu kabisa sioni tabu kabisa.

  sikumbuki kama JF waliwahi kutoa ushaurikuwa hakimu huyu ahamishwe sidhani kabisa,
   
 12. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Watu inabidi tujifunze due process, watu hawajui kwamba dhamana ni haki ya kisheria na default ni mtu kupewa dhamana, prosecution inabidi ifanye kazi kuonyesha kwamba wewe ni flight risk au kuna tishio kwa maisha yako ili unyimwe dhamana.

  Sasa hapa tunakuja na witchunts zinazotaka shortcuts bila hata kuelewa mfumo wa sheria unasemaje.
   
 13. O

  Ogah JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Unaweza kutusaidia JF walitoa huo ushauri katika mada ipi?
   
 14. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #14
  Sep 21, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Ndugu tukiendeleza mada za hivi itakuwa hatari sana watu kujadili hoja , mod tunaomba ubadilishe jina la thread na huyo mwanachama aombe msamaha mara moja kwa kutenda makosa hata kama ni bahati mbaya iwe fundisho kwa wengine - hii inaweza kucost wengine hapo baadaye
   
 15. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Maoni ya wana JF na wengineo yamechangia kwa huyu hakimu kuhanishwa kituo cha kazi
   
 16. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #16
  Sep 21, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  huyu hakimu hakuwa pekeyake katika ile kesi sasa inakuwaje msalaba abebe peke yake
   
 17. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #17
  Sep 21, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Soma thread inayoitwa {Amatus Liyumba:Balaa} anzia page ya 27 na kuendelea anzia maoni ya Scientist.
   
 18. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Usijifanye unajua sana kila kitu sitaomba msamaha kwa sababu nina uhakika kuwa tulimjadili huyo hakimu hapa JF. Soma thread inayoitwa {Amatus Liyumba:Balaa} anzia page ya 27 na kuendelea anzia kusoma maoni ya Scientist.
   
 19. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #19
  Sep 21, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Yaliyotendeka mwezi wa pili huwezi kuyajua kwani wewe bado mchanga sana humu ndani. Hii kauli ya kuwa hukumbuki kuwa JF WALIWAHI KUJADILI HILI SWALA niya ajabu sana ambayo sikuitegemea kutoka kwako waachie kina shy wabishi waendelee kubisha.
   
 20. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #20
  Sep 21, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wakuu
  Hivi Tanzania hakimu kama amekosea katika kuamua haki hafukuzwi kazi kwa sababu tuna shida ya mahakimu basi anahamishwa tu au?
   
Loading...