SHIEKA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,244
- 4,258
Nilikuwa navifurahia sana vifurushi vya CHEKA BOMBASTIK vilivyokuwa vikiuzwa na mtandao wa Vodacom. Kipengele cha 'Kwenda Mitandao Yote' kwenye hicho kifurushi kilikuwa mkombozi wangu. Vodacom sijui walipata ushauri kutoka wapi, ghafla wakarekebisha kipengele cha 'Kwenda Mitandao Yote' na kupunguza mvuto wake. Kwa kuwa nahitaji mawasiliano na watu wangu walio kwenye mitandao mingine, nilianza kazi ya kutafuta mtandao mbadala. Tafuta yangu ikanifikisha mtandao wa Airtel. Hawa, wana vifurushi maridadi sana kuliko huko nilikotoka!Vifurushi vya siku ni kwa kila aina ya mfuko, kuanzia sh 399 mpaka 999 unachagua. Mimi hujiunga kile cha sh 999 ambacho unapata dk 40 kupiga mtandao wowote Tz, meseji 1000, na MB 300 za intaneti. Mungu anipe nini zaidi? Voda wasingenitibua, nisengegundua haya mambo ndo maana nawashukuru!