Asante Wananchi wa Arumeru kwa Zawadi Nzuri ya Pasaka Mliyotupatia Watanzania. Mungu Awabariki!

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
Ndugu zangu wanaArumeru,

Kwanza, nianze kwa kuwapongeza wananchi wa Arumeru kwa kazi nzito ya kupiga kura na kufuatilia kwa ukaribu wa uhesabuji na kuzuia kabisa mbinu chafu za kubadili matokeo na hatimaye kumwezesha kijana wenu na chaguo lenu kupata ushindi. Ushindi uliopatikana siyo wa chedema bali ni wenu wenyewe. Ninachotaka kuwahakikishia wanaArumeru ni kwamba mmechagua ushindi. Ushindi dhidi ya ccm ni ushindi dhiti ya ufisadi na ni ushindi dhidi ya umaskini. Kila mtanzania mpenda amani, mshikamano na maendeleo kwa sasa anatambua wazi kwamba kuichagua ccm maana yake ni kuchagua kushindwa jambo ambalo ningewashangaa sana mngefanya hivyo. Sasa, shirikianeni na kijana wenu katika kujiletea maendeleo yenu.

Pili, nimpongeze Meneja wa Kampeni, viongozi wote wa chadema, wanachama na wapenzi wote kwa ujumla wao ndani na nje ya nchi kwa jitihada zao zilizowezesha kupatikana kwa ushindi. Najua kazi imefanyika kubwa lakini kubwa zaidi ni mshikamano wenu wakati wa kampeni. Ushindi huu iwe ni chachu ya ushindi mkubwa wa uchaguzi wa 2015 na watanzania wengi ndiyo tunaousubiri kwa hamu kubwa.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa.
 
Mkuu ni kweli tumshukuru Mungu kwani ukombozi wa nchi yetu ni dahiri sasa sio tena ndoto kama tulivyoanza miaka ya 1992. Nami naungana nawe kuwashukuru Wameru woote kwa ujasiri wao,
 
Hii safi sana, ukombozi wa nchi yetu umekaribia sana! Hongereni sana wana wa Arumeru.
 
leo nimekaa class saaaaaaafi wala sina stress......jamani mwigulu nchemba,nape wamejificha wapi....na yule mzee wa matusi maana matusi yake hata kwenye dictionary ya shetani sijui kama yapo!!!!!!!!kweli mungu anaipenda tanzania.....kawaletea wana arumeru mwana "mumtunze".....

MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI AFRIKA,MUNGU IBARIKI CHADEMA...
 
WanaArumeru wametupa zawadi nzuri ya mwaka, na Pasaka pia itakuwa njema mno safari hii!
 
kwenye chaguzi zote zilizo fanyika jana na kukipatia ushindi CHADEMA
nizawadi tosha ya PASAKA nidalili ya kuelekea kuchukua dola mwaka
2015 Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Chadema - Aman
 
Back
Top Bottom