Asanteni jf doctors members

ROKY

Senior Member
May 4, 2011
182
70
Ni muda kidogo umepita tangu niliposoma post ya Natalia(kama sikosei)akiomba ushauri kuhusu kupunguza uzito,watu wengi walichangia mengi,mimi pia yamenisaidia sana na nasema asante kwa mawazo yenu.nilisumbuliwa sana na uzito mkubwa na jitihada za kupunguza zikawa zinanichosha kwa kuona sipungui,kama mwezi hivi umepita nilipata kichomi ndani ya kifua upande wa kulia,nikaenda hospitali,nikapima kila kitu kipo sawa isipokuwa uzito,dokta akanishauri niache kula mlo wa usiku jambo ambalo nililizingatia na kuamua kuchukua wazo la member mmoja(bahati mbaya simkumbuki jina),yeye alisema ukitumia maji ya moto unaweka asali vijiko viwili na limao unakunywa asubuhi,saa nne,saa saba,saa kumi na saa mbili usiku,nimefanya hivyo na nimeacha kula usiku nimefanikiwa kupunguza kilo nne ndani ya mwezi mmoja,najua ni kilo chache lakini kwangu ni hatua kubwa.
Asanteni sana jf members,asante wewe ulie toa ushauri katika post ile ya natalia.
Tuendelee kuelimisha.
 
Jf ni kila kitu! Acha wanaoipond hadharani huku gizani wakiifurahia wafanye hivyo! God bless jf members.
 
JF iko juu' mimi ninaikubali, imekuwa mkombozi, kusema kweli tunajifunza mengi na kuelimika kupitia hapa jukwaani. Big up JF.
 
Jf ni kila kitu! Acha wanaoipond hadharani huku gizani wakiifurahia wafanye hivyo! God bless jf members.

Unadhani kunaanaye iponda jf basi...Ni ukweli mchungu ndo huwa unawaumiza lakini nakuhakikishia hao wanaoichukia jf hawalali bila kuchungulia humu..
 
Wengi waleta mada(wagonjwa, waomba ushauri, n.k), hawaleti majibu juu ya ushauri wanaopewa(ukiacha wale wa PM), ingekuwa vizuri/vyema kuleta feedback na personal experience kuliko kuingia mitini.

This is a good start ROKY, goodluck.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom