Asante wajumbe wa CCM wilaya ya Rorya: Magufuli tunaomba uturudishie Japhari Chege

OBWERE

Member
Jan 14, 2011
46
8
na Mwl Matete - MUST

Nipende kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM wilaya ya Rorya kwa kazi kubwa waliofanya kutuletea mshindi ambaye kwa maoni yangu ni mtu sahihi kwa wakati huu. Kura ya maoni iliyofanyika wiki iliopita ni wazi kuwa hata wajumbe walichoka siasa za ukabila na utarafa ndani ya wilaya ya Rorya.​

Nimpongeze mshindi wa kura ya maoni ndugu yangu Japhari Chege Wambura, ni kweli amewashangaza wengi kwa kumbwaga yule alitegemewa na kujihakikishia ushindi kwa kumwaga hela kwa wajumbe lakini bado wajumbe waliona hatoshi kuliongoza jimbo la Rorya. Tulilalamika sana kuhusu mtia nia huyu kwa kutoa rushwa tena hadharani na hakuona aibu mpaka wananchi walikuwa wakiimba MSHAHARA.... MSHAHARA wakiona gari lake.​

JAPHARI CHEGE WAMBURA (JCW) ATAMSHINDA EZEKIA DIBOGO WENJE (EDW)

Kwa maoni yangu katika uchaguzi wa wabunge (sio madiwani na Urais) JAPHARI CHEGE WAMBURA ataipa ushindi CCM wilaya ya Rorya kwa kumbwaga WENJE, kuliko akipewa nafasi hio Francis Genga Olwero (FGO) zipo sababu nyingi sana lakini kubwa kuliko ni mgawanyiko uliopo wa kikabila na kitarafa uliopo katika jimbo la Rorya.​

Kwanini JCW atamshinda EDW?
Maoni yangu:​
1. Ni dhahiri na ni wazi kuwa wananchi wa tarafa ya Suba wametafuta nafasi hii ya kupata mwakilishi kutoka kwao kwa muda mrefu kwahio hawatafanya kosa iwapo jina la JCW litarudishwa na CCM hivyo tarafa ya Suba ni eneo na ngome kuu ya JCW hivyo kwa maoni yangu:​
JCW atapata 95%
Kwa sababu ni ngome yake imara​
EDW nampa 05%
Hizi asilimia nampa kwa sababu ya uwepo wa watu wenye asili ya Nyancha kule Suba​

2. Tarafa ya Nyancha
Tunategemea iwe ngome ya EDW kura za Wenje zipo kata ya Mkoma, Nyahongo, Tai, Raranya, na nampa 75%​
- kwasababu ni eneo lake la makazi na ukoo wake wote unapatikana kwenye maeneo hayo​
- wakati JCW nampa 25% kata hizo​
JCW atashinda kata ya Nyamtinga, Kinyenche, Kirogo, Kigunga, Nyamagaro, Kyangasaga​
- Kwasababu, moja ni maeneo na ngome ya CCM na upinzani haijawahi kushinda kwenye kura za ubunge na urais katika chaguzi zilizopita na pili uwepo wa makabila yenye lugha nasaba na kisimbiti. Wapo wakine, wasweta, wahacha, wasurwa, .......ambao watamuona JCW kama mtu wao anaeongea lugha yao (na iwapo JCW atawasalimia kwa Kisimbete atakuwa ameteka hadhira) hivyo ni ngumu sana kwa EDW kushinda:​
JCW nampa 65%​
EDW nampa 45% kwenye kata hizo​
- Kata ya Bukura ni ujumbani kwa JCW (kijiji cha Nyahera) hivyo ni dhahiri atapata kura za kutosha Nyahera na Nyambori​
Hapa nampa JCW = 50%
EDW= 50%

3. Tarafa ya Girango
Kwa maoni yangu JCW atamshinda vizuri sana EDW kata ya Bukwe, Mirare na Koryo​
- Kwasababu moja ni uwepo wa LOA maeneo hayo na kama ilivyo ada ya CCM atatumia nguvu zake zote kumpatia ushindi JCW​
- Kata tajwa hapo juu ni ngome imara ya CCM​
- Ni ngumu sana kwa EDW kushinda maeneo hayo:​
JCW nampa 70%
EDW nampa 30%
- Ushindi wa EDW utatokea kata ya Ikoma, Goribe na Kitembe​
- kwasababu ya mchango wa Stephen Owawa (lakini itategemeana na hasira za wafuasi wa Owawa kama watatulizwa wasilipize kisasi ya kushindwa kwenye kura ya maoni CDM)​
JCW nampa 25%
EDW nampa 75
- Kata ya Roche naiweka pembeni kwani ni eneo la Charles Ochelle Ombuto (COO) ambaye ni mwenyekiti wa CCM wilaya lakini taarifa zilizopo ni kuwa hakubaliki saaana kwenye kata yake ya Roche hivo utabiri wangu ni:​
JCW nampa 50%
EDW nampa 50%

Tarafa ya Luo imbo
Hapa ndiyo kura za maamuzi zitatokea. Kama Francis Genga Olwero (FGO) hatorudishwa basi tutegemee pengine Luo-imbo wakapiga kura za maruhani. Lakini kama ilivyo ada ya CCM aliyeshindwa kwenye kura ya maoni ni lazima amsaidie mshindi kufanya kampeni. Bahati nzuri tarafa ya Luo-imbo ina wapiga kura wachache sana hivyo nampa EDW ushindi kiduchu.​
- Pia mgogoro wa ardhi kati ya Luo-imbo na Suba inaweza kumkosesha kura JCW​
JCW nampa 45%
EDW nampa 55%

JUMLA KUU ...JCW = 50.71% EDW=49.29%

KWANINI JINA LA JAPHARI LIRUDI NA SIO OLWERO GENGA
1. Kwa maoni yangu iwapo CCM itafanya makosa ikarudisha jina la Olwero na kumkata Japhari basi tutegemee Wenje kushinda ubunge kwa kishindo labda itokee na itumike nguvu za ziada. Tutegemee watu wa Suba na Nyancha wote kuungana kumchagua EWD kwani watakuwa wamethibitishiwa zile hisia kuwa hawatakiwi kuwa na mbunge kutoka maeneo yao.​

2. Wenje na kundi lake watapata hoja ya kuwaaminisha wapiga kura ile dhana ya ukabila na utarafa uliojengeka katika jimbo la Rorya​

3. Olwero anahusishwa na kundi la G6 hasa LOA ambaye hakubaliki kwa lolote tarafa ya Nyancha hasa kata ya Mkoma, Raranya, Bukura,Tai, Kinyenche, Nyahongo nk na hata tarafa ya Suba LOA hana mvutano bila hela zake. Hivyo hoja ya LOA kulazimisha kurudi kwa jina la Olwero hasa kwa kuandikiwa taarifa nzuri kutoka wilayani na mkoani itakayoishawishi NEC itakuwa imepata nguvu na ilikulinda biashara zake​

WITO WANGU
- Namuomba Mhe JPM arudishe jina la JCW kama CCM inahitaji ushindi mwepesi na wa kishindo jimbo la Rorya​
- Tuache siasa chafu ambazo zinapikwa dhidi ya mshindi wa kura ya maoni. Hoja kama hajui kijaluo hayana msingi maana hatutafuti mwl wa lugha ya kiluo.​
- Tuache tuhuma za rushwa kama hatuna ushahidi wa kutosha maana tunajua waliohusianishwa na kutuhumiwa kutoa rushwa kubwa kubwa na ni wao baada ya kushindwa uchaguzi wanaleta siasa za kuchafuana ili mwenzao akose nafasi hio.​
- Tuache kuwahusianisha Wasimbete na uwizi wa mifugo kama inavyopotoshwa kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili ya kumchafua JCW. Maana hakuna ng'ombe iliyowahi kuibwa tarafa ya Nyancha, Girango au Luo-imbo na kupatikana tarafa ya Suba. Sote tunajua wezi wa mifugo wanatokea wapi na wanaoshirikiana nao!!!​

TUACHE SIASA ZA MAJI TAKA TUMSUBIRI PIA LUIGI COLINA YUKO NEC

Maoni​
+255 752 761116
 
Kura ya maoni iliyofanyika wiki iliopita ni wazi kuwa hata wajumbe walichoka siasa za ukabila na utarafa ndani ya wilaya ya Rorya.
pili uwepo wa makabila yenye lugha nasaba na kisimbiti. Wapo wakine, wasweta, wahacha, wasurwa, .......ambao watamuona JCW kama mtu wao anaeongea lugha yao
Duuh Ni ngumu sana, Umeanza kwa kusema kwamba ukabila, lakini as you proceed to explain naona ukabila umeshamiri haswaaa...!! Yaan nyie ndio mnatufanya wazungu huku watubague tupigwe Risasi, Kumbe ubaguzi unaanza na nyinyi wenyewe.

Uchambuzi wako umejaa ukabila brother; Anyway ni maoni yangu binafsi.
 
na Mwl Matete - MUST

Nipende kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM wilaya ya Rorya kwa kazi kubwa waliofanya kutuletea mshindi ambaye kwa maoni yangu ni mtu sahihi kwa wakati huu. Kura ya maoni iliyofanyika wiki iliopita ni wazi kuwa hata wajumbe walichoka siasa za ukabila na utarafa ndani ya wilaya ya Rorya.​

Nimpongeze mshindi wa kura ya maoni ndugu yangu Japhari Chege Wambura, ni kweli amewashangaza wengi kwa kumbwaga yule alitegemewa na kujihakikishia ushindi kwa kumwaga hela kwa wajumbe lakini bado wajumbe waliona hatoshi kuliongoza jimbo la Rorya. Tulilalamika sana kuhusu mtia nia huyu kwa kutoa rushwa tena hadharani na hakuona aibu mpaka wananchi walikuwa wakiimba MSHAHARA.... MSHAHARA wakiona gari lake.​

JAPHARI CHEGE WAMBURA (JCW) ATAMSHINDA EZEKIA DIBOGO WENJE (EDW)

Kwa maoni yangu katika uchaguzi wa wabunge (sio madiwani na Urais) JAPHARI CHEGE WAMBURA ataipa ushindi CCM wilaya ya Rorya kwa kumbwaga WENJE, kuliko akipewa nafasi hio Francis Genga Olwero (FGO) zipo sababu nyingi sana lakini kubwa kuliko ni mgawanyiko uliopo wa kikabila na kitarafa uliopo katika jimbo la Rorya.​

Kwanini JCW atamshinda EDW?
Maoni yangu:​
1. Ni dhahiri na ni wazi kuwa wananchi wa tarafa ya Suba wametafuta nafasi hii ya kupata mwakilishi kutoka kwao kwa muda mrefu kwahio hawatafanya kosa iwapo jina la JCW litarudishwa na CCM hivyo tarafa ya Suba ni eneo na ngome kuu ya JCW hivyo kwa maoni yangu:​
JCW atapata 95%
Kwa sababu ni ngome yake imara​
EDW nampa 05%
Hizi asilimia nampa kwa sababu ya uwepo wa watu wenye asili ya Nyancha kule Suba​

2. Tarafa ya Nyancha
Tunategemea iwe ngome ya EDW kura za Wenje zipo kata ya Mkoma, Nyahongo, Tai, Raranya, na nampa 75%​
- kwasababu ni eneo lake la makazi na ukoo wake wote unapatikana kwenye maeneo hayo​
- wakati JCW nampa 25% kata hizo​
JCW atashinda kata ya Nyamtinga, Kinyenche, Kirogo, Kigunga, Nyamagaro, Kyangasaga​
- Kwasababu, moja ni maeneo na ngome ya CCM na upinzani haijawahi kushinda kwenye kura za ubunge na urais katika chaguzi zilizopita na pili uwepo wa makabila yenye lugha nasaba na kisimbiti. Wapo wakine, wasweta, wahacha, wasurwa, .......ambao watamuona JCW kama mtu wao anaeongea lugha yao (na iwapo JCW atawasalimia kwa Kisimbete atakuwa ameteka hadhira) hivyo ni ngumu sana kwa EDW kushinda:​
JCW nampa 65%​
EDW nampa 45% kwenye kata hizo​
- Kata ya Bukura ni ujumbani kwa JCW (kijiji cha Nyahera) hivyo ni dhahiri atapata kura za kutosha Nyahera na Nyambori​
Hapa nampa JCW = 50%
EDW= 50%

3. Tarafa ya Girango
Kwa maoni yangu JCW atamshinda vizuri sana EDW kata ya Bukwe, Mirare na Koryo​
- Kwasababu moja ni uwepo wa LOA maeneo hayo na kama ilivyo ada ya CCM atatumia nguvu zake zote kumpatia ushindi JCW​
- Kata tajwa hapo juu ni ngome imara ya CCM​
- Ni ngumu sana kwa EDW kushinda maeneo hayo:​
JCW nampa 70%
EDW nampa 30%
- Ushindi wa EDW utatokea kata ya Ikoma, Goribe na Kitembe​
- kwasababu ya mchango wa Stephen Owawa (lakini itategemeana na hasira za wafuasi wa Owawa kama watatulizwa wasilipize kisasi ya kushindwa kwenye kura ya maoni CDM)​
JCW nampa 25%
EDW nampa 75
- Kata ya Roche naiweka pembeni kwani ni eneo la Charles Ochelle Ombuto (COO) ambaye ni mwenyekiti wa CCM wilaya lakini taarifa zilizopo ni kuwa hakubaliki saaana kwenye kata yake ya Roche hivo utabiri wangu ni:​
JCW nampa 50%
EDW nampa 50%

Tarafa ya Luo imbo
Hapa ndiyo kura za maamuzi zitatokea. Kama Francis Genga Olwero (FGO) hatorudishwa basi tutegemee pengine Luo-imbo wakapiga kura za maruhani. Lakini kama ilivyo ada ya CCM aliyeshindwa kwenye kura ya maoni ni lazima amsaidie mshindi kufanya kampeni. Bahati nzuri tarafa ya Luo-imbo ina wapiga kura wachache sana hivyo nampa EDW ushindi kiduchu.​
- Pia mgogoro wa ardhi kati ya Luo-imbo na Suba inaweza kumkosesha kura JCW​
JCW nampa 45%
EDW nampa 55%

JUMLA KUU ...JCW = 50.71% EDW=49.29%

KWANINI JINA LA JAPHARI LIRUDI NA SIO OLWERO GENGA
1. Kwa maoni yangu iwapo CCM itafanya makosa ikarudisha jina la Olwero na kumkata Japhari basi tutegemee Wenje kushinda ubunge kwa kishindo labda itokee na itumike nguvu za ziada. Tutegemee watu wa Suba na Nyancha wote kuungana kumchagua EWD kwani watakuwa wamethibitishiwa zile hisia kuwa hawatakiwi kuwa na mbunge kutoka maeneo yao.​

2. Wenje na kundi lake watapata hoja ya kuwaaminisha wapiga kura ile dhana ya ukabila na utarafa uliojengeka katika jimbo la Rorya​

3. Olwero anahusishwa na kundi la G6 hasa LOA ambaye hakubaliki kwa lolote tarafa ya Nyancha hasa kata ya Mkoma, Raranya, Bukura,Tai, Kinyenche, Nyahongo nk na hata tarafa ya Suba LOA hana mvutano bila hela zake. Hivyo hoja ya LOA kulazimisha kurudi kwa jina la Olwero hasa kwa kuandikiwa taarifa nzuri kutoka wilayani na mkoani itakayoishawishi NEC itakuwa imepata nguvu na ilikulinda biashara zake​

WITO WANGU
- Namuomba Mhe JPM arudishe jina la JCW kama CCM inahitaji ushindi mwepesi na wa kishindo jimbo la Rorya​
- Tuache siasa chafu ambazo zinapikwa dhidi ya mshindi wa kura ya maoni. Hoja kama hajui kijaluo hayana msingi maana hatutafuti mwl wa lugha ya kiluo.​
- Tuache tuhuma za rushwa kama hatuna ushahidi wa kutosha maana tunajua waliohusianishwa na kutuhumiwa kutoa rushwa kubwa kubwa na ni wao baada ya kushindwa uchaguzi wanaleta siasa za kuchafuana ili mwenzao akose nafasi hio.​
- Tuache kuwahusianisha Wasimbete na uwizi wa mifugo kama inavyopotoshwa kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili ya kumchafua JCW. Maana hakuna ng'ombe iliyowahi kuibwa tarafa ya Nyancha, Girango au Luo-imbo na kupatikana tarafa ya Suba. Sote tunajua wezi wa mifugo wanatokea wapi na wanaoshirikiana nao!!!​

TUACHE SIASA ZA MAJI TAKA TUMSUBIRI PIA LUIGI COLINA YUKO NEC

Maoni​
+255 752 761116

Kama unataka arudishwe aliyeshindwa kura za maoni kwa nini wanaccm wanaotoka maeneo yote hayo uliyotaja hawakumchagua huyo kipenzi chako, si walikuwepo kwenye kura za maoni? Subirini mtandikwe fimbo ya kichwa na Wenje kwenye uchaguzi mkuu.
 
Back
Top Bottom